Chama Cha Wanasheria Tanganyika(TLS) kwenda mahakamani kesho

Chama Cha Wanasheria Tanganyika(TLS) kwenda mahakamani kesho

Nicolas J Clinton Gabone

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
879
Reaction score
491
Chama Cha Wanasheria Tanganyika kimetangaza kwenda mahakamani kesho ili kutafuta uwezekano wa kutafasiri sheria juu ya nini kinatakiwa kujadiliwa na bunge maalumu katika mchakato wa katiba mpya.

Jopo hilo litaongozwa na wanasheria wanne na mahakama zote kuu za Bara na Visiwani zitausika baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.
 
Chama Cha Wanasheria Tanganyika kimetangaza kwenda mahakamani kesho ili kutafuta uwezekano wa kutafasiri sheria juu ya nini kinatakiwa kujadiliwa na bunge maalumu katika mchakato wa katiba mpya. Jopo hilo litaongozwa na wanasheria wanne na mahakama zote kuu za Bara na Visiwani zitausika baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

nawaunga mkono sana TLS mchakato huu tukiwaachia CCM itapat8iana katiba ya hovyo kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hii..ni vizuri tufuate mkondo n tabia za wakenya ambapo jambo lolote linalobishaniwa lazima lipate determination ya mahakama namna linavyopaswa kushughulikiwa..

hatua hii ya TLSinafungua njia ya kupata tafsiri sahihi kisheria kuhusu sinema za kipumbavu zinazoendelea hapa nchini kuhusu kat8ba mpya.....CCM wanadhani kwamva wanaweza kufanya kila kitu hata bila kutii matakwa ya wananchi

kinachotakiwa ni kila mmoja wetu kuchukua hatua kuepuka utekaji nyara wa mchakato huu muhimunkwa mustakabali wa nchi hii na watu wake. tukiruhusu upuuzi wa akina werema na saliva rweyemu kutamalaki nchi hii itaishia kwenye maafa.

inafika mahali hata afisa habari ikulu anazungumza kama rais wa nchi.hiki ni kiwango kikubwa cha dharau dhidi ya mamlaka ya wananchi..haivumiliki kabisa
 
Bila shaka itasaidia kuwaamsha CCM kuwa kumbe wao sio miungu wa Tanzania yetu

umejua lakini kinachoenda kufanywa au hujui hata kusoma na kuchambua maandishi.
 
Chama Cha Wanasheria Tanganyika kimetangaza kwenda mahakamani kesho ili kutafuta uwezekano wa kutafasiri sheria juu ya nini kinatakiwa kujadiliwa na bunge maalumu katika mchakato wa katiba mpya. Jopo hilo litaongozwa na wanasheria wanne na mahakama zote kuu za Bara na Visiwani zitausika baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

Hili ndilo lilitakiwa lifanywe na UKAWA toka mwanzo.Tumeshauri wee hawasikii.UKAWA ni wanasiasa Uchwara.

Utasikia baadhi yao wanaropoka hata majukwaani kuwa fulani ni fisadi na tunao ushahidi. Ukiwaambia mburuzeni mahakamani basi huyo fisadi wenu ambaye mnao ushahidi hawaendi. Ukiwaambia basi kama hamuendi sasa hivi kuna kesi ya fisadi fulani mnayemtaja kwenye mikutano yenu ya hadhara nendeni basi mkawe mashahidi kwenye hiyo kesi unakuta wanakataa.UKAWA kisiasa bure kabisa.

Hongereni chama cha wanasheria kwa kuamua kufanya hilo.
 
Hasira zako usimalizie kwa mtoto. Wewe si msemaji wa TLS na wala siyo mahakama. Kinachokwenda kufanyika mahakamani kitatoka kwa wahusika. Siyo wewe!.

umejua lakini kinachoenda kufanywa au hujui hata kusoma na kuchambua maandishi.
 
Yaani vyovyote watakavyoitafsiri hiyo sheria lazima ile kwa ccm/serikali. Ukiona umma unaiandama serikali kila kona watu wanapiga kelele ujue kumekucha watu wanataka nchi yao. This is a great revolution
 
TLS oyeee
cccm wamenichosha akili kila kitu ubabe mpaka kwenye mambo ya sheria,kama ni posho si waibe pesa huko hazina ila katiba watuachie?
 
Chama Cha Wanasheria Tanganyika kimetangaza kwenda mahakamani kesho ili kutafuta uwezekano wa kutafasiri sheria juu ya nini kinatakiwa kujadiliwa na bunge maalumu katika mchakato wa katiba mpya. Jopo hilo litaongozwa na wanasheria wanne na mahakama zote kuu za Bara na Visiwani zitausika baada ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu.

Shukrani TLS. Hatua hii ndiyo inayokwenda kuondoa sintofahamu inayoendelea sasa. Tumekuwa tukishauri hili lifanyike ili kujua nani kati ya pande zinazobishana wapo sahihi ili shughuri hii muhimu ya kutunga sheria kuu iendelee pasipo kuwachanganya wananchi.

Najuwa kwa wanaojuwa kuwa walikuwa wapotoshaji, hawataifurahia hatua hii inayochukuliwa na TLS sababu itakuwa ndio mwisho wa longolongo
 
Mtikila naye ataenda kufungua kesi mahakamani baada ya kukamilisha zoezi la kukusanya sahihi za watanzania elfu ishirini, naona Sitta anazidi kukabwa koo na namwona anapumua kwa shida.
 
umejua lakini kinachoenda kufanywa au hujui hata kusoma na kuchambua maandishi.

Ndio tatizo la kutaka kila mtu aseme jambo kwa kutumia maneno unayoyajua wewe. Kumbuka kuwa sio wote ni slow learners kama ulivyo
 
Kimkakati ccm watanufaika,sana na,kesi itakapofunguliwa mahakamani na kulizuia bunge kuendelea.itakuwa ni ushindi kwako...kilichotakiwa hapa ni kuwaacha kabisaa waendelee na kuiba posho alafu baadaye washindwe kuipitisha rasimu kutokana na kutokukidh takwa la 2/3
 
Werema ameshapata tumbo la kuharisha mpaka sasa.
prudent men on land wameona waingilie kati huu unajisi wa katiba mpya unaofanywa na JK na CCM kwa ujumla.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Hili ndilo lilitakiwa lifanywe na UKAWA toka mwanzo.Tumeshauri wee hawasikii.UKAWA ni wanasiasa Uchwara.

Utasikia baadhi yao wanaropoka hata majukwaani kuwa fulani ni fisadi na tunao ushahidi. Ukiwaambia mburuzeni mahakamani basi huyo fisadi wenu ambaye mnao ushahidi hawaendi. Ukiwaambia basi kama hamuendi sasa hivi kuna kesi ya fisadi fulani mnayemtaja kwenye mikutano yenu ya hadhara nendeni basi mkawe mashahidi kwenye hiyo kesi unakuta wanakataa.UKAWA kisiasa bure kabisa.

Hongereni chama cha wanasheria kwa kuamua kufanya hilo.
UKAWA wanajijua ni kikundi haramu ndio maana hawajatia mguu mahakamani, wangeaibika vibaya!
 
huu ni ushindi kwa mashetani ilipaswa waachwe ili mambo yawagomee huko huko Dodoma
 
Back
Top Bottom