Chama cha Upinzani Namibia chapinga uteuzi wa Jaji Damaseb kuwa Mjumbe wa Tume ya Jaji Lila

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Chama cha upinzani cha Namibia, Affirmative Repositioning (AR) kimepinga vikali uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Petrus Tileinge Damaseb, kuwa mjumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi nchini Tanzania, kikisema hatua hiyo ni ya kisiasa na inaweza kuhatarisha uhuru wa mahakama ya Namibia.

Kwa mujibu wa Taarifa ya chama hicho iliyotolewa Agosti 6, 2026, uteuzi huo ulifuatia ombi la serikali ya Tanzania baada ya ziara ya hivi karibuni ya Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, nchini Tanzania, huku kikidai kuwa taratibu za kawaida za mahakama hazikufuatwa.

Katika taarifa hiyo pia imedai kuwa tume hiyo haina uhalali wa kutosha na ikaishutumu kwa kutumika kuisafisha serikali ya Tanzania dhidi ya tuhuma zinazohusiana na matukio yaliyotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025.

Chama hicho pia kimesema kumteua Naibu Jaji Mkuu anayehudumu kwa sasa katika tume hiyo kunaweza kudhoofisha taswira na uaminifu wa mahakama ya Namibia kimataifa.

AR imetaka Tume ya Huduma za Mahakama ya Namibia (JSC) kutoa maelezo ya umma kuhusu msingi wa kisheria na kimaadili wa uteuzi huo, huku ikimtaka Jaji Damaseb kuukataa uteuzi huo.

Chama hicho pia kimeonya kuwa kinaweza kuchukua hatua za kisheria ikiwa uteuzi utaendelea. Aidha, AR imeeleza mshikamano wake na wanaharakati pamoja na makundi ya upinzani nchini Tanzania, ikisema itaendelea kushinikiza uwajibikaji na haki katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.

---------

Ikumbukwe Leo Agosti 7, 2026 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akizindua rasmi ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, aliweka wazi kuwepo kwa Wajumbe wawili wa Tume hiyo kutoka nchini Uganda na Namibia.

Soma Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha
 
Attachments

Hapa kuna kitu kinafichwa bwana. Kama kweli lengo ni kupata broad perspective, mbona wamemteua huyo Jaji mara baada ya Rais wa Namibia kutembelea Tanzania? Hiyo timing inaacha maswali mengi, inaonekana kabisa ni dili la kisiasa lililomalizwa juu kwa juu.
 
Nimepitia document na nitaipitia tena; kuna misamiati ifuatayo nimeipenda kutoka kwa Mwandishi Dr. SHIPULULO.

Amesema vyama hivi viwili yaani SWAPO na CCM ni "Liberation-era dinosaurs". Maana yake ni kwamba vyama hivi vya ukombozi kimsingi dhamira yake ilishakufa; yaani haipo. Dinosaurs walishapotea juu ya uso wa dunia. 😊

Pia amesema tume hii mpya ni "Afterthought" yaani imeundwa kwa minajiri ya kupitisha fikra au maazimio ambayo yameshafikiwa. Ni tume inaundwa ili kupewa maazimio "consensus". Na hii ni utaona hakuna hadidu za rejea "Terms of Reference (ToR), ila ni huyo mama kusema wakatafute flani na flani. Tayari huyo mama ameshakuwa na "findings" sasa anataka kuonyesha kuwa hana na ajazitengeza yeye hizo "findings" 😊

Amesema pia kitendo cha kuunda tume hii ni "whitewash", kwa maana tume hii imeundwa kwa lengo la kutakatisha taswira na madoa ya utawala wa huyo mama!

Ngoja niende nikaprint hii "press release"; niiweke kwenye shajala yangu. Kuna elimu kubwa sana ya kupigia mfano katika hii nyaraka.
 
Chama cha upinzani cha Namibia, Affirmative Repositioning (AR) kimepinga vikali uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Petrus Tileinge Damaseb, kuwa mjumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi nchini Tanzania, kikisema hatua hiyo ni ya kisiasa na inaweza kuhatarisha uhuru wa mahakama ya Namibia.

Kwa mujibu wa Taarifa ya chama hicho iliyotolewa Agosti 6, 2026, uteuzi huo ulifuatia ombi la serikali ya Tanzania baada ya ziara ya hivi karibuni ya Rais wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah, nchini Tanzania, huku kikidai kuwa taratibu za kawaida za mahakama hazikufuatwa.

Katika taarifa hiyo pia imedai kuwa tume hiyo haina uhalali wa kutosha na ikaishutumu kwa kutumika kuisafisha serikali ya Tanzania dhidi ya tuhuma zinazohusiana na matukio yaliyotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025.

Chama hicho pia kimesema kumteua Naibu Jaji Mkuu anayehudumu kwa sasa katika tume hiyo kunaweza kudhoofisha taswira na uaminifu wa mahakama ya Namibia kimataifa.

AR imetaka Tume ya Huduma za Mahakama ya Namibia (JSC) kutoa maelezo ya umma kuhusu msingi wa kisheria na kimaadili wa uteuzi huo, huku ikimtaka Jaji Damaseb kuukataa uteuzi huo.

Chama hicho pia kimeonya kuwa kinaweza kuchukua hatua za kisheria ikiwa uteuzi utaendelea. Aidha, AR imeeleza mshikamano wake na wanaharakati pamoja na makundi ya upinzani nchini Tanzania, ikisema itaendelea kushinikiza uwajibikaji na haki katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.

---------

Ikumbukwe Leo Agosti 7, 2026 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati akizindua rasmi ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, aliweka wazi kuwepo kwa Wajumbe wawili wa Tume hiyo kutoka nchini Uganda na Namibia.

Soma Rais Samia: Tumeamua kuwashirikisha wenzetu kutoka Uganda na Namibia kupata muono mpana. Tume inakwenda kutafuta nani walichochea, waliotoa fedha
Ni kilaza kutoka huko tumeletewa hapa sio? Serikali itoe maelezo.
 
Na sisi tuipinge hii tume dhalimu iliyoundwa na muuaji ili kujisafisha. Tuikatae kwa nguvu zote. CHADEMA itisheni petition ya kuipinga kabisa hii tume
 
Fazafaka alipaswa kuialika Commonwealth au UN kuleta timu ya uchunguzi badala ya yeye kujiundia tume ya uchunguzi kwa namna anayopenda!
 
Back
Top Bottom