Chama na kipa Ally ndio walioiondosha Simba mashindanoni

Chama na kipa Ally ndio walioiondosha Simba mashindanoni

... na kumuamini kijana kinda kulisababisha Simba kuingia hasara kubwa sana ya kutolewa mashindanoni na timu dhaifu ya Wydad,
Yaani Wydad imekuwa dhaifu ghafla? Si mlikuwa mnatuambia imeipiga Rivers united 6-0 kwa hiyo na Simba ijiandae na kipigo kikubwa? Baada ya kuona mnyama amekomaa kwa bingwa mtetezi na kumlazimisha ashinde kwa penati, mnaanza kusema eti Wydad ni timu dhaifu!
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Huwezi kuzuia hisia zetu kwa maneno rahisi TU hayo. Simba na Yanga ndio furaha zetu, Simba ameukimbia urithi kwa Mama ujue wa 10m kila goli. Sasa hivi watatamba Yanga TU kma nao watapita. Tutaficha wp nyuso zetu?
Sasa ulitaka wajilipue? Ndio matokeo hayo. Jifunze kupokea matokeo vyovyote vile yalivyo, vinginevyo utaugua sonona.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
UTAONGEA YOTE mkuu lakini mchawi ni.........

KUHUSU SUALA LA USAJILI.

NASHAURI YAFUATAYO.

1. NIMESIKITIKA UONGOZI KUMUACHA BENO KAKOLANYA.
Kupata Golikipa aina ya kakolanya itakuwa mtihani mkubwa sana.
Sijui kama Tutakuwa na Golikipa No 2 mwenye ubora wa Kakolanya.
Sijui kama hatutaenda Nje kutafuta mbadala wa MANURA.

2.UBAHILI NA 10% KWENYE IDARA YA USAJILI.
tumeshuhudia wakiletwa wachezaji cheep mno kwenye usajili wachezaji wenye uwezo mdogo sana na gharama ndogo sama

3. USAJILI WA QUALITY NDOGO NA KUKOSA SCAUT WAZURI.

I. Ismail sawadogo.
II .mohamed Qottara
III. Augustino Okkrah. (9)
IV. Peter Banda.
V. Sadio Kanute atafutiwe mbadala(8)
VI. Sackho nae Atupishe.

4. WACHEZAJI WAZAWA NAPO NI SHIDA.
Changamoto ya umli.
Nyoni, Boko, mkude,
Viwango vidogo.
Kapama, Gadiel, Mwanuke,

MASHABIKI TUMECHOSHWA KUISHIA ROBO FAINALI.
TUNA HELA ZA KUTOSHA KWA AJILI YA USAJILI.
HELA YA SUPER CUP 4 BILION.
HELA YA CAF. CAFCL 2 BILION

UONGOZI PUNGUZENI UBAHILI
ROBERTINO ASAJILI.
Hiyo ni mihemko.. Yani sacko na kanoute watoke kwa sababu zipo.. 🤣 🤣 🤣
 
Malengo ya robatihno ilikuwa afikishe timu nusu final, je, malango aliyopewa yamefikiwa? Ana hoja dhaifu eti amelidhika na kiwango. Malengo yalikuwa kupandisha kiwango Cha timu au nusu final?
 
Sasa ulitaka wajilipue? Ndio matokeo hayo. Jifunze kupokea matokeo vyovyote vile yalivyo, vinginevyo utaugua sonona.
Tumeshayapokea hii ni postmortem TU. Hata jogoo akikatwa shingo anaweza kuendelea kuwika kwa muda.
 
Lawama atupiwee kocha na kina mgundaa. Simba ilistahiki kwenda next ¹ step Ila wakakwamishwa na chama na kipa
 
Yagangwe yajayo...
Sasa hivi ni Yanga Yanga Yanga TU kila Kona mpaka Ikulu, hii haikubaliki sisi robo fainali tunaambulia maruturutu TU, wenzetu robo finali 1 TU imezaa nusu finali,
 
Kilichoiua simbà ni kuwa na kikosi chembambà sana Cha wazee wanaocheza mechi zote, Binadamu sio mashine lazima wanapata uchovu na maumivu lakini wanaogopa kusema illi wasieleweke vibaya na kukosa namba. Saido, Kapombe, Shabalala,, onyango, Inonga, Baleke wamechezeshwa mechi zooooote kubwa na ndogo utafhani ni maroboti. Timu inaishia robo finali kila mwaka, haikui kama vile mtoto aliyebemendwa. Timu Ina wachezaji waliosajiliwa kwa 10% ambao hawachezi. Sifa walizopewa akina sawadogo, Qatara, okrah, okwah, sakho, Banda na phiri wakati wakati wanasajiliwa ni nyingi sana kiasi Cha kuachwa kusugua mbao ndefu uwanjani. Timu yetu imejaa wachezaji na viongozi wachawi wanaoamini ulozi kwenye kupata namba na kupata matokeo uwanjani. Timu Ina uwekezaji janjajanja, usajili janjajanja, transformation janjajanja na mipango ya janjajanja. Pesa walizokuwa wakichangishana kujenga uwanja alizosema Barbra ziko wapi na kwa nani. Zile 20b ziko kwenye account ipi, mchakato wa mabadiliko umekwamia wapi?
 
Huyu sio Uto mwenzangu Mkuu! Huyu lazima atakua dunduka, anaongea kwa uchungu mno.
Tatizo Utopolo ni makocha,wachambuzi na wataalamu wa utabiri.Wachezaji hatuwadai chochote Wamejitahidi na penalti zimeamua.Kuhusu Inonga lazima wewe Utopolo uweweseke na kukubali uwezo wake.Alikutungua tarehe 16 April.Inonga ametimiza wajibu wake ndio maana ni beki bora Nchini.
Eti Wydad wamepungua uwezo?
 
Kocha huyu ni kweli alikisea sana. Kwanza alishindwa kujua kuwa baadhi ya wachezaji wake Wana umri mkubwa lakini aliruhusu wachezaji walewale wacheze mechi ya Ihefu, derby, Wydad mechi ya kwanza na Wydad mechi ya pili. Hizi ni mechi kubwa na ngumu zote kuwaacha wachezaji waaalewaaale wacheze dk 90. Pili alikubali kudanganywa kuwa kipa namba 2 hastahili kuweko kiwanjani na tatu kuamua kwenda kupaki basi kule Morocco. Alipaswa kuchezesha wachezaji kwa kuwapunzisha kama Nabi anavyofanya
Nabi huyo huyo aliyetolewa Champions league na kuangukia Losers Cup au mwingine?Nabi huyo huyo anayeburuzwa na Robertinho kila timu zao zikikutana?Nabi huyo huyo aliyezungumza kipare baada ya Debi kwa kutajiwa jina la Robertinho?
 
Hao mnaowaita "wazee" waliwatungua 2 nunge.Mkapoteana kila mmoja akabaki kusema lake. Wanayefungwa na "wazee" wanakua nani?Viwete??
 
Ajabu waliyetolewa Simba na wanaoumia ni Gongowazi!
Simba huwasikii hata wakilalamika.
 
Tatizo Utopolo ni makocha,wachambuzi na wataalamu wa utabiri.Wachezaji hatuwadai chochote Wamejitahidi na penalti zimeamua.Kuhusu Inonga lazima wewe Utopolo uweweseke na kukubali uwezo wake.Alikutungua tarehe 16 April.Inonga ametimiza wajibu wake ndio maana ni beki bora Nchini.
Eti Wydad wamepungua uwezo?
Wydad wabovu tu Mkuu.
 
Hizi ni kauli dhaifu sana kutoka kwa mtu asiyekuwa makini. Hata kupiga na kudaka penati kuna kwata (drill) yake wakati wa mazoezi uwanjani. Ni mtu wa hovyo kabisa anaefurahia kushindwa kwa njia ya penati. Kwani hiyo bahati isiwaangukie Simba iende kwa Wydad ambao wapigaji wao wote walifunga na kipa wao kudaka penati mbili? Unahalalisha uzembe utumike kuficha ukweli. Kupiga penati na kudaka penati kunahitaji ufundi pia sio bahati peke yake inayoamua penati. Yaani Simba kuishia robo finali mara 4 unasema ni kwa bahati mbaya tu, Simba tuna matatizo makubwa sana ambayo yanaigharimu timu. Kocha Robatihno analazimika kutumia wachezaji haohao kila mechi kwa dk 90 kwasababu walioko kwenye benchi ni malonyalonya tu, haoni ni nani anaweza kumuingiza kuchukua nafasi ya Onyango hata kama Onyango hafanyi vizuri, haoni mbadala wa Baleke, chama, saido, shabalala, kapombe, inonga, Kibu wala Mzamiru hata kama kama wawe wamepewa kadi ya njano, wameumia, wamechoka au wameamkaa vibaya siku hiyo. Lazima wanasimba wote wapaze sauti kuuanika ukweli huu kwa wafanya maamuzi., Simba ni mbovu sana hata hapo ilipofika ni kwahisani ya Vipers, Big Bullets, de agosto. Horoya na Wydad mbovu msimu huu. Uchochoro wa simba treet inawezekana umepatikana kwa bahatibahati tu au kwa njia ya mchongo fulani.
 
Lawama atupiwee kocha na kina mgundaa. Simba ilistahiki kwenda next ¹ step Ila wakakwamishwa na chama na kipa
Simba bado iko kwenye uendeshaji wa aina ileile ya zama za akina Gulamali za kuagiza bure bila ushuru makontena 5 ya tv na kuwapa wachezaji tv 25 tu kama zawadi ya kutwaa ubingwa.
 
Hizi ni kauli dhaifu sana kutoka kwa mtu asiyekuwa makini. Hata kupiga na kudaka penati kuna kwata (drill) yake wakati wa mazoezi uwanjani. Ni mtu wa hovyo kabisa anaefurahia kushindwa kwa njia ya penati. Kwani hiyo bahati isiwaangukie Simba iende kwa Wydad ambao wapigaji wao wote walifunga na kipa wao kudaka penati mbili? Unahalalisha uzembe utumike kuficha ukweli. Kupiga penati na kudaka penati kunahitaji ufundi pia sio bahati peke yake inayoamua penati. Yaani Simba kuishia robo finali mara 4 unasema ni kwa bahati mbaya tu, Simba tuna matatizo makubwa sana ambayo yanaigharimu timu. Kocha Robatihno analazimika kutumia wachezaji haohao kila mechi kwa dk 90 kwasababu walioko kwenye benchi ni malonyalonya tu, haoni ni nani anaweza kumuingiza kuchukua nafasi ya Onyango hata kama Onyango hafanyi vizuri, haoni mbadala wa Baleke, chama, saido, shabalala, kapombe, inonga, Kibu wala Mzamiru hata kama kama wawe wamepewa kadi ya njano, wameumia, wamechoka au wameamkaa vibaya siku hiyo. Lazima wanasimba wote wapaze sauti kuuanika ukweli huu kwa wafanya maamuzi., Simba ni mbovu sana hata hapo ilipofika ni kwahisani ya Vipers, Big Bullets, de agosto. Horoya na Wydad mbovu msimu huu. Uchochoro wa simba treet inawezekana umepatikana kwa bahatibahati tu au kwa njia ya mchongo fulani.
Wewe mbona unaumia kuliko hata wanasimba?Au Haji Manara in disguise?
Mpira una matokeo matatu.Au upo deluded na hujui chochote kuhusu mpira?Una timu yako hayo mawazo peleka huko.
Ulikuwa wapi walipofungwa 2?Na walipotolewa Champions League?Kocha uchwara!
 
Wydad imeshuka kiwango, hasa baada ya kuondokewa na wachezaji wake muhimu wa msimu uliopita. Simba wangeweza kufika nusu final kwa kupitia Wydad msimu huu kama sio ujinga wa bench la ufundi, uongozi wa Simba, Chama na Ally Salim.

Wydad waliokolewa na golikipa wao kudaka mikwaju 2 iliyopigwa vizuri na kapo Kapombe na Chama kitu ambacho Ally Salim hakuweza kukifanya kutokana na uchanga wake golini.

Uongozi wa Simba na bench la ufundi kuacha kumtumia Beno Kakolanya kwasababu za kijinga, kipuuzi, kibwege, unsporting na kichawi kukaa langoni kudaka penati na kumuamini kijana kinda kulisababisha Simba kuingia hasara kubwa sana ya kutolewa mashindanoni na timu dhaifu ya Wydad, Ningekuwa mimi ni mo ningemsaka aliyesema Beno kipa namba 2 asikae golini kwenye mashindano haya makubwa baada ya Manula kuumia.

Chama na Kapombe hawakuwa makini na kazi Yao pia ingawa penati huwa hazina mwenyewe lakini "why us" every day tutolewe robo final?

Bench la ufundi lilipaswa kumwingiza Beno kudaka japo penati TU badala ya mtoto Ally ambae aliteseka sana kujirusha chini kwa namna ileile kwa penalti zote.

Swali ni je, Simba itakuwa na ubavu wa kumzuia Inonga abaki Simba? Inonga pekee ndiye aliyepunguza idadi ya magoli siku Ile.
Msimu ukiisha Inonga ni Mwananchi.
 
Baki na Yanga yako!
 
Back
Top Bottom