Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Wakuu,
Haya ni maoni binafsi kuhusiana na mienendo ya siasa za Tanzania.
1. Chama tawala-mmepewa dhamana ya kuongoza watu wa imani, itikadi, rangi, kabila zote bila kujali nafasi ya kiuchumi, kiuongozi, kiusalama, kiafya na kijinsia ili wajikwamue kutokana na lindi la umasikini ambaye ni adui mmojawapo wa maendeleo; muwavumilie wanaowakosoa kutokana na makosa ya kimfumo au binadamu, tendeeni kila mtu kwa usawa ilimaradi katiba, sheria na kanuni hazivunjwi
2. Vyama mbadala-mmepewa dhamana kubwa ya kukosoa aliyeko kwenye zamu ya uongozi, kuonesha njia, kushauri vyema jamii, kutii katiba, sheria na kanuni zinazoongoza kwenye shughuli za kiuchumi au kijamii kila siku ili kila mmoja awe na fahari na tamanio la kuishi kama mamba na kiboko kwenye dimbwi moja bila kudhuriana.
3. Vyombo vya dola - mnadhamana kubwa ya kulinda maisha ya watu na mali zao lakini kuhakikisha mipaka ya nchi ni salama. Chukueni hatua kwa yule anayekiuka katiba, sheria na kanuni izinazowaongoza katika usimamizi huo kwa weledi kuepusha uzalishaji wa hisia hasi miongoni mwa raia wengine;
4. Vyombo vya kutoa haki-mahakama, tume mbalimbali, mnawajibu wa kuhakikisha kwamba jambo ambalo mtu anastahiki au kitu anachostahili kuwa nacho anakipata kwa wakati bila vikwazo visivyo vya kisheria.
5. Raia pamoja na kustahili kutendewa haki ya asili na kisheria pia mnawajibu kutekeleza kila kinachowataka kutenda kwa ukamilifu wa haki yako
Wanasiasa msifanyiane visa vya uadui katika jamii mnatengeneza uasi wa kitamaduni ambao kuurekebisha pindi mkishindwa kuafikiana katika mambo yenye msitakabali wa taifa hamtaweza kuundoa hata kama jua likishuka kwa joto la nyuzi 0C 1,000,000