Changamoto Kubwa Kwa Jamii - Nafasi Nyingi za Uongozi Zinashikiliwa na Wasio Na Sifa za Uongozi

Changamoto Kubwa Kwa Jamii - Nafasi Nyingi za Uongozi Zinashikiliwa na Wasio Na Sifa za Uongozi

Mchanya

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
997
Reaction score
1,568
Jamii yetu ya Tanzania kama zilivyo jamii zingine, inakabiliwa na changamoto lukuki, tofauti iliyopo kati ya jamii yetu na zingine ni aina ya uongozi bora na jinsi unavyojikita katika kutatua changamoto hizo kwa wananchi wake, na hatimaye kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi wao.

Kuwa mwadilifu, mbunifu, mwaminifu, mwenye uwezo wa kuwasiliana, mwajibikaji, anayekubali kukosolewa, muwazi na mkweli, kuwa msikilizaji mzuri, mwenye kujiamini, mwenye kupenda majadiliano badala ya kuamrisha, mwenye kutenda haki kwa wote bila kupindisha, anayeweza kudhibiti hisia zake, asiye mwoga, mwenye hekima, busara na anayeonesha shukurani, ni baadhi ya sifa za kiongozi bora. Sifa hizi za kuwa kiongozi bora unazipata kutokana na mafunzo au kama una karama au kipaji ulichozaliwa nacho.

Tuna changamoto nyingi ambazo viongozi wetu walipaswa kuwa mstari wa mbele kuwa wabunifu katika kuzitatua, lakini viongozi wengi wanashindwa kwasababu aidha wameshikilia nafasi za uongozi wakiwa hawana sifa za uongozi, au wamewekwa tu, na matokeo yake ni wananchi kuendelea kutaabika na nchi na jamii yote kukosa mwelekeo na maendeleo.

Kuna mifano mingi inayoonesha jinsi viongozi wanavyobabaika katika kutatua changamoto nyepesi na ndogo kabisa maishani, wakati mwingine wanakuwa wakali na kutumia mabavu mahali ambapo hekima na busara ndogo tu ilihitaji kutumika.

Jaribu kuangalia wale walioshikilia nafasi za uongozi kama wanazo sifa za kuwa viongozi kwenye nafasi hizo au wapo tu? mfano kwenye ngazi zote, kama familia, ofisini, wilayani, mkoani, wizarani hadi kwenye serikali kuu.

Jaribu kuangali jinsi wananchi wanavyotaabika katika kupata huduma za jamii za afya hospitalini, usalama na elimu, hata upatikanaji wa ajira, na hali ya ugumu wa maisha hadi unajiuliza viongozi wako wapi?

Wewe unaonaje? Tunao viongozi wenye sifa hizo kweli?
 
Tatizo si kukosa sifa kwa viongozi tu.

Kuna tatizo kubwa katika mfumo mzima wa kupata uongozi.

Imekuwa kama vile zile zinazotakiwa kuwa sifa za uongozi, umezitaja hapo juu, kwa mfano uadilifu, ndizo zinamkosesha mtu uongozi. Halafu zile sifa za kumkosesha mtu uongozi, kama kupenda rushwa, ndizo zinamfanya mtu apate uongozi.

Kuna mzee mmoja muadilifu sana, alistaafu, akaombwa kugombea ubunge. Alichokutana nacho kwenye mchakato aliona kuwa anatakiwa kusema uongo sana, anatakiwa kuchukua pesa chafu sana, na alitakuwa kutumia makanisa sana katika kufanya kampeni za siasa. Akaona yote hayo hakubaliani nayo, akashindwa kugombea ubunge.

Hapo akaja mtu ambaye yeye haoni tabu kufanya yote matatu hayo, akafanya, akapata ubunge. Na hao wanaopata ubunge ndio wanaokwenda kuwa mawaziri na marais.

Mfumo wenyewe umekaa kutompandisha mtu mwenye uadilifu na kumpandisha mla rushwa asiye muadilifu.
 
Umenena kweli kabisa, inasikitisha sana kwamba nchi yetu iliyojaa rasilimali lukuki lakini haiwezi kuendelea kwa mtindo huu uliopo, swali kubwa ni tufanyeje sasa!!??
 
Hii ipo hata kwa taaluma muhimu, unakuta mtu ni mwalimu lakini codes na ethics za ualimu hana. Uwezo wa kuyatawala maarifa anayofundisha kwa wanafunzi ni wa kubabaisha
 
Back
Top Bottom