Changamkia fursa ya helping hands international H2i

Changamkia fursa ya helping hands international H2i

Naipenda hii thread maana alieianzisha ndie anaejichangia mwenyewe kila mara....masikini kawa kama yatima...mkuu nipo tayari kutapeliwa njoo pm uniibie yaishe.
Anafanya hivyo ili thread yake ibakie relevant. Pyramid scheme yake haieleweki na badala ya kuieleza vizuri watu wakaielewa naona amegeukia mipasho kama Hadija Kopa. Anaporomosha mipasho ya kimotivational speakers kama hana akili nzuri.

No buying...
No selling...

Sasa sijui pesa zinapatikanaje. Maajabu ya dunia !!!

Watu wameshaamshwa na utitiri wa pyramid schemes za akina GNLD, ORIFLAME, RIFARO, TREVO, FOREVER LIVING na wengineo na kuwapata kwenye hizi Schemes sasa ni ngumu. Atashusha mipasho na kujijibu mwenyewe thread nzima jamaa wamepotezea tu. Sad !!!
 
FB_IMG_1484387441926.jpg
 
Naipenda hii thread maana alieianzisha ndie anaejichangia mwenyewe kila mara....masikini kawa kama yatima...mkuu nipo tayari kutapeliwa njoo pm uniibie yaishe.
Mkuu wise boy, comment yako imenifanya nicheke kwa sauti mpaka watu wananishangaa.
Kiufupi ni hivi, jana nimeunganishwa kwenye group la WhatsApp na nikakuta hii mada inayohusu kujiunga na H2i. Kiufupi sijaelewa. Nikaamua kugoogle nakitana inanileta JF nako nakutana na jamaa anajaza thread peke yake.
Anatakiwa afafanue ukishaingia na wakapata kiingilio chako utakua na majukumu gani kama mwanachama? Au ndio kazi unayoifanya ni kuleta watu tu?
Kweli hizi Riffaro zinarudi kwa aina nyingine aisee. 'Mvinyo ileile ila imebadilishiwa chupa tu'.
 
Back
Top Bottom