Mwl Athumani Ramadhani
JF-Expert Member
- Sep 10, 2022
- 1,280
- 2,522
- Thread starter
- #41
Unafikiri Sina KAZI!!?
Hapa nilipo napiga kazi ipasavyo !!
Tanzania KWANZA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unafikiri Sina KAZI!!?
Kweli kabisa inabidi serikali iwe mfano wa kuigwa kwa sekta binafsi na sio sekta binafsi kuwa mfano wa kuigwa kwa serikali.Kenya na Rwanda wameiga tuliyokuwa enzi za Nyerere na wanapiga hatua Kwa haraka.
ELIMU inayotolewa shule za Umma ni Bora au Ina Quality zaidi ya ELIMU itolewayo private school.
TUSUBIRI
Kwa nini una muambia hivyo ? Umejuaje Kama hana kazi ya kufanya?
Nguvu ya pesa ndio uamua Sheria.Hilo ni tatizo tulilo nalo , lakini hatupaswi kukubali matatizo yetu yawe sugu kwetu bali inabidi tuya komeshe kwa sheria kali zenye adhabu kali.
Tufanye nini SAsa hili tuwe sehemu ya Sheria,TUSUBIRI
TANZANIA mpya haishindwi Ndugu!!
Kuwa sehemu ya upya wake!!
Tatizo hilo mkuu , lakini hatupaswi kujikatia tamaa kabisa kuwa hakuna nuru yoyote mbele yetu.Nguvu ya pesa ndio uamua Sheria.
Akitokea kiongozi afatae sheria ana malizwa.
Ujamaa unaouongelea ni ngumu kuleta tija ktk mazingira ya sasa.Baada ya katiba mpya kupatikana hiki ni Moja ya chama kitakacho sajiliwa kikiwa na dhamira njema ya kurudisha nguvu ya umma kwenye rasilimali zetu yaani wananchi wapate gawio la Moja KWA Moja la rasilimali zao kupitia akaunti za Benki na simu zao.
Wadau wa uchumi mnadhani ndoto hiyo inaweza kutimia kwamba KILA Mwezi mwananchi wa kawaida apate gawio la Rasilimali zilizopo kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa kwenye migodi,Mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vya utalii!!?
Tunaomba mchango wenu katika hilo tupate pa kuanzia,Sijawahi kusikika hili jambo tangu kuanzisha KWA Taifa hili!Tuna dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha KILA mtanzania anafaidika Moja KWA Moja na rasilimali hizi huko mbeleni KWA kupata gawio la Moja KWA Moja ambalo litamsaidia kujikimu kimaisha kama nchi zilizoendelea zinavojali Hali ya Maisha ya wa Hali ya chini.
Sisi kama wajamaa wa kisasa tuna lengo la kulifanya jeshi la magereza na jkt kama kitovu kikuu cha uchumi wa nchi yetu KWA kuanzia kwenye kilimo,usafirishaji wa bidhaa na abiria na VIWANDA kama ifuatavyo;-
KILIMO NA MIFUGO
Serikali yetu itatenga maeneo makubwa ya kilimo na ufugaji,kilimo cha mazao ya chakula na biashara pamoja na usindikaji wake Ili kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula kama mafuta ya kula!tutakuwa na maduka ya vyakula ya umma!bidhaa zote zitatoka VIWANDA vya serikali Ili kudhibiti mfumuko wa bei kutoka sekta Binafsi.
Jeshi la magereza na jkt ndio wazalishaji wakuu na kitovu kikuu cha uchumi wetu!tutajenga makambi mashambani na wataishi huko huko kama wazalishaji wakuu!kesi za mahabusu zitaharakishwa Ili kupata nguvu kazi na vijana WENGI waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne watajiunga na jkt na kutumika KWA miaka kumi mfululizo Ili kulitumikia nchi yao !na sera hii itapunguza idadi ya wahuni mtaani!
Maziwa,nyama na bidhaa nyingi zitazalishwa KWA wingi ili kuwafikia watumiaji kirahisi na KWA bei nafuu mfumuko wa bei utaisha,pia serikali itapata mapato mengi kuliko kutegemea Tozo na kodi pekee!tutashirikiana na sekta binafsi katika uuzwaji wa bidhaa hasa machinga na wenye mitaji mikubwa!
UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI
Vyombo vya usafiri vya serikali vitachuana na sekta binafsi Ili kuleta tija kwa wasafiri kuanzia boda boda,bajaji,dala dala,malori na mabasi yatachuana vilivyo na sekta binafsi Ili kudhibiti mfumuko wa bei za nauli kiholela holela!!
Hayo ni baadhi ya malengo makuu ya chama chetu Baada ya katiba kupatikana !tumeona sekta Binafsi pekee imeshindwa kuwa msaada na kuwa mnyonyaji wa wananchi.
Wakati wa kurudi kwenye misingi ya uwajibikaji umefika!
Tunaomba mchango wenu kufanikisha azma na ndoto hii kutimia kwa nchi yangu Tanzania.
"Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"
Majeshi yafundishe nidhamu na UZALENDO ktk mifumo ya ELIMU Ngazi zote Ili wakifika makazini tayari wanakuwa wamepikika.nimependa hoja yako ya majeshi yawe chanzo cha ajira, na kujitegemea ningeshauri elimu iwe bure , atakayefeli sharti aende kutumikia jeshini miaka mitano kwanza arudishe hela ya serikali,
aanze na bodaboda ziwepo za jeshi,
uba za jeshi,
seremala,
makampuni ya ulinzi na usafi, makampuni ya kilimo na sekta zote na watu wafundishwe nidhamu , uwajibikaji na uchapa kazi. tungeipa miaka mitano tanzania .Tunakuwa donor country sema rais lazima aweke rehani maisha yake
Avatar Yako ni kama raia wa KP!!!!
Naendelea kupiga chaki HUKU nikiiandaa Tanzania Mpya ijayo kwa mstakabali wa Taifa letu mkuu!Piga chaki mwl,siasa haina pesa.
Najua ndugu yako kp ana hisa Sana kwenye kampuni za madini!sera Hii mtaipinga coz inahatarisha maslahi yake na wale jamaa!tutaangalia Namna NZURI ya kuliweka hilo Maana sote ni ndugu!!
Hahah wew unaona inawezekana hicho kitu ?nimependa hoja yako ya majeshi yawe chanzo cha ajira, na kujitegemea ningeshauri elimu iwe bure , atakayefeli sharti aende kutumikia jeshini miaka mitano kwanza arudishe hela ya serikali,
aanze na bodaboda ziwepo za jeshi,
uba za jeshi,
seremala,
makampuni ya ulinzi na usafi, makampuni ya kilimo na sekta zote na watu wafundishwe nidhamu , uwajibikaji na uchapa kazi. tungeipa miaka mitano tanzania .Tunakuwa donor country sema rais lazima aweke rehani maisha yake
Hautokuwa ujamaa unaoujua bali hybrid socialism!!Hahah wew unaona inawezekana hicho kitu ?
Ujamaa kama wazo tu lilifeli
Na nakuahidi nchi zote zenye ujamaa zitaendelea kufeli hadi mwisho wa Dunia
Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Njaa inakusumbua, ngoja sa100 akupe u Dc.Naendelea kupiga chaki HUKU nikiiandaa Tanzania Mpya ijayo kwa mstakabali wa Taifa letu mkuu!
Kuwa sehemu ya upya wake!!