CHAMA Cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kinaungana na Chama cha Waandishi wa Habari mkoa Simiyu (SMPC), kulaani tukio la Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga kuwadhalilisha wanahabari.
Kwa mujibu wa taarifa ya SMPC, Simalenga ambaye amewahi kufanyakazi katika chombo kimoja cha habari alitoa anadaiwa kutoa maagizo ya kufukuzwa wanahabari katika kikao cha Ushauri cha Wilaya Bariadi (DCC).
Tumaamini Mkuu huyu wa wilaya hata kama alikuwa na sababu kutotaka vyombo vya habari katika kikao hicho, angetumia ustaarabu kuwaomba na baada ya kikao angeweza kutoa taarifa za kikao.
Hata hivyo kitendo cha kuwafukuza na kuangiza milango kufungwa si cha kiungwana hasa kwa kuwa kikao hicho sio cha siri na ajenda zake ni kujadiliana mambo ya maendeleo.
Hivyo JOWUTA inaungana na SMPC kukemea na kulaani matukio kama hayo, lakini pia uamuzi wa klabu hiyo kutoandika habari za mkuu huyo wa wilaya zinapaswa kuungwa mkono na wadau wote wa habari, ili kuikomesha tabia za viongozi wa aina ya Simalenga.
JOWUTA inamtaka Mkuu huyu wa wilaya kujitokeza hadharani kuomba radhi kwa tukio hili.
JOWUTA inawaomba viongozi wa juu wa Serikali kukemea vitendo vya udhalilishaji wanahabari ambavyo vimekuwa vikifanywa na viongozi mbalimbali.
JOWUTA inaamini kunyamazia hali hiyo kunapelekea kuwagombanisha wanahabari na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo tangu imeingia madarakani imekuwa na mahusiano mazuri na wanahabari.
JOWUTA itaendelea kufanyakazi na viongozi wote ambao wanaheshimu taaluma ya habari na uhuru wa vyombo vya habari ambao unatokana na Katiba ya Tanzania.
Imetolewa na Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa.
Mussa Juma
Pia soma:
Waandishi wa Habari Simiyu watangaza kutofanya kazi na DC Bariadi