CHAN2021: Mchezo umemalizika kwa Taifa Stars kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zambia

Kwa jinsi timu inavyocheza, mbinu za kocha wetu jumlisha na uzembe kupitiliza wa wachezaji wetu, nachelea kusema sidhani kama tutapata hata point 1 kwenye group letu.

Soka la Tanzania, bila ya wachezaji wa kigeni ni bure kabisa. Leo Taifa stars wamecheza kama Mbao Fc.

Ni wakati sasa wa kwenda kumuomba msamaha mzee Mwinyi kabla hajatangulia, msemo wa kichwa cha mwendawazimu unaendelea kututesa sana!
 
Taifa stars imeanza vibaya huko Cameroon dhidi ya Zambia kwa kulala 2-0.
Nadhani rais atatekeleza ahadi Yake ya kutumbua waziri wa michezo ingawa hakucheza.
Kuna msemo kwamba, kuna watu wakiwa na nyundo, wanafikiri tatizo lolote ni msumari, walimalize kwa kugonga kwa nyundo.

Maana yake, hata wakiwashwa korodani watataka kumaliza tatizo hilo kwa kujigonga korodani kwa nyundo.

Tumbua ni tool moja tu katika toolbox, kama nyundo.

Kuna matatizo mengine, kama kuwashwa korodani, hayamalizwi kwa nyundo.

Kuna matatizo mengine hayamalizwi kwa tumbua tumbua.
 
Kipindi cha dikteta wa kifashisti Benitho Mussolini Italy ilichukua kombe la dunia mara mbili mfululizo.
Mwaka 1934 na 1938, unajua aliwaambia nini wachezaji na makocha kabla ya mechi ???
 
Kipindi cha dikteta wa kifashisti Benitho Mussolini Italy ilichukua kombe la dunia mara mbili mfululizo.
Mwaka 1934 na 1938, unajua aliwaambia nini wachezaji na makocha kabla ya mechi ???
tushushie simulizi mwalimu...
vipi jamaa aliwaahidi kifo kwa kila mchezaji?
 
Kipindi cha dikteta wa kifashisti Benitho Mussolini Italy ilichukua kombe la dunia mara mbili mfululizo.
Mwaka 1934 na 1938, unajua aliwaambia nini wachezaji na makocha kabla ya mechi ???
Eeh
 
Wakati mpira wa Zambia vs Tanzania unaendelea nikasikia commentary anasema "Baada ya Micho kuita kikosi chake Cha CHAN wadau wengi wa soka Zambia walimkosoa kwa kuacha baadhi ya wachezaji, kitendo ambacho kilipelekea Micho awambie wadau wa soka Zambia waite kikosi chao wao ili ipigwe friendly match na kikosi chake, baada ya hiyo mechi Micho aliwaongeza wachezaji wa 5 kwenye kikosi chake kutoka kikosi hicho cha wadau wa soka"

Kwangu Mimi Kuna kitu Cha kujifunza hapa kwa nchi zetu zinazoendelea katika soka ni vizuri kocha kuwa karbu Sana na wadau wa soka na kuwasikiliza walau kidgo, maana wao ndo wanawajua wachezaji kuliko kocha, kocha ametoka Europe, America etc hawezi jua wachezaji wa bongo kuliko wabongo wenyewe

Rejea world cup 2018, Blanc alilaumiwa sana kwa kumucha Giroud lakn akabeba ubingwa na Giroud wake, kumbuka Giroud alizungukwa na Kante, Pogba, Griezmann, Mbappe, Matudi etc yani kifupi quality na experience ilikuwa nayo ya kutosha.. TZ ya leo ilikuwa na wachezaji non experience 9, hivi unategemea kupata matokeo hapo au ndo matokeo ya kimazabe zabe

Ni muda wa kubadilika kwa makocha wetu hasa wa kigeni, kuwasikiliza wadau hata kwa 1%, mtu anaweza akawa hajui ku.koachi lakn haimfanyi kutojua Metacha, Muhhamed Hussein, Mzamiru etc Ni wachezaji wazuri

NOTE: Hii nchi ishakuwa ya kusifu na kuabudu Sana, kesho utasikia wanahabari za michezo wakimtetea Etienne wakati Kama Zambia wangekuwa makin Leo hii ngoma ingekuwa 4+ leo
 
Kuna shida kubwa, hivi kwanini kocha ameita vijana wengi bila walau kuweka wakongwe kama akina Dilunga, Miraji n.k? Kuna wachezaji kuwa Simba/Yanga tu kuna quality inaongezeka kutokana na presha ya timu hizo.

Lakini pia uwezo wa kocha unatia shaka sana ...
 
Kipindi cha dikteta wa kifashisti Benitho Mussolini Italy ilichukua kombe la dunia mara mbili mfululizo.
Mwaka 1934 na 1938, unajua aliwaambia nini wachezaji na makocha kabla ya mechi ???
Hata watoto wa Saddam Husein yule Uday&Qusay walikua wanawachapa viboko wachezaji wa timu yao ya taifa kule kwny vyumba vya wachezaji.

Daah ila sio poa lkn.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…