Hamna lolote! Acacia ilikuwa ni subsidiary ya Barrick, halafu Barrick ikaamua kuingilia kati na kuidissolve Acaia, badala yake ikakubaliana na serikali kuundwa kwa Twiga. Kwa hiyo mpaka sasa hivi tunavyoongea Acacia ni nonexitent entity, na iwapo Barrick walikubaliana na serikali, na tayari wameshailipa serikali sehemu ya zile damages, sijui ni nani atapeleka mashitaka hayo unayohofia zaidi kuliko kutunza raslimali zako. Yaani kuogopa kushitakiwa kwa kulinda mali zako inakuwa ni tatizo kweli jamani? Tanzania tulipigania uhuru dhidi ya umoja wa mataifa halafu leo tuogope kupigania raslimali zetu kutoka makampuni ya watu binafsi kweli?
Anayeogopa kushitakiwa kuingia ndani ya nyumba yake akaamua kubaki nje usiku kucha hasitahili kumiliki nyumba hiyo!