Champions League quarter-final draw: PSG face Manchester City – as it happened

Champions League quarter-final draw: PSG face Manchester City – as it happened

natamani ingetokea Bayern Munich vs Atletico Madrid, hatujawahi shuhudia hii match, japokua inaoneksna kama itaboa vile
Ndo ingekuwa Game kali kuliko Classico, Atletico sio wajinga na wachovu kama Juventus. Juventus majuzi baada ya kuchoka akaanza kupak bus na kuruhusu mashambulizi mwanzo mwisho. Atletico hawachoki aiseeee, na defense yao si mchezo.
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Atletico walicheza final na real madrid mwaka 2014, wakaongoza 1-0 hadi dakika ya 92 kwa kupaki basi, madrid wakasawazisha zikaongezwa dakika 30 wakapigwa 4-1
ni wachovu tu kama wengine, sema timu ina wachezaji wabishi wengi ila wachovu tu
 
Mkuu nafuatilia haya mambo kulko unavyofkiria, ni wazi barca alifanya vzuri game walizokutana hvi karibuni, but hapa tunaongelea quarter final ya uefa na si la liga, and by the way mpira hauangaliwi hvyo, kua kama barca kamfunga atletico la liga na uefa atamfunga. Kama ukifkiria hivyo then you know absolutely nothing about atletico katika game kama hzi
Wewe ndio hujui kitu, jamaa amekwambia kwamba Atletico iliyomtoa Barca kipindi kile ni tofauti na sasa. Barca ile ni tofauti na ya sasa.

Kwanini unakataa kupima uwezo wa ligi au mechi za ligi kisha ukashindanisha na UEFA? Unajua hata haya mashindano yanaitwa LIGI YA MABINGWA?

Angalia kwa asilimia kubwa timu inayofanya vema LA LIGA kisha tazama uwezo wake hata na UEFA.

Yote tisa, kumi ni kwamba Barca ipo ktk form vibaya sana na ni timu ambayo imewekeza pesa nyingi kwenye kikosi chake. Atletico timu bado haijatulia na kama wewe kweli unaangalia LA LIGA utaona mapungufu kwa Atletico ya sasa na ile ya zamani.

Kiwango cha ufungaji wa magoli Atletico ni hafifu, ni sawa anaweza akazuia, Je nani atafanya kazi ya kufunga? Na Barca udhaifu wake ni kupata washambuliaji wenye kasi ili kuwafunga. Griezzman pekee ndo anayeweza kuwika, atashirikiana na nani?

Atletico anaaga haya mashindano na hata Simeone msimu huu baada ya kupigwa Barca nje ndani amesema HAKUNA TIMU YA KUINYAMAZISHA BARCA MSIMU HUU.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Wanaichukulia poa sababu msimu huu wa ligi ya Spain atletico hajamfunga Barcelona
Na msimu uliopita je? Vipi Copa del rey msimu uliopita pia? Hakupigwa nje ndani?
Unazungumzia vipi uhaba wa ufungaji wa maana kwa Atletico?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
unadhan barcelona ataingia uwanjani kwa kujiamini kua keshaitoa atletico hapana, atletico ndo strongest opponent katika wote walioingia robo fainal, so barcelona wataingia kwa tahadhari kubwa sana kuliko tunavyodhani
Jukwaa la Barca nilisema kuwa huenda El Classico isiwe tamu sana kutokana na mtihani mzito uliopo mbele ya Barca. Mimi naamini kabisa Barca akili yote ipo kwa Atletico, na Game ya kwanza hapo Camp Nou Barca atacheza kufa na kupona ili ashinde. Kule ugenini ni ngumu kuizuia Barca isifunge walau goli mbili, check Game za Atletico pale kwao na Barca uone Barca ka anakosaga kumfunga kwake.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kabla ya draw ya jana nliamini kabisa kati ya timu ambazo barca asingependa kukutana nazo kwa sasa ni atletico, na jana baada ya draw mwanabodi mmoja wa barca alipohojiwa alikiri hilo. Sisemi kwamba barca hawako vizuri, maana wote tunajua uwezo wao. Ila kati ya timu zote zilizobaki including bayern, kama kuna timu inaweza kumtoa barca basi ni atletico, na wenyewe wanatambua hilo, na kwa mtazamo wangu kama barca atapita hapa bila shaka rekodi ya kuchkua ubingwa mfululizo tangu hii michuano ianze kuitwa uefa itakua inamuhusu, maana sioni kama kuna mwingine anaeweza kumzuia kufanya hivyo zaidi ya atletico ya diego simeone
Wanachoomba Barca ni wasipate majeruhi, hata Atletico anajua kuwa mpinzani wake mkubwa ni Barca, hakupenda akutane nae kabisa.

Kinachomhofu sana Atletico ni safu yake ya ushambuliaji, bado hakuna mtu wa kusimama wa kueleweka kuweka mpira wavuni.

Barca ataingia uwanjani huku Messi na Neymar wakijua kwamba ndani ya nafasi 5 basi wamefunga 4.

Game itakuwa ngumu sana, hata ikiwa droo mechi ya kwanza haimaanishi kwamba Barca katoka au Atletico kapita. Ila sioni kama draw itapatikana kirahisi, kumzuia Messi na Neymar wasikufunge ni ngumu sana.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Atletico walicheza final na real madrid mwaka 2014, wakaongoza 1-0 hadi dakika ya 92 kwa kupaki basi, madrid wakasawazisha zikaongezwa dakika 30 wakapigwa 4-1
ni wachovu tu kama wengine, sema timu ina wachezaji wabishi wengi ila wachovu tu
Kama unaangalia Game hiyo tu basi tuangalie uwezo wao wa miaka ya hivi karibuni, Real kaumia mno kuliko Atletico.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kama unaangalia Game hiyo tu basi tuangalie uwezo wao wa miaka ya hivi karibuni, Real kaumia mno kuliko Atletico.
no lengo langu sio kuwalinganisha na real, nilitka kusema pia wao huwa wanachoka
 
Hoja isiyo na mashiko, hiyo draw unayosema inachanganywa ni siasa za kimpira tu. Ila Draw inapangwa na wao wenyewe ili kuleta faida kwa shirikisho.
Madrid ina mchango mkubwa ktk hili kombe, we jiulize Mtoano kapewa Roma, Robo pia anapewa huyu dogo. Kama sio mbeleko ni nini?

Mkuu hiyo siyo hoja kama unavyoita wewe, that's the fact. Draw imechezeshwa mbele ya macho yetu tumeona wote. Hayo unayojiminisha wewe na imani yako hayatuhusu. Mbona quarter final ya msimu uliopita ilikuwa Real Madrid vs Atletico na kila mtu alichukulia kawaida tu. Why always drama starts with You Cules?
 
Na msimu uliopita je? Vipi Copa del rey msimu uliopita pia? Hakupigwa nje ndani?
Unazungumzia vipi uhaba wa ufungaji wa maana kwa Atletico?
Nakumbuka vyote. Ila mimi naamini hawa Atletico hawatakubali kuwa wateja wenu kirahisi hivyo safari kwenye uefa. Ingawa mechi itakuwa ngumu
 
Huu utaratibu sio mzur wa kuvuruga kila hatua, zamani walikuwa wanavuruga baada ya kupata timu 16 then fixture inakuwa inajulikana. Warudishe utaratibu wa zamani. Utaratibu wa sasa unasababisha timu zisizokuwa na uwezo kufika hatua kubwa kibahati bahati, ona sasa hivi benfica na wofsburg zna ubora gani wa kuzd Asernal na Chelsea?
Ni bora sana kuliko hizo timu za ligi ya mchangani kwenu.
 
Mkuu hiyo siyo hoja kama unavyoita wewe, that's the fact. Draw imechezeshwa mbele ya macho yetu tumeona wote. Hayo unayojiminisha wewe na imani yako hayatuhusu. Mbona quarter final ya msimu uliopita ilikuwa Real Madrid vs Atletico na kila mtu alichukulia kawaida tu. Why always drama starts with You Cules?
Achana na majuha hayo kazi kulalamika tu kila kitu kiko wazi kwenye kuchezesha draw.
 
Ndo ingekuwa Game kali kuliko Classico, Atletico sio wajinga na wachovu kama Juventus. Juventus majuzi baada ya kuchoka akaanza kupak bus na kuruhusu mashambulizi mwanzo mwisho. Atletico hawachoki aiseeee, na defense yao si mchezo.
Umejisahaulisha fainali aliyokutana na Madrid!? Ramos aliwanyonyoa dkk ya ngapi vile?kisha mvua ya magoli ikaanza kumiminika.
 
Atletico ni wepesi sana kwa barca ya sasa, nou camp tutauona udhaifu wa atletic
 
Wako wapi wale waliokua wanabisha kuhusu barca kutolewa na atletico? Wote wamekimbia
 
Ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindanno kuliko Barcelona kumfunga Atlético de Madrid...Namaanisha Barcelona keshatoka kweli hili kombe kuchukua maraa ya pili ni ngumu..

Uzuri wa champions league yeyote anaweza kuvuka hatua hiyo....hakuna underdogs huko....kumbuka 2012...kumbuka juve alivyomtoa Madrid...
Nimejikumbuka PNC uko wapi?
 
Back
Top Bottom