Chama kipya chasajiliwa...

Chama kipya chasajiliwa...

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Posts
3,154
Reaction score
71
Aziza Athuman na Minael Msuya

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini , John Tendwa jana alisajili chama kipya cha siasa kinachojulikana kama Alliance for Tanzania Farmers Party (ATFP).

Chama hicho chenye kauli mbiu ya 'Mtunze Mkulima Kwanza', ni cha 18 kusajiliwa nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Baadhi ya vyama hivyo ni Chama Cha Mapinduzi, Chama cha wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , NCCR-Mageuzi, United Demokrasy Party na Tanzania Labour Party (TLP).

Vingine ni DP, FORD, UPDP, UMD, PPT, NLD, NRA, TADEA, CHAUSTA, MAKINI, JAHAZI ASILI, SAU, na PONA

Chama hicho kipya chenye Makao yake Makuu wilayani Temeke jijini Dar es Salaam kinaongozwa na mwenyekiti Soud Said na Katibu Rashid Lai.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Tendwa alisema kati ya vyama hivyo 17, vyama vilivyo hai ni saba tu.

"Kumekuwepo na usajili wa vyama wa mara kwa mara, lakini nikiangalia katika takwimu zangu hapa zinanionyesha kuwa kati ya vyama 17 nilivyovisajili vyama saba tu ndivyo vilivyo hai " alisema Tendwa.

Tendwa alikitahadharisha chama hicho kuwa, hatasita kukichukulia hatua za kisheria chama hicho pindi kitakapokiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kukifutia usajili wake.

"Ninavyosema kwamba vyama kumi haviko hai sio kwamba nafurahishwa na suala hilo, kuna taratibu za kisheria ambao tumeanza kufanya kwa maana hiyo sio kujisajili tu, tunachotaka ni chama kifanye kazi kama tulivyokisajili," alisema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho alisema uongozi wake hautakuwa tofauti na uongozi wa Mwalimu Nyerere kwa kusema chama kitatilia mkazo katika msemo maarufu aliokuwa akiutumia mwalimu ujulikanao kama "Siasa safi na uongozi Bora".

Said aliongeza kuwa mpaka sasa chama hicho kina idadi ya wanachama 2,500 na kuwa chama kinategemea kuwa na wanachama wengi kulingana na mapokeo yake kwa wananchi wa hali ya chini hasa wakulima.

"Idadi ya wanachama hawa imepatikana hata kabla ya usajili, hii ni kwa sababu sera za chama changu zinakubalika kwa kuwa zinaonye jinsi mkulima atakavyonufaika," alisisitiza Said.

Alisema nchi ina rasilimali nyingi ambazo kama ingezitumia kwa umakini ingeweza kuendeleza sekta ya elimu ambayo ingeweza kuleta mabadiliko katika jamii ya sasa.

Akikumbushia historia Said alisema kuwa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) lingepewa nafasi ya kuwa jeshi la wananchi kulingana na umuhimu wake ulioionyesha mwaka 1978 wakati wa vita vya kumuondoa nduli Idd Amin Dadaa wa Uganda ambapo jeshi hilo lilijenga daraja la mto Kegera kwa siku moja.
 
My take: Ndiyo kile cha mwanakijiji au?
 
I doubt the new party will have any impact. Politics is about popularity and sadly they don't have any big name politician who can publicize the party. I say it dies a slow and natural death.
 
I doubt the new party will have any impact. Politics is about popularity and sadly they don't have any big name politician who can publicize the party. I say it dies a slow and natural death.
Popularity can be built with time...so lets wait and see...
 
Popularity can be built with time...so lets wait and see...

True mkuu but politics is survival of the fittest. I don't think the Political elements will just wait for the party to gain popularity. They must have a survival plan for the time being or risk being just another political party which came by.
 
Aziza Athuman na Minael Msuya

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini , John Tendwa jana alisajili chama kipya cha siasa kinachojulikana kama Alliance for Tanzania Farmers Party (ATFP).

Chama hicho chenye kauli mbiu ya 'Mtunze Mkulima Kwanza', ni cha 18 kusajiliwa nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. ....

...mnh, pakianzishwa 'alliance for Tanzania Businessmen Party' kitawakomba wengi iwapo kitahusisha wafanyabiashara maarufu nchini mfano; Mengi, Manji, Bakhressa,... (wazawa wenye asili tofauti)
 
Msianze kukisemea kwa sasa kwa kuwa kuna leo na kesho...na maisha hayatuami sikuzote hubadilika.
 
Hiki ni chama cha wakulima tu au na siasa mbona kinachanganya.

Kinatetea maslahi ya wakulima pekee au na wananchi wengine wa kawaida?

Du, kaaazi kwelikweli!
 
Chama chenyewe kinaanza kwa kuji limit kwa wakulima.

What do they think this is? '47 Tanganyika with "Baba Kabwela" at the helm?

They will have to either expand their scope or die from malnutrition.

That is if their entire purpose is not just to gain some ruzuku.
 
mafisadi haoo wanakuja kweli Wadanganyika mpaka lini tutapiga hesabu ya nchi badala ya tumbo, Mimi nasema hao wamepiga mbali uchaguzi unakuja watapata ruzuku bila jasho haya tudanganyikeni
 
Bluray,
Ukiona hivi fahamu kwamba hakuna vyama mbadala vya Upinzani hivyo watazoa washabiki..
Siku zote ukiona nchi ina vyama vingi ni kutokana na kutokuwepo na Upinzani wa kweli..watu wanakimbilia ruzuku tu.
 
Tutaipata na kukiona cha moto. Burudani ya maneno ni maarufu Tanzania, Kingine kinakuja karibuni, WPP = Weusi Peoples Party!

Leka
 
I doubt the new party will have any impact. Politics is about popularity and sadly they don't have any big name politician who can publicize the party. I say it dies a slow and natural death.

May be there are big names behind, let wait and see.
 
Hiki ni chama cha wakulima tu au na siasa mbona kinachanganya.

Kinatetea maslahi ya wakulima pekee au na wananchi wengine wa kawaida?

Du, kaaazi kwelikweli!

Wakulima ndo wengi nchi hii na ndo wenye shida, upataji wa kura huenda ukawa mkubwa kutokana na kuwalenga wakulima. Je sera za hiki chama zinasemaje??????????
 
I think chama hiki ni cha Mh. fulani kwani nilisikia anataka kugombea Urais mwaka 2010 sasa tuweni makini maana si tunahitaji chama chenye sera madhubuti kikisaidia na chama Cha Walalahoi chenye kupinga Ufisadi ( Chadema) ili kiwe na nguvu. OK mgeni karibu tuone Sera zako
 
Hao viongozi wenyewe wa hicho chama ni wakulima?
 
May be there are big names behind, let wait and see.

Hawa jamaa wana akili na wameona mbali sana, this is political speculation unakuwa na chama kilichosajiliwa ambacho kipo kipo tu. Sababu kubwa ya kufanya hivi ni process ndefu ya kuanzisha chama kipya na ukiritimba wa msajili akiona chama imara kinaanzishwa kukabili chama tawala.

Ona jina lao halijakaa kisiasa kabisa na halina mvuto wa kisiasa lakini sheria inaruhusu kubadili jina la chama, viongozi hawajulikani kabisa kisiasa.

Hali ya siasailivyo sasa yaani kutokaa vizuri na kutoaminika ndani ya chama Tawala na kutokuwa na wagombea binafsi kunakifanya chama hicho kuwa meeting place ya watu ambao wataenda wakati kile alichosema Baba wa taifa kitatokea, mgawanyiko ndani ya CCM, msikidharau hich chama it is a force to reckon ngojeni mwaka kesho.

Give them time.
 
Wakulima ndo wengi nchi hii na ndo wenye shida, upataji wa kura huenda ukawa mkubwa kutokana na kuwalenga wakulima. Je sera za hiki chama zinasemaje??????????

Alama ya jembe kwenye bendera ya CCM ina maana gani labda ndio maana inashinda kila siku kumbe siri ni wakulima, mtu wa kijijini anaelewa lakini maana ya Alliance for Tanzania Farmers Party ili awe sehemu ya chama hicho?
 
Bluray,
Ukiona hivi fahamu kwamba hakuna vyama mbadala vya Upinzani hivyo watazoa washabiki..
Siku zote ukiona nchi ina vyama vingi ni kutokana na kutokuwepo na Upinzani wa kweli..watu wanakimbilia ruzuku tu.

Mkubwa
Naona siasa za Canada, US, UK zimekuathiri kweli. Mbona kule Scandinavia kuna utitiri wa vyama. Inatokea wakati wa uchaguzi mkuu wapiga kura hutawanyika na kulazimisha kuundwa kwa serikali ya mseto wa vyama. Lakini ukisikia historia yao ni kwamba nao walikuwa na CCM yao (iliyo safi lakini) kwa miongo kadhaa, huku vyama vya upinzani vikisindikiza tu. CCM hiyo haikumeguka hadi leo, ila imekuwa dhaifu, maana chama ni wanachama na wapenzi.
 
Alama ya jembe kwenye bendera ya CCM ina maana gani labda ndio maana inashinda kila siku kumbe siri ni wakulima, mtu wa kijijini anaelewa lakini maana ya Alliance for Tanzania Farmers Party ili awe sehemu ya chama hicho?

Wakati wa kampeni watajulishwa maana yake hapo ndo kazi inaanza kuhamia kwenye hicho chama maana watajua ni cha wakulima
 
Back
Top Bottom