Tanziti
Member
- Sep 15, 2022
- 6
- 2
Wakati sisi tukila kushiba na kulala pazuri kwenye majumba mazuri kuna mtoto wa mika 7 hadi 17 analala nje ya kibalaza bila shuka wala godolo! Mimi binafsi huwa najiuza hawa Watoto wanatokaje majumbani mwao nakuja kulanda landa mtaani kwa akili ya haraka unaweza kuanza kulaumu wazazi ama walezi lakin lakin yapo mezila mengi yanayowafanya Watoto hawa kuzikimbia familia zao yakiwemo unyanyasaji,hali ngumu za familia zao, kufanyishwa kazi ngumu, malezi mabaya,na zingine huchangiwa na jamii yenyewe.
Mimi huwa najiuliza na ninapowaona Watoto wakiume tu ndio hulanda landa mitaani huku nikishuhudia idadi ndogo sana na kwa nadra ya mtoto wakike akizulura mtaani bila makazi na huwa nikimuona najiuliza huyu usiku analala wapi na anakumbana na changamoto gani!, huwa najiuliza ni Watoto wakiume tu ndio huzikimbia familia zao jibu nihapana wapo Watoto wakike pia hukimbia familia zao lakin hatuwaoni mtaani je, huwa wanaenda wap?
Kwamafikilio ya haraka hujikuta wakiingia katika ajira za utotoni , ndoa za utotoni pamona na kuuzwa na kutumikishwa Pamoja nakufanyiwa vitendo vya ukatili katika kazi mbalimbali nje na ndani ya nchi. Wakati sisi tukifurahi na Watoto wetu majumbani tukiwapeleka shule za gharama wakila na kulala pazuri tukiwapenda na kuwatoa out nje na ndani ya nchi!
Kuna mtoto mwenzake analala nje bila shuka na nguo zake zikiwa zimechanika na mwenye kutia huruma kulingana njaa aliyonayo akisubili watu wabakize vyakula vyakula mezani nayeye amalizie! Wanajiona wametengwa na jamii na hawafai na ndio maana siku za Karibuni tumekuwa tukishudia makundi mbalimbali ya kiharifu yakihusisha Watoto na vijana wadogo kabisa.
Niwajibu wetu sasa kama jamii kulibeba hili na kuwasaidi Watoto hawa badala ya kuwaona waharifu na kuwanyanyapaa tukiwahisi waharifu na wasiofaa katikati yetu. Jamii imeyageuzia kisogo mambo haya kwa siku za Karibuni na kuona kila mmoja sio jukumu lake na halimhusu na badala yake tumekuwa tukisubiri kulaamu na kulalamika, Kama jamii Watoto hawa wanatokea kwenye familia zetu, majirani zetu, mitaa yetu na tumekuwa hatuwajibiki ipasavyo kukomesha changamoto hzi ambazo huwaleta Watoto mtaani ikiwemo mifarako ya wazazi,mimba za utotoni ambazo hupelekea Watoto kulelewa na bibi na babu, mmomonyoko wa maadili,vifo vya wazazi na mengine. Katika kutatua hili la Watoto kuzulula mtaani na wengi wao wakiwa na vipaji na taranta mbali mbali nimekuja na wazo la kuwaweka Watoto hawa Pamoja na kuwasikiliza na kuwaendeleza katika talanta zao kama ifuatavyo:-
Nipo tayari kuwafanya Watoto wa mtaani kufurahi na kufufua matumaini na ndoto zao wewe Je?.
Imeandikwa na Pius Beatus
Asante.

- Kuanzisha matamasha kila mtaa yatakao wahusisha Watoto wote lakin yenye kuwalenga Zaidi Watoto hawa wamtaani, matamsha kama kuanzisha mashindano ya mpira, mziki, riadha nk. Watoto wengi hupenda sana michezo hivyo kupitia njii hii itakuwa njia rahisi kuwapata, hivyo kutupa urahisi wa kuwasikiliza changamoto zao walikotoka na kuzitatua inapobidi kwa kushilikiana na mamlaka husika kwa sababu sio wote wanachangamoto za kifamilia wengine wazazi wao wameshinwa kuwajibika ipasavyo kupitia mamlaka zitamtaka mzazi kutimiza wajibu wake kwa mtoto ikiwemo kumtunza.
- Kuwaweka Pamoja Watoto hawa na kuwaendeleza kielimu kwa kushilikiana na mashilika mbali mbali ya kusaidia Watoto. Binafsi naamini Watoto hawa na vipaji na talanta kubwa wakiendelezwa tutapata watu wakubwa na nguvu kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo ya Nchi.
- Kuwatafutia academy mbalimbali kulingana ta talanta zao nakuwaendeleza hadi kuzifikia ndoto zao binafsi nipo tayari kuwalipia Watoto 100 wasome na kujifunza wanachokipenda na amini kila kitu huanza na mmoja wapo wengi watavutiwa na hili nakuniunga mkono nahiyo tutakuwa tumeisaidia jamii yetu na kutumiza ndoto za wengi.
- Kuwaweka Pamoja na kuwapa elimu ya jinsia na kujitambua, Watoto hawa wamekuwa wahanga wa madawa ya kulevya, mimba za utotoni, uharifu, kuambukizwa maradhi mbalimbali ikiwemo ukimwi. Hii nikutokana na kukosa elimu sahihi kwa sababu ya kutengwa nakukosa elimu mhimu ya kujitambu na hivyo kuendelea kuzalisha kukuza jamii masikini na kukosa nguvu kazi mhimu ya kulitumikia taifa.

Upvote
0