Chama kipya chaundwa Tanzania kuendeleza falsafa ya Magufuli

Hiki chama cha wasukuma hakitafanikiwa.
Hiki si Chama Cha Wasukuma,ni Chama Cha Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao.Muache kukipaka matope.Tunataka kuitawala nchi yetu,ku-own our resources na hivyo kuwaletea wananchi wetu maendeleo ya kweli.Mimi nakipenda hiki Chama for what it stands for,lakini sio Msukuma.Tupo kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
 
Chama kinataka kuendeleza haya.

Kifie mbali
1650295306129.jpg
1650281288122.jpg
1650526286254.jpg
 
Hiki si Chama Cha Wasukuma,Ni Chama Cha Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao.Tunataka kuitawala nchi yetu,ku-own our resources na hivyo kuwaletea wananchi wetu maendelea ya kweli.Mimi nakipenda hiki Chama for what it stands for,lakini sio Msukuma.Tupo kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Watu wanaelewa vizuri mkakati wa chama hiki. Kuna watu waliofaidika na utawala wa Magufuli, walikula asali lakini ghafla wakaonjeshwa shubiri, hawa ni akina Makonda na wengine wengi kutoka kanda ya ziwa. Sasa hawa wanataka kurudi kivingine. Nembo ya chama ni picha ya Magufuli hili nalo kosa kubwa.
 
Kwani huyo jamaa yenu alishawahi kuwaga na falisafa? Ipi?
Jamaa yetu?Kama una maana ya Magufuli commitment yake ilikuwa kulinda rasilimali za nchi na kuwaletea Watanzania maendeleo kwa kutumia rasilimali za nchi zao.
 
Chama la wasukuma, tunataka chama cha watanzania siyo cha ukabila,

Hawa wasukuma wameshefeli tayari, akili yao ndo imefikia hapo,

Magufuli alitesa wengi kujiegemeza kwake moja kwa moja wamepoteza wengi, familia na jamii kubwa ya watanzania walioumizwa na utawala wake!!

Wasukuma kwa sababu kila kitu kwao enzi ya Magufuki ilikuwa mteremko wanajiaminisha kuwa tanzania nzima walikuwa na raha kama wao!!

CCM bado sana itaongoza na hamna wa kuweza kuitingisha kwa ujumla wake!!

Huo Umoja wa Wasukuma Party ushaenda kwenye trush tayari!!
 
Wataungwa mkono na walio wengi !!

Wachache wa juu ndo watawapinga!!.

Ukweli ni kua Magufuli alipendwa na walio wengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna uzi humu, nimeusahau, unajibu vizuri na kitaalamu kabisa kuhusu hao 'wengi' wanaompenda magufuli. Tz ukiijulia kidogo tu utapendwa sana.........anayeimba habari za kuinama na kupachika rungu au kufudua na kusafishwa mtaro anapata mashabiki lukuki huku anayemuimbia mama yake kule kjjn kuwa akaze moyo mwanae anatafuta, anajipatia mashabiki wawili tu.

Ule uzi umeeleza kitaalamu kabisa, ukiwaelewa hawa hawakupi shida hata kidogo. Mi binafsi najua kuwa kuna wengi wanampenda mjomba jpm lkn sishtushwi hata kidogo kwn najua n watu wa aina gn.....ni watz
 
UTANGULIZI
TAFADHALI NAOMBA NISIRUSHIWE MADONGO,MIMI NI MJUMBE TU.HATA HIVYO NIKIRI KWAMBA HILI WAZO NIMELIPENDA,INGAWA MIMI NI MWANA CCM.NIKIRI KWAMBA BAADA YA MIAKA 61 YA UHURU,BADO CCM INATUPIGISHA WATANZANIA MAKIDA MAKIDA.

Chama kipya cha kisiasa kimeanzishwa nchini Tanzania, kikiwa na lengo la kuendeleza sera na mtindo wa uongozi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.

Waanzilishi wa Umoja party wanaripotiwa kuwa wanachama na watu maarufu ndani ya chama kinachotawala cha CCM, ambao hawana furaha na uongozi wa sasa.

Mwanzilishi wa chama hicho Seif Maalim Seif, ameambia sauti ya Amerika VOA kwamba “Tuliwasilisha maombi ya usajili mwaka jana na tumefikia hatua ya marekebisho kadha wa kadha. Katika Ofisi ya msajili wa vyama kuna katiba na kanuni za chama chetu na vielezo vyote vinavyotakiwa.”

Baadhi ya vigogo wa CCM wanaunda Umoja party?

Kuna ripoti kwamba huenda watu maarufu na wa ngazi ya juu katika chama kinachotawala, ambao wangependelea Tanzania iongozwe namna alivyokuwa anaongoza aliyekuwa rais wa nchi hiyo hayatoi John Pombe Magufuli, ndio wanaosukuma kuundwa kwa chama cha umoja.

“Chama chetu kilifikia hatua ya kuwekwa kwenye gazeti la serikali mwezi Novemba mwaka jana kwa mda wa siku 21 kwa yeyote aliye na pingamizi. Kwa hivyo hiki chama sio kwamba watu wamejikusanya na kuamua kufanya hivi na hivi. Tunachosubiri ni maelekezo ya msajili wa vyama kwa ajili ya kupewa cheti cha usajili.” Amesema Maalim Seif.

Picha za watu ambao wamevalia fulana za chama cha umoja, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Fulana hizo zina picha ya aliyekuwa rais wa Tanzania John Magufuli.

“sisi wa upande wetu hatuna deni lolote la mahitaji ya kisheria ya kutaka kusajiliwa. Ni Afisi tu ya msajili wa vyama kutuambia kiachofuata. Tulishamaliza mwaka mmoja sasa.” Ameongezea Seif Maalim Seif.

Malengo ya umoja party

Misingi ya chama hicho ni kuendeleza falsafa ya aliyekuwa rais John Mgufuli. Waanzilishi wake wanasema kwamba Tanzania sasa ipo katika hali ya sintofahamu, miongoni mwa vyama vya kisiasa huku hali ya maisha kwa watanzania ikiendelea kuwa ngumu, na kwamba ipo haja ya kufuata nyayo za Magufuli kuongoza taifa hilo.

Hata hivyo, Seif Maalim amesita kusema iwapo chama cha mapinduzi kina mapungufu kwa sasa kuendeleza falsafa ya Magufuli akisema kwamba “nadhani falsafa yake, kama chama cha mapinduzi kinaitumia au la, ni jukumu la wananchi wenyewe kuamua.”

Wanachama wengine wa Umoja party hata hivyo bado ni siri ya wenye chama.

“Jamii inaona ukweli ni akina nani wana dhati ya kumuenzi rais Magufuli. Wale ambao wapo tayari kupoteza nyadfa zao, na wale wanaoona kwamba falsafa ya Magufuli haitekelezwi. Siwezi kuwataja majina lakini dhamira zao zinajulikana.” Amesema Maalim Seif, akiongezea kwamba “wimbi la kisiasa ni la kawaida” akiwa anajibu swali iwapo kuundwa kwa umoja Party kutavuruga chama cha CCM ambacho alikipenda John Magufuli.

Mvutano ndani ya chama cha CCM

Mnamo mwezi Januari, mjadala mkali ulitokea Tanzania kuhusu deni la nchi hiyo linaloendelea kuongezeka, baadhi ya viongozi katika chama kinachotawala cha CCM wakisikika hadharani wakimkosoa rais Samia Suluhu Hassan kwa kile walisema ni “kuendelea kukopa kiholela” ili kufadhili miradi ya serikali.

Mjadala huo ulipelekea spika wa buge la taifa Job Ndugai kujiuzulu.

Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa CCM walikosoa uongozi wa rais Samia, ambaye baadaye alifanya mabadiliko serikali na kuwatimua baadhi ya viongozi, siku chache baada ya kusema hadharani kwamba angewatimua wale ambao wanataka kufanya siasa badala ya kutumikia wananchi kuleta maendeleo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC
Falsafa ya kuendeleza kazi ya Magufuri itawasaidia sana lakini watakwama kwa sababu Magufuri hakupenda kukosolewa hivyo waanzilishi wake nao hawatopenda kukosolewa ili kulinda heshima ya Hayati Magufuri.
 
UTANGULIZI
TAFADHALI NAOMBA NISIRUSHIWE MADONGO,MIMI NI MJUMBE TU.HATA HIVYO NIKIRI KWAMBA HILI WAZO NIMELIPENDA, INGAWA MIMI NI MWANA CCM.NIKIRI KWAMBA BAADA YA MIAKA 61 YA UHURU, BADO CCM INATUPIGISHA WATANZANIA MAKIDA MAKIDA.

Chama kipya cha kisiasa kimeanzishwa nchini Tanzania, kikiwa na lengo la kuendeleza sera na mtindo wa uongozi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.

Waanzilishi wa Umoja party wanaripotiwa kuwa wanachama na watu maarufu ndani ya chama kinachotawala cha CCM, ambao hawana furaha na uongozi wa sasa.

Mwanzilishi wa chama hicho Seif Maalim Seif, ameambia sauti ya Amerika VOA kwamba “Tuliwasilisha maombi ya usajili mwaka jana na tumefikia hatua ya marekebisho kadha wa kadha. Katika Ofisi ya msajili wa vyama kuna katiba na kanuni za chama chetu na vielezo vyote vinavyotakiwa.”

Baadhi ya vigogo wa CCM wanaunda Umoja party?

Kuna ripoti kwamba huenda watu maarufu na wa ngazi ya juu katika chama kinachotawala, ambao wangependelea Tanzania iongozwe namna alivyokuwa anaongoza aliyekuwa rais wa nchi hiyo hayatoi John Pombe Magufuli, ndio wanaosukuma kuundwa kwa chama cha umoja.

“Chama chetu kilifikia hatua ya kuwekwa kwenye gazeti la serikali mwezi Novemba mwaka jana kwa mda wa siku 21 kwa yeyote aliye na pingamizi. Kwa hivyo hiki chama sio kwamba watu wamejikusanya na kuamua kufanya hivi na hivi. Tunachosubiri ni maelekezo ya msajili wa vyama kwa ajili ya kupewa cheti cha usajili.” Amesema Maalim Seif.

Picha za watu ambao wamevalia fulana za chama cha umoja, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Fulana hizo zina picha ya aliyekuwa rais wa Tanzania John Magufuli.

“sisi wa upande wetu hatuna deni lolote la mahitaji ya kisheria ya kutaka kusajiliwa. Ni Afisi tu ya msajili wa vyama kutuambia kiachofuata. Tulishamaliza mwaka mmoja sasa.” Ameongezea Seif Maalim Seif.

Malengo ya umoja party

Misingi ya chama hicho ni kuendeleza falsafa ya aliyekuwa rais John Mgufuli. Waanzilishi wake wanasema kwamba Tanzania sasa ipo katika hali ya sintofahamu, miongoni mwa vyama vya kisiasa huku hali ya maisha kwa watanzania ikiendelea kuwa ngumu, na kwamba ipo haja ya kufuata nyayo za Magufuli kuongoza taifa hilo.

Hata hivyo, Seif Maalim amesita kusema iwapo chama cha mapinduzi kina mapungufu kwa sasa kuendeleza falsafa ya Magufuli akisema kwamba “nadhani falsafa yake, kama chama cha mapinduzi kinaitumia au la, ni jukumu la wananchi wenyewe kuamua.”

Wanachama wengine wa Umoja party hata hivyo bado ni siri ya wenye chama.

“Jamii inaona ukweli ni akina nani wana dhati ya kumuenzi rais Magufuli. Wale ambao wapo tayari kupoteza nyadfa zao, na wale wanaoona kwamba falsafa ya Magufuli haitekelezwi. Siwezi kuwataja majina lakini dhamira zao zinajulikana.” Amesema Maalim Seif, akiongezea kwamba “wimbi la kisiasa ni la kawaida” akiwa anajibu swali iwapo kuundwa kwa umoja Party kutavuruga chama cha CCM ambacho alikipenda John Magufuli.

Mvutano ndani ya chama cha CCM

Mnamo mwezi Januari, mjadala mkali ulitokea Tanzania kuhusu deni la nchi hiyo linaloendelea kuongezeka, baadhi ya viongozi katika chama kinachotawala cha CCM wakisikika hadharani wakimkosoa rais Samia Suluhu Hassan kwa kile walisema ni “kuendelea kukopa kiholela” ili kufadhili miradi ya serikali.

Mjadala huo ulipelekea spika wa buge la taifa Job Ndugai kujiuzulu.

Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa CCM walikosoa uongozi wa rais Samia, ambaye baadaye alifanya mabadiliko serikali na kuwatimua baadhi ya viongozi, siku chache baada ya kusema hadharani kwamba angewatimua wale ambao wanataka kufanya siasa badala ya kutumikia wananchi kuleta maendeleo.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC
Na mimi nitaanzisha chama ili kulinda mema yote yale aliyoyafanya Rais wa Awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa.
 
Chama la wasukuma, tunataka chama cha watanzania siyo cha ukabila,

Hawa wasukuma wameshefeli tayari, akili yao ndo imefikia hapo,

Magufuli alitesa wengi kujiegemeza kwake moja kwa moja wamepoteza wengi, familia na jamii kubwa ya watanzania walioumizwa na utawala wake!!

Wasukuma kwa sababu kila kitu kwao enzi ya Magufuki ilikuwa mteremko wanajiaminisha kuwa tanzania nzima walikuwa na raha kama wao!!

CCM bado sana itaongoza na hamna wa kuweza kuitingisha kwa ujumla wake!!

Huo Umoja wa Wasukuma Party ushaenda kwenye trush tayari!!
Mbona mwanzilishi wa hicho chama ni mzanzibar wapi kimeonesha kina muundo wa kisukuma au wanahubiri ukabila?
 
Falsafa ya Magufuli ni nini? Nafikiri tunachanganya Falsafa na vitu vya kijinga
 
Chama la wasukuma, tunataka chama cha watanzania siyo cha ukabila,

Hawa wasukuma wameshefeli tayari, akili yao ndo imefikia hapo,

Magufuli alitesa wengi kujiegemeza kwake moja kwa moja wamepoteza wengi, familia na jamii kubwa ya watanzania walioumizwa na utawala wake!!

Wasukuma kwa sababu kila kitu kwao enzi ya Magufuki ilikuwa mteremko wanajiaminisha kuwa tanzania nzima walikuwa na raha kama wao!!

CCM bado sana itaongoza na hamna wa kuweza kuitingisha kwa ujumla wake!!

Huo Umoja wa Wasukuma Party ushaenda kwenye trush tayari!!
Subiri msajili akatae siyo wewe, hebu tuliza mshono na usikilize utaratibu hapo chini
 
Back
Top Bottom