Baada ya katiba mpya kupatikana hiki ni Moja ya chama kitakacho sajiliwa kikiwa na dhamira njema ya kurudisha nguvu ya umma kwenye rasilimali zetu yaani wananchi wapate gawio la Moja KWA Moja la rasilimali zao kupitia akaunti za Benki na simu zao.
Wadau wa uchumi mnadhani ndoto hiyo inaweza kutimia kwamba KILA Mwezi mwananchi wa kawaida apate gawio la Rasilimali zilizopo kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa kwenye migodi,Mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vya utalii!!?
Tunaomba mchango wenu katika hilo tupate pa kuanzia,Sijawahi kusikika hili jambo tangu kuanzisha KWA Taifa hili!Tuna dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha KILA mtanzania anafaidika Moja KWA Moja na rasilimali hizi huko mbeleni KWA kupata gawio la Moja KWA Moja ambalo litamsaidia kujikimu kimaisha kama nchi zilizoendelea zinavojali Hali ya Maisha ya wa Hali ya chini.
Sisi kama wajamaa wa kisasa tuna lengo la kulifanya jeshi la magereza na jkt kama kitovu kikuu cha uchumi wa nchi yetu KWA kuanzia kwenye kilimo,usafirishaji wa bidhaa na abiria na VIWANDA kama ifuatavyo;-
KILIMO NA MIFUGO
Serikali yetu itatenga maeneo makubwa ya kilimo na ufugaji,kilimo cha mazao ya chakula na biashara pamoja na usindikaji wake Ili kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula kama mafuta ya kula!tutakuwa na maduka ya vyakula ya umma!bidhaa zote zitatoka VIWANDA vya serikali Ili kudhibiti mfumuko wa bei kutoka sekta Binafsi.
Jeshi la magereza na jkt ndio wazalishaji wakuu na kitovu kikuu cha uchumi wetu!tutajenga makambi mashambani na wataishi huko huko kama wazalishaji wakuu!kesi za mahabusu zitaharakishwa Ili kupata nguvu kazi na vijana WENGI waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne watajiunga na jkt na kutumika KWA miaka kumi mfululizo Ili kulitumikia nchi yao !na sera hii itapunguza idadi ya wahuni mtaani!
Maziwa,nyama na bidhaa nyingi zitazalishwa KWA wingi ili kuwafikia watumiaji kirahisi na KWA bei nafuu mfumuko wa bei utaisha,pia serikali itapata mapato mengi kuliko kutegemea Tozo na kodi pekee!tutashirikiana na sekta binafsi katika uuzwaji wa bidhaa hasa machinga na wenye mitaji mikubwa!
UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI
Vyombo vya usafiri vya serikali vitachuana na sekta binafsi Ili kuleta tija kwa wasafiri kuanzia boda boda,bajaji,dala dala,malori na mabasi yatachuana vilivyo na sekta binafsi Ili kudhibiti mfumuko wa bei za nauli kiholela holela!!
Hayo ni baadhi ya malengo makuu ya chama chetu Baada ya katiba kupatikana !tumeona sekta Binafsi pekee imeshindwa kuwa msaada na kuwa mnyonyaji wa wananchi.
Wakati wa kurudi kwenye misingi ya uwajibikaji umefika!
Tunaomba mchango wenu kufanikisha azma na ndoto hii kutimia kwa nchi yangu Tanzania.
"Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"
Wazo zuri,
Juzi YOWERI MUSEVENI kaongea point muhimu tuifanyie KAZI nanukuu:
"Kuwa na NATURAL RESOURCES ni jambo moja, bt Kuzibadili national Resources Ili ziku TAJIRISHE ni jambo jingine"
Mfano.
1. Tuna ardhi ya kutosha Kwa kilimo bt kilimo chenye kuleta tija kinahitaji uwekezaji kwenye ELIMU na utafiti, Mitaji na vitendeakazi.
Kumbe unaweza kuwa na Mali na Bado ukawa maskini.
Tuna madini Nchi nzima Kweli, bt yatatutajirishaje kama Nchi ikiwa ELIMU na teknolojia ya kuyachimba hatuna,
Kuyabadili madini Ili yawe Vito na yauzwe kibiashara ni jambo jingine, je tuna ELIMU ya kutosha juu ya mambo hayo?
Hatujawekeza vya kutosha Badala yake uchimbaji unaenda kuharibu vyanzo vya maji Kwa kutiririsha zebaki.
3. Tuna Bahari na maziwa ukubwa wa kutosha, bt Umewatajirisha wavuvi na Nchi Kwa kiasi Gani?
Ili bahari itutajirishe tunahitaji Meli za kisasa za uvuvi, je tunaweza kuzitengeneza? Kama ni hapana, itabidi tupate pesa za kuwalipa watujengee au tushirikiane nao na tatizo huanzia hapo!!!
SOLUTION.
1. Raslimali Ili zitutajirishe tunahitaji kuwekeza kwenye ELIMU, ELIMU, ELIMU kama alivyosema Mzee wa mamvi.
Tofauti na hapo lazima tutakuwa vibarua ktk Kuzibadili raslimali zetu wenyewe kuwa matajiri.
ELIMU ni solution no moja. Na zingine zitafuata juu ya msingi wa ELIMU.
Tukiisoma vizuri RASIMU alosimamia Judge WARIOBA imeyaangalia mambo haya vizuri, Tuipambanie itatupa njia hata ya Kupata Vyama vitakavyoendana na Maono yetu kama Nchi.
Ameeeen.