Ndugu wana Jf amani iwe nanyi.kwa mda mrefu nimesoma maandiko kadha wa kadha juu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji humu Jf na nimehamasika.kwa kuanzia na kwa mazingira niliyopo nimeanza na kuku 50 wa kienyeji . wiki ijayo nitaongeza kuku 100 .sasa baada ya kusoma post tofauti tofauti juu ya mbinu anuai ningependa kushauri tuanzisheni chama cha wafugaji kuku wa kienyeji.hii itakuwa na faida zifuatazo kwa uchache ;(1) kubadilishana uzoefu na mbinu za ufugaji bora (2) kujenga mtandao wa masoko.karibuni kwa mjadala tuboreshe wazo hili.