Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wagombea nafasi ya Uenyekiti kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa Chama cha National League of Democracy (NLD) wamebainisha kuwa zipo kero ambazo watakwenda kuzifanyia kazi kwa maslahi ya wananchi kwani ni za muda mrefu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkutano wao wa hadhara ikiwa ni mundelezo wa kufanya kampeni kwaajili ya kujinadi kwa wananchi wa kata ya Sindeni,wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga wamesema migogoro ya wakulima na wafugaji,kero ya kukosa maji ya uhakika na ile ya kukosekana barabara za mitaa.
Akiwanadi wagombea hao Katibu Mkuu wa Chama cha NLD Doyo Hassani Doyo amesema endapo wananchi watawachagua pia watatafuta dawa ya kukomesha migogoro ya wakulima na wafugaji,kwani imekuwa ni changamoto kwa wananchi.
Doyo amesema "Kama mtatupa lidhaa ya kuwa viongozi katika hiki kijiji mkatuchagulia viongozi serikali mkaibadilisha tuwaahidi ndugu zangu tutakwenda kutengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kukomeaha matatizo ya wakulima na wafugaji kwenye eneo hili",
Mgombea nafasi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Sindeni Athuman Mgaza amesema kero ya kwanza kukosekana maji ya uhakika kwa wakazi wa Sindeni licha ya uwepo wa chanzo cha maji,ila maji yamekuwq yakitoka mara chache sana na kusababisha huduma kuwa ni changamoto.
Amesema taarifa zinadai maji yapo na ni kweli kwenye tanki la eneo hilo kuna maji,ila changamoto maji hayo hayafiki kwa wananchi kama inavyotakiwa,hivyo atashughulikia changamoto hiyo kama watamchagua kuwa mwenyekiti.
"Kama mtanipa nafasi ya kuwa Mwenyekiti nitahakikisha nasimamia wale ambao wamerukwa na huduma ya umeme wa Rea,wanapata na kuendelea na shughuli zao,kwani wengine uwezo wa kulipia umeme wanao ila hawajashushiwa nyaya kwasababu ambazo hazijabainishwa",amesema Athuman
Aidha Omari Madebe ambae anagombea nafasi ya mjumbe wa kitongoji cha Sindeni amesema changamoto ambayo anaona ni kero kubwa ni barabara za mitaa kufungwa kwa wananchi kujenga sehemu ambazo haziruhusiwi na viongozi husika walishindwa kuchukua hatua.