sasa kwanini wakishafanya hiyo michakato hawakupi mrejesho kwanini hukutunukiwa? au wewe unaona kawaida tu. Kuna mkataba kama umeandika bei ya chini ukashindwa kusambaza si unalipia hasara
Huu mfumo umetengenezwa na binadamu na kwa matumizi ya binadamu. Hapa inabidi uelewe tu kuwa kuna mapungufu, na watu watatumia hayo mapungufu ya mfumo ili kupitisha mambo yao.
Shida kubwa ambayo PPRA wameshindwa kuitatua, ni kuufanyia mafunzo mapana huu mfumo. Hata zile video za training huwa hazijibu maswali basic kama hayo.
Ninakushauri, siku nyingine ukiomba tender, uwe na kawaida ya kuulizia imekuwaje ili kuweza kujua mrejesho na nini uboreshe katika uombaji.