Tumain
JF-Expert Member
- Jun 28, 2009
- 3,154
- 71
Aziza Athuman na Minael Msuya
MSAJILI wa vyama vya siasa nchini , John Tendwa jana alisajili chama kipya cha siasa kinachojulikana kama Alliance for Tanzania Farmers Party (ATFP).
Chama hicho chenye kauli mbiu ya 'Mtunze Mkulima Kwanza', ni cha 18 kusajiliwa nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Baadhi ya vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi, Chama cha wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , NCCR-Mageuzi, United Demokrasy Party na Tanzania Labour Party (TLP).
Vingine ni DP, FORD, UPDP, UMD, PPT, NLD, NRA, TADEA, CHAUSTA, MAKINI, JAHAZI ASILI, SAU, na PONA
Chama hicho kipya chenye Makao yake Makuu wilayani Temeke jijini Dar es Salaam kinaongozwa na mwenyekiti Soud Said na Katibu Rashid Lai.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Tendwa alisema kati ya vyama hivyo 17, vyama vilivyo hai ni saba tu.
"Kumekuwepo na usajili wa vyama wa mara kwa mara, lakini nikiangalia katika takwimu zangu hapa zinanionyesha kuwa kati ya vyama 17 nilivyovisajili vyama saba tu ndivyo vilivyo hai " alisema Tendwa.
Tendwa alikitahadharisha chama hicho kuwa, hatasita kukichukulia hatua za kisheria chama hicho pindi kitakapokiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kukifutia usajili wake.
"Ninavyosema kwamba vyama kumi haviko hai sio kwamba nafurahishwa na suala hilo, kuna taratibu za kisheria ambao tumeanza kufanya kwa maana hiyo sio kujisajili tu, tunachotaka ni chama kifanye kazi kama tulivyokisajili," alisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho alisema uongozi wake hautakuwa tofauti na uongozi wa Mwalimu Nyerere kwa kusema chama kitatilia mkazo katika msemo maarufu aliokuwa akiutumia mwalimu ujulikanao kama "Siasa safi na uongozi Bora".
Said aliongeza kuwa mpaka sasa chama hicho kina idadi ya wanachama 2,500 na kuwa chama kinategemea kuwa na wanachama wengi kulingana na mapokeo yake kwa wananchi wa hali ya chini hasa wakulima.
"Idadi ya wanachama hawa imepatikana hata kabla ya usajili, hii ni kwa sababu sera za chama changu zinakubalika kwa kuwa zinaonye jinsi mkulima atakavyonufaika," alisisitiza Said.
Alisema nchi ina rasilimali nyingi ambazo kama ingezitumia kwa umakini ingeweza kuendeleza sekta ya elimu ambayo ingeweza kuleta mabadiliko katika jamii ya sasa.
Akikumbushia historia Said alisema kuwa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) lingepewa nafasi ya kuwa jeshi la wananchi kulingana na umuhimu wake ulioionyesha mwaka 1978 wakati wa vita vya kumuondoa nduli Idd Amin Dadaa wa Uganda ambapo jeshi hilo lilijenga daraja la mto Kegera kwa siku moja.