Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania chamtaka Rostam Aziz kuthibitisha tuhuma alizotoa dhidi ya Majaji na Mahakama ya Kisutu

Rostam akathibitishe ukweli kwenye vyombo vinavyotumika kupindisha ukweli? Alichosema Rostam ni ukweli wa wazi.
Hiki chama cha Majaji na mahakimu ni chama cha KINAFIKI sana. Alichosema Rostam ndio ukweli

1. JPM aliposema Serikali ni mhimili uliochimbia chini zaidi , mbona hatukuwasikia hawa Majaji na Mahakimu
2. Kiongozi wao aliposema ' maamuzi yazingatie mihimili mingine' mbona hatukuwasikia
3. JPM alipotunga sheria za kudidimiza haki za watu mbona hatukuwasikia
4. Kesi za watu zina miaka 10 kama zile za Masheikh wakinyimwa haki za kusikiliza, mbona hatukuwasikia
5. JPM alipofanya upuuzi wa plea bargain ikiwa ni dhuluma mbona hatukuwasikia
6. Jaji Mugasha alipotoa angalizo la CJ kuongezewa muda , mbona hatujasikia msimamo wao

Hawa ni wanafiki tu wanaotaka kusikika wateuliwe katika bodi za mashirika na taasisi. Hawa hawana interest na nchi.

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Kuna yule jaji aliewahi sema kati ya vitu ambavyo hawezi sahau ni HUKUMU aliyoandika KUCHANWA CHANWA waziri mkuu mmoja wa hii (wako wengi)

HUKUMU yake iliitwa TAKATAKA na huyo waziri mkuu
Watu wenye pesa na wale wenye madaraka makubwa huwa wanazarau sana Mahakama zetu, na hii imesababishwa na Watumishi wenyewe wa Mahakama kwa kupenda sana kitu kidogo kutoka kwa matajiri hao!!
 
Mbona kasanda kirahisi sana?
Sasa Kama Mtu kapewa mlango wa kutokea( kuomba radhi) unategemea afanye nini!? Majaji walitakiwa wamwambie neno moja tu, nalo ni "Thibitisha" siyo kuambiwa au aombe radhi!!
 

Uko sahihi kabisa. Siku za mwanzo za utawala wa Magufuli alisema kuna majaji wanakula rushwa, na majina yao anayo. Na hata wanaowalipia safari zao kwenda nje ya nchi kwa ajili ya likizo anawajua. Kwa kauli toka siku ile ndio ilikuwa mwanzo wa kuinyamazisha mahakama, na mahakama ikaanza kufanya kama atakavyo Magufuli, na sio sheria zitakavyo.

Huyo Rostam kaongea ukweli, kuanzia Rostam, mahakama pamoja na sisi wananchi, wote tunajua kaongea ukweli. Wanachokifanya mahakama ni kumtishia ili awasafishe, lakini ujumbe umefika kiusahihi kuwa mahakama haziko huru.
 
Tarehe Saba Nane
Ni siku ya Ukombozi.
Mahakama itoe haki, rudisheni mkataba huu Dubai.
 
Kumbe walimshika pabaya huyu muajemi anayejidai ni mtanzania kuliko watanzania halisi. Mtu kama yeye ajishughulishe tu na biashara sio kupanda majukwaani kujidai kutetea wananchi.
Pamoja na faida ya uwepo wafanyabiashara, wengi ni wadhambi kwa kuwadhulumu wanyonge. Kwenye biblia yesu hakukataa uwezekano kuingia mbinguni wafanya biashara wakubwa ila akasema uwezekano wao kuona ufalme wa mbinguni ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
 
Ni mtanzania kama wewe....

Wewe huna utanzania wa kumzidi yeye.....

Baada ya bendera ya UNION JACK kushushwa ule usiku......kila aliyekuwa mkazi wa Tanganyika akawa raia....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…