Chama cha ujamaa na kujitegemea cuk(self reliance and socialist party SSP) na dhamira yake ya gawio la Rasilimali KWA kila mwananchi!je itawezekana!!?

Chama cha ujamaa na kujitegemea cuk(self reliance and socialist party SSP) na dhamira yake ya gawio la Rasilimali KWA kila mwananchi!je itawezekana!!?

Kenya na Rwanda wameiga tuliyokuwa enzi za Nyerere na wanapiga hatua Kwa haraka.

ELIMU inayotolewa shule za Umma ni Bora au Ina Quality zaidi ya ELIMU itolewayo private school.
Kweli kabisa inabidi serikali iwe mfano wa kuigwa kwa sekta binafsi na sio sekta binafsi kuwa mfano wa kuigwa kwa serikali.
 
nimependa hoja yako ya majeshi yawe chanzo cha ajira, na kujitegemea ningeshauri elimu iwe bure , atakayefeli sharti aende kutumikia jeshini miaka mitano kwanza arudishe hela ya serikali,
aanze na bodaboda ziwepo za jeshi,
uba za jeshi,
seremala,
makampuni ya ulinzi na usafi, makampuni ya kilimo na sekta zote na watu wafundishwe nidhamu , uwajibikaji na uchapa kazi. tungeipa miaka mitano tanzania .Tunakuwa donor country sema rais lazima aweke rehani maisha yake
 
Baada ya katiba mpya kupatikana hiki ni Moja ya chama kitakacho sajiliwa kikiwa na dhamira njema ya kurudisha nguvu ya umma kwenye rasilimali zetu yaani wananchi wapate gawio la Moja KWA Moja la rasilimali zao kupitia akaunti za Benki na simu zao.

Wadau wa uchumi mnadhani ndoto hiyo inaweza kutimia kwamba KILA Mwezi mwananchi wa kawaida apate gawio la Rasilimali zilizopo kutokana na uwekezaji unaoendelea kufanywa kwenye migodi,Mbuga za wanyama na vivutio mbali mbali vya utalii!!?

Tunaomba mchango wenu katika hilo tupate pa kuanzia,Sijawahi kusikika hili jambo tangu kuanzisha KWA Taifa hili!Tuna dhamira ya dhati kabisa kuhakikisha KILA mtanzania anafaidika Moja KWA Moja na rasilimali hizi huko mbeleni KWA kupata gawio la Moja KWA Moja ambalo litamsaidia kujikimu kimaisha kama nchi zilizoendelea zinavojali Hali ya Maisha ya wa Hali ya chini.

Sisi kama wajamaa wa kisasa tuna lengo la kulifanya jeshi la magereza na jkt kama kitovu kikuu cha uchumi wa nchi yetu KWA kuanzia kwenye kilimo,usafirishaji wa bidhaa na abiria na VIWANDA kama ifuatavyo;-

KILIMO NA MIFUGO

Serikali yetu itatenga maeneo makubwa ya kilimo na ufugaji,kilimo cha mazao ya chakula na biashara pamoja na usindikaji wake Ili kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula kama mafuta ya kula!tutakuwa na maduka ya vyakula ya umma!bidhaa zote zitatoka VIWANDA vya serikali Ili kudhibiti mfumuko wa bei kutoka sekta Binafsi.

Jeshi la magereza na jkt ndio wazalishaji wakuu na kitovu kikuu cha uchumi wetu!tutajenga makambi mashambani na wataishi huko huko kama wazalishaji wakuu!kesi za mahabusu zitaharakishwa Ili kupata nguvu kazi na vijana WENGI waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne watajiunga na jkt na kutumika KWA miaka kumi mfululizo Ili kulitumikia nchi yao !na sera hii itapunguza idadi ya wahuni mtaani!

Maziwa,nyama na bidhaa nyingi zitazalishwa KWA wingi ili kuwafikia watumiaji kirahisi na KWA bei nafuu mfumuko wa bei utaisha,pia serikali itapata mapato mengi kuliko kutegemea Tozo na kodi pekee!tutashirikiana na sekta binafsi katika uuzwaji wa bidhaa hasa machinga na wenye mitaji mikubwa!


UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI

Vyombo vya usafiri vya serikali vitachuana na sekta binafsi Ili kuleta tija kwa wasafiri kuanzia boda boda,bajaji,dala dala,malori na mabasi yatachuana vilivyo na sekta binafsi Ili kudhibiti mfumuko wa bei za nauli kiholela holela!!

Hayo ni baadhi ya malengo makuu ya chama chetu Baada ya katiba kupatikana !tumeona sekta Binafsi pekee imeshindwa kuwa msaada na kuwa mnyonyaji wa wananchi.

Wakati wa kurudi kwenye misingi ya uwajibikaji umefika!

Tunaomba mchango wenu kufanikisha azma na ndoto hii kutimia kwa nchi yangu Tanzania.

"Mzee Warioba ajumuishwe kwenye kikosi kazi cha mkandala mchakato wa katiba mpya ukamilike"
Ujamaa unaouongelea ni ngumu kuleta tija ktk mazingira ya sasa.

Ujamaa wa aina hii wa Serikali KUSIMAMIA raslimali moja Kwa moja, Enzi za Nyerere ulisababisha wananchi kuwa WAVIVU na kugeuka WEZI na WAHUJUMU wa raslimali zao wenyewe.

Mfano, Serikali ilijenga na kuhodhi na kuviendesha viwanda Nchi nzima,matokeo tulikuwa tunajiendesha Kwa hasara Nchi nzima. Na wafanyakazi waliiba wazi wazi wakisema Mali ya Serikali Haina mwenyewe.

Njia sahihi, ya kuiendea Ili kupata POSITIVE impact ni kuzikabidhi Kwa mifumo imara ktk sekta binafsi za kiuendeshaji Ili zilete tija.

IPO mifano mizuri nchini, CRDB , NHC na shirika la madini ni moja ya mifano mizuri.

Shirika la madini lilianzishwa KUSIMAMIA masuala ya madini na Tumeona wakimiliki migodi na kusuport uchimbaji mdogo mdogo.

Wana uwezo sasa wa kupeleka wananchi kusomea utaalaumu ktk vyuo vya ndani na nje ya nchi.

Zinaundwa taasisi na zinaachwa zijiendeshe bila kuingiliwa na Serikali, Tumeona mafanikio makubwa japo Si sana.

Njia hiyo itumike ktk Kila sekta zote za kiuchumi mf KILIMO, MIFUGO, UVUVI, AFYA , ELIMU, USAFIRISHAJI,UTALII, KILIMO nk.

Mfano, UTALII,viundwe taasisi imara itakayoweza kukopesheka ktk mabenki ya kimataifa dhamana ikiwa ni raslimali walizopewa na Nchi kizisimamia ktk UTALII,

Wajipe malengo ya kuuupeleka UTALII uwe kibiashara mfano, kujenga HOTELS za NYOTA Hadi 5 Nchi nzima ktk maeneo yenye mbuga za wanyama,

Pia kufanya promotions kibiashara kabisa kuvuta na kuleta watalii duniani kote.

Serikali ijenge Taasisi imara zitakazoweza kujiendesha zenyewe Serikali ikiziangalia na kuzisaidia INDIRECT.

Kuyafikia hayo, KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA ihusike.

Pia Tuombee kumpata kiongozi mwenye VISION.

Ameeeen.
 
nimependa hoja yako ya majeshi yawe chanzo cha ajira, na kujitegemea ningeshauri elimu iwe bure , atakayefeli sharti aende kutumikia jeshini miaka mitano kwanza arudishe hela ya serikali,
aanze na bodaboda ziwepo za jeshi,
uba za jeshi,
seremala,
makampuni ya ulinzi na usafi, makampuni ya kilimo na sekta zote na watu wafundishwe nidhamu , uwajibikaji na uchapa kazi. tungeipa miaka mitano tanzania .Tunakuwa donor country sema rais lazima aweke rehani maisha yake
Majeshi yafundishe nidhamu na UZALENDO ktk mifumo ya ELIMU Ngazi zote Ili wakifika makazini tayari wanakuwa wamepikika.


Ameeeen.
 
Inakuwa ngumu kutekelezeka kutokana na mikataba mibaya juu ya hizi rasilimali zetu.Utakapo ingia ndani(kushika dola) ndiyo utakuja kugundua rasilimali zote zilishauzwa tena kwa mikataba ya miaka 100 plus,na utakapotaka kugusa hiyo mikataba utakachokutana nacho ni R.I.P.
 
Broo tafuta kazi nyingine ya kufanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Najua ndugu yako kp ana hisa Sana kwenye kampuni za madini!sera Hii mtaipinga coz inahatarisha maslahi yake na wale jamaa!tutaangalia Namna NZURI ya kuliweka hilo Maana sote ni ndugu!!

Hatuna lengo la kufukuzwa wawekezaji nchini bali kuweka mazingira mazuri Kwenu na WANANCHI!!
 
nimependa hoja yako ya majeshi yawe chanzo cha ajira, na kujitegemea ningeshauri elimu iwe bure , atakayefeli sharti aende kutumikia jeshini miaka mitano kwanza arudishe hela ya serikali,
aanze na bodaboda ziwepo za jeshi,
uba za jeshi,
seremala,
makampuni ya ulinzi na usafi, makampuni ya kilimo na sekta zote na watu wafundishwe nidhamu , uwajibikaji na uchapa kazi. tungeipa miaka mitano tanzania .Tunakuwa donor country sema rais lazima aweke rehani maisha yake
Hahah wew unaona inawezekana hicho kitu ?
Ujamaa kama wazo tu lilifeli
Na nakuahidi nchi zote zenye ujamaa zitaendelea kufeli hadi mwisho wa Dunia

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hahah wew unaona inawezekana hicho kitu ?
Ujamaa kama wazo tu lilifeli
Na nakuahidi nchi zote zenye ujamaa zitaendelea kufeli hadi mwisho wa Dunia

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Hautokuwa ujamaa unaoujua bali hybrid socialism!!

Yaani serikali itajiingiza kwenye uzalishaji Ili kumlinda mwananchi dhidi ya makali ya sekta binafsi!!
Tunaweza KWA pamoja kama wachina walivyo Sasa!!
 
Back
Top Bottom