Changamoto na mitihani unayopitia haipo kwa bahati mbaya

Smile Digital Stationery

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2024
Posts
202
Reaction score
317
Hello wana JF;

Leo nimekuja na hii Mada kwaajili ya kujifariji na kuwafariji wengine,

Ipo hivi; Dunia ni kama Darasa, na kila mwanafunzi ana uelewa wake katika kumwelewa Mwalimu.

Sote katika Binadamu tunapitia changamoto mbalimbali, na kila mmoja ana changamoto yake anayoipitia, wapo wanaopitia changamoto za maradhi ya aina mbalimbali (Mwenyezi Mungu awaponye🤲). Lakin pia wapo wanaopitia changamoto za ukata wa kifedha na ufukara, kuuguza n.k.

Changamoto hizo ndo naweza ziita (Mitihani).

Kila binadamu lazima apitia changamoto zake na kama mpaka sasa hujazipitia basi zipo mbele yako utakutana nazo kabla hujaondoka kwenye hii dunia (kufa).

Ila kaa ukiamini kwamba Mungu hakupi mtihani ambao huwezi kuujibu, hakupi magumu ambayo huwezi kuyakabili.
Na hayafanyiki hayo ila kujenga kiakili, kifikra, hekima na busara. Na kubwa zaidi ni kipimo kwako kwa Muumba wako kama utamshukuru au utamkufuru?

Ndugu zangu; Changamoto na mitihani ulloipitia ama ulonayo sasa hutakiwi kuijutia maana isingemkuta mwengine badala yako ila ni wewe mwenyewe na M/Mungu anayekujua vizuri kaona kwamba utaimudu, sasa ni jukumu lako kuthibitisha hilo.
Ridhika na hali yako na usipende kulalamika kwa wengine maana hawatokusaidia ila unatakiwa kujisaidia wewe mwenyewe kwa kumtegemea M/Mungu tuu.
Amini kwamba, wewe kuwepo tuu hapa duniani tayari wewe ni mshindi na ulishashinda wengine kama Milioni 200 hadi milioni 500 (kama sijakosea) pale madaktari wanaposema kuwa katika kujamiiana Mwanaume hutema mbegu za uzazi (sperms) zinazokadiriwa kufikia idadi hyo na mbegu moja tuu itakayowahi kufikia ndio inayoruhusiwa kuingia kwenye yai la mwanamke kwaajili ya kutunga kwa mimba. Sasa hyo mbegu moja iliyowahi kulifikia yai ni mimi na nyie, hvyo tulishashinda tokea tukiwa hatujitambui.

Kwahyo tusikubali kushindwa kwa yoote magumu tunayopitia, kwani wahenga wanasema NYAKATI NGUMU HAZIDUMU.

Kila mmoja ana mitihani yake, na pindi wewe unajipojiona kuwa yakwako ni migumu zaidi pindi utakaposikia mwengine akielezea yakwake utajiona kumbe yakwako ni chamtoto!?.

Mf. Munamuona ndg Tundu Lisu?, Hiv mnadhani kuwa anayoyapitia anayapitia kwa bahati mbaya?, Laahasha, ile ni mitihani alopangiwa aje kuipitia ktk hii dunia na hyo haitadumu itafika nyakati itapita na ataenjoy nyakati nzuri, na kingne kama unajua kuunganisha dot basi utaniafiki kuwa kuna mission amepangiwa kuikamilisha kabla ya umauti wake na ndo maana kipindi kile hakufa, ile haikutokea kwa bahati mbaya.🤝

Nimalizie kwa kusema; Kwa changamoto na mitihani ya kidunia uliyonayo, 💪 Kaza, kuwa na subra na kabiliana nazo katika njia sahihi, na isiwe ni chanzo cha kupotea njia.
 
🙏
 
Hakika, dunia ni darasa la maisha ambalo kila mmoja anajifunza/atajifunza kupitia changamoto zake. Remember, God never gives a burden heavier than you can carry. Kila mtihani ni fursa ya kujifunza, kuimarika, na kuonyesha nguvu zako halisi. Stay patient, trust the process, and keep your faith strong.

Success and peace are on the other side of hardship. Don’t give up!
 
.

Hizi ni kauli za kujifariji tu mkuu. Nyakati ngumu zinadumu pia wakati mwingine. Kwani hakuna ambao hupitia nyakati ngumu na mwishowe hufa kwazo?

Si kila anayepitia wakati mgumu huishia kuwa na joyful ending
 
Hakika, dunia ni darasa la maisha ambalo kila mmoja anajifunza/atajifunza kupitia changamoto zake. Remember, God never gives a burden heavier than you can carry. Kila mtihani ni fursa ya kujifunza, kuimarika, na kuonyesha nguvu zako halisi. Stay patient, trust the process, and keep your faith strong.

Success and peace are on the other side of hardship. Don’t give up!
Upo sahihi kabisa swahiba
 
Mbaya itakuwa kama nyakati nzuri ndo ulishazipitia na zimeisha! Phase 2 ndo hiyo, Kamata - Mbagala, watu wanapandia madirishani yaani!
 
Back
Top Bottom