Chama tawala chini ya Masisi chapoteza madaraka katika uchaguzi Botswana baada ya miaka 58

Chiluba alifanya siku nyingi,na bado CCM inadunda tu,anzisheni chama kitachounganisha dini na makabila yote,siyo chama cha wachaga na wachungaji,hamtopata nchi ng'o
tanzania hakuna chama cha kikabila na udini kilichosajiliwa.CHADEMA ni kama CCM tu, kina wanachama wa kabila zote na dini zote, acha uchuro
 
Au tuseme BDP haina urafiki na CCM, masisi anakubalije kushindwa huku akiwa ameongoza muhula mmoja? Angeomba ushauri kwa ccm wampe mbinu za kushinda kwa kishindo
 
Africa kumeanza kuchangamka.
Siyo Afrika yote, kuambuka: Botswana Hakuna utawala wenye itikadi za siasa za kikomunisti/ ujamaa, Bali kuna siasa za mfumo wa ubepari sambamba kabisa na nchi ya Afrika ya Kusini na Namibia.
Makaburu walifanya kazi kubwa sana ya kujenga mifumo ya siasa za ubepari katika nchi hizo.
 
Masisi was too arrogant hata chama chake walikuwa hawamtaki ,anajiona anajua kioa kitu
 

Attachments

  • Screenshot_20241101-110050_Chrome.jpg
    64.6 KB · Views: 1
Kipimo kikuu cha kujua uchaguzi huru na wa haki ni pale chama tawala kinaposhindwa kwenye uchaguzi lakini pale chama chochote kunapokuwa madarakani miaka nenda rudi ujue hapo hakuna uchaguzi.
True......kwenye mazingira Free and Fair hakuna chama kinaweza kujihakikisha kutawala kwa miongo kwani Binadamu wana tabia ya kuchoka na kuchokwa.
 
Sisi tubakie hivyo hivyo kuandika vya wenzetu tu kwa sisi hakuna cha kujifunza wala uthubutu wa kijiamulia nini hatutaki nini tunataka.
 
WAPIGAKURA nchini Botswana wamekikataa chama tawala cha muda mrefu cha nchi hiyo (BDP) katika matokeo ambayo yanaashiria tetemeko la ardhi la kisiasa katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa almasi kusini mwa Afrika.

BDP - Chama cha Kidemokrasia cha Botswana - kilichokuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1966 - kimeshinda kiti kimoja pekee cha ubunge kufikia mapema Ijumaa asubuhi. Inaonekana nafasi yake kuchukuliwa na Umbrella for Democratic Change yaani Mwavuli wa Mabadiliko ya Demokrasia (UDC).

Rais Mokgweetsi Masisi amekubali kushindwa, akisema ni wazi kuwa chama chake cha BDP kimeshindwa "pakubwa".

Licha ya kusimamia mabadiliko makubwa nchini Botswana, ukuaji duni wa uchumi wa hivi karibuni na ukosefu mkubwa wa ajira ulidhoofisha umaarufu wa BDP.

"Nitang’atuka kwa heshima na kushiriki katika mchakato mzuri wa kukabidhi mamlaka kabla ya kuapishwa," amesema Masisi katika mkutano na waandishi wa habari asubuhi ya leo Ijumaa.

Amewataka wafuasi wake kuwa watulivu na kuiunga mkono serikali mpya.

UDC, inayoongozwa na wakili wa haki za binadamu Duma Boko, imeshinda viti 25, kulingana na hesabu za mapema. Chama hicho kinatarajiwa kupata Zaidi ya kizingiti cha viti 31 ili kuwa na wingi wa wabunge.

Chama cha Botswana Patriotic Front (BPF) kinachoungwa mkono na Rais wa zamani Ian Khama, kimepata viti vitano huku Chama cha Botswana Congress Party (BCP) hadi sasa kimepata viti saba.

Chama chenye wingi wa wabunge ndicho kinatarajiwa kuunda serikali. Boko yuko mbioni kuwa mkuu wa nchi mara baada ya Bunge kukutana kwa mara ya kwanza.

Wafuasi wa UDC wamekuwa wakisherehekea katika mji mkuu Gaborone na maeneo mengine ya nchi. Masisi amekuwa madarakani tangu 2018 aliporithi madaraka kutoka kwa Khama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…