Mkuu mpira wa sasa umebadilika, na unahitaji uwekezaji mkubwa. Miaka ya hivi karibuni berlusconi alikua mgumu kufungua pochi, na hiyo ikapelekea sisi kusaini mediocre players tofauti na ilivyokua zamani, ambapo milan ilikua ni kivutio cha wachezaji wakubwa. Kinachohitajika pale ni uwekezaji, na hilo lishaonekana na linashughulikiwa. Kuna jamaa anaitwa mr bee alitaka kuchkua hisa za kutosha toka kwa berlusconi, ila kuna mambo hayakua sawa. Kwa sasa kuna mpango wa kuuza 50% ya hisa zote kwa wachina ambao wako backed na serikali yao. Hiyo italeta mpunga wa kutosha, na ndipo timu itakapojengwa kucompete ktk level kubwa kama ilivyokua awali