Changamoto 3 kubwa za mapenzi ya mbalimbali

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Mapenzi ya mbalimbali yanajumuisha;

Mapenzi na mtu wa mbali na unapoishi (mkoa mwingine/ nchi nyingine).
Mapenzi na mtu mtandaoni na hujawahi kukutana naye.
Mapenzi na mtu ambaye ratiba zenu haziruhusu kukutana kwa muda mrefu.

Kwenye mapenzi haya inabidi uwe makini, na ujue changamoto zake.

Kupungua mapenzi ya kimwili.
Hata ule ukaribu mliokua nao mwanzo unapungua.
Raha ya mahusiano ni kuweza kumshika, kumkumbatia na kumpeti mpenzi wako. Iko kikikosekana unaweza jihisi mpweke japo una mpenzi.

Mpenzi wako anaweza kukusaliti.
Kama binadamu tuna hamu ya mapenzi.
Lakini mkiwa mbali na mpenzi wako mapenzi ya mwili hakuna. Endapo mpenzi wako hawezi kujiongoza vizuri na hajui thamani ya uaminifu, ni rahisi kukusaliti. Hasa pale atakapokua na hamu ya mapenzi sana.

Pengine anaweza asikusaliti lakini wewe ndo ukabaki na mawazo.

Mawazo kwamba atakusaliti. Ili kumfanya asikusaliti unaanza kufanya vitu nje ya mipaka yako. Unajikuta king’ang’anizi ili tu usisalitiwe.
Kama vile kuangalia simu kila saa kama umejibiwa sms.
Kumpigia mpenzi wako kila muda ili ujisikie amani.
Au kukosa amani kiujumla sababu ya mawazo kama mpenzi wako bado yupo nawe.

Kuchelewa kutatua changamoto zenu.
Kwanza sababu ya mawasiliano kidogo, pili umbali.
Mkiwa mbali mbali mnaweza kuona mnaendana sana. Sababu mnajuana juu juu. Bila kujua huyo mwenzio ana shida gani endapo mkiwa karibu karibu.

Pia ni rahisi kwa uliyenaye kuigiza kwa muda mchache ambao mnawasiliana, na kukufanya uone umepata.

Muhimu ni kujua malengo yako kwenye mapenzi kabla ya kuwa kwenye mapenzi yoyote. Ili usijikute unapoteza muda wako na mtu ambaye huendani naye.
 
Yapo mapenzi mengine yanahitaji umbali Ili yadumu mfano mke mbabe mme mbabe hawawezi kaa nyumba moja kwa amani yafaa waishi mbalimbali ikibidi hata miji tofauti.
Mwanadamu ni roho ugomvi utokea kwa sababu ya Roho zenu kutoendana. Pana wapenzi wanandoa hawawezi kaa pamoja mwezi pasipokuvurugana.
Watu kama hawa Ili wadumu tiba ni distance.
Ishu ya uaminifu sio suala la distance,ni ishu ya tabia.
Pana dada anasema yeye na mme wake hawaishi pamoja lazima wazinguane Mme Arusha kikazi yeye yupo mkoa mwingine kikazi pia na maisha yanaendelea.
Fahari wawili hawakai zizi moja.
Huwezi ishi na feminist nyumba moja mkaenda busara ni bora ukeep distance.
 
Daaadh mpka chozi hii mada imegusa inaumaaa aje mpenzi wangu sijamuona toka August
last year....💔💔💔

Back
Top Bottom