Hizi ni kauli dhaifu sana kutoka kwa mtu asiyekuwa makini. Hata kupiga na kudaka penati kuna kwata (drill) yake wakati wa mazoezi uwanjani. Ni mtu wa hovyo kabisa anaefurahia kushindwa kwa njia ya penati. Kwani hiyo bahati isiwaangukie Simba iende kwa Wydad ambao wapigaji wao wote walifunga na kipa wao kudaka penati mbili? Unahalalisha uzembe utumike kuficha ukweli. Kupiga penati na kudaka penati kunahitaji ufundi pia sio bahati peke yake inayoamua penati. Yaani Simba kuishia robo finali mara 4 unasema ni kwa bahati mbaya tu, Simba tuna matatizo makubwa sana ambayo yanaigharimu timu. Kocha Robatihno analazimika kutumia wachezaji haohao kila mechi kwa dk 90 kwasababu walioko kwenye benchi ni malonyalonya tu, haoni ni nani anaweza kumuingiza kuchukua nafasi ya Onyango hata kama Onyango hafanyi vizuri, haoni mbadala wa Baleke, chama, saido, shabalala, kapombe, inonga, Kibu wala Mzamiru hata kama kama wawe wamepewa kadi ya njano, wameumia, wamechoka au wameamkaa vibaya siku hiyo. Lazima wanasimba wote wapaze sauti kuuanika ukweli huu kwa wafanya maamuzi., Simba ni mbovu sana hata hapo ilipofika ni kwahisani ya Vipers, Big Bullets, de agosto. Horoya na Wydad mbovu msimu huu. Uchochoro wa simba treet inawezekana umepatikana kwa bahatibahati tu au kwa njia ya mchongo fulani.