KERO Changamoto na unyonyaji wa wafanyakazi - Jambo Group of Companies, Shinyanga

KERO Changamoto na unyonyaji wa wafanyakazi - Jambo Group of Companies, Shinyanga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi pia nilikuwa mfanyakazi wa Jambo Group of Companies, hivyo haya ninayoyaeleza siyo taarifa ambazo nimezisikia tu kutoka kwa watu wengine, bali ni mambo ambayo nimeyaona, nimeyapitia na nimefanya kazi katika mazingira hayo mwenyewe. Hadi sasa mimi mwenyewe ni mdaiwa wa kampuni kutokana na mfumo huu wa kazi.

Kampuni ya Jambo Group of Companies iliyopo Shinyanga inaonekana kuwa inawa-exploit wafanyakazi wake, hususani wafanyakazi wa kitengo cha Sales na wapakiaji wa mizigo.

Kuna changamoto kubwa ya kuchelewesha mishahara na kutowalipa baadhi ya wafanyakazi, na wanapodai pesa zao wanaambiwa kuwa kampuni haiwatambui na kwamba wao siyo wafanyakazi wa kampuni. Hii inatokana na kutowapa wafanyakazi mikataba ya ajira.

Kazi ya Sales ina risk mbalimbali kama vile damage ya bidhaa, kuumwa ukiwa safarini na risk nyingine zinazoweza kutokea wakati wa kazi. Sasa hakuna mkataba unaoeleza hayo yote au kueleza endapo risk nyingine zikitokea nini kinafanyika na nani anawajibika.

Wao wanachokifanya, ukitokea products zimepata damage, wanasema wewe Sales ulipe gharama na wanakuandikia deni, ikiwa hakuna mkataba unaobainisha hayo. Mfanyakazi anaweza kubebeshwa deni kutokana na bidhaa kuharibika bila kuwa na utaratibu wa wazi unaoeleza ni katika mazingira gani mfanyakazi anapaswa kuwajibika kwa uharibifu huo.

Watu wa Sales wanatoka na gari kubwa kuzunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania mpaka mzigo wa juice, pipi, biskuti na maziwa uishe. Kama haujaisha, wanasema hakuna kurudi kiwandani. Watu wanakaa kwenye mauzo mpaka mzigo uishe, na wakati mwingine mtu anaweza kukaa zaidi ya siku 30 akiwa kwenye mauzo.

Expense za sokoni kama kula, kulala, parking ya gari lao wenyewe na ushuru ni juu yako wewe mtu wa Sales. Expense inazidi hata mshahara.

Hii hali inapelekea watu wa Sales kuwaandikia madeni, hali ya kuwa watu wanatumia pesa zao wenyewe katika kutafuta soko na kuuza bidhaa za kampuni. Wanafanya kazi katika mikoa ambayo siyo wenyeji wao, hawana ndugu wala sehemu ya bure ya kukaa. Sometimes wanaenda mpaka remote areas, hivyo wanatumia pesa zao kwa ajili ya chakula, malazi, parking, ushuru na gharama nyingine za safari na mauzo.

Pia damage ya bidhaa inapelekea wafanyakazi kuwa na madeni wakati mtu wa Sales yeye hajaharibu mzigo. Mzigo wanapanga wao kwenye gari na dereva ni wa kampuni yao. Sometimes gari inapita kwenye rough roads/barabara mbovu, hali ambayo inaweza kupelekea bidhaa kupata damage, lakini hawataki kusikia hilo. Badala yake, mfanyakazi wa Sales anaambiwa alipe gharama ya bidhaa iliyoharibika na anaandikiwa deni.

Pia wanatishia wafanyakazi kwa kuwafunga, eti kila siku polisi wanakuja kuripoti kiwandani kwao. Hii imekuwa kama sehemu ya kujigamba kwamba polisi ni wao au kwamba wana connection na polisi, jambo ambalo linaweza kuwafanya wafanyakazi kuogopa kudai haki zao au kuhoji masuala yanayowahusu.

Sales wanauza mzigo wa zaidi ya TZS milioni 30 hadi TZS milioni 60, lakini total ya commission haizidi TZS laki 3 hadi TZS laki 5, ambayo ni kati ya takribani 1% hadi 1.7%, na wakati mwingine hata kufikia 2%, jambo ambalo linahitaji kuchunguzwa kama linaendana na makubaliano na taratibu zinazotakiwa katika ajira na mfumo wa commission.

Kama nilivyosema, mimi si mtu ambaye nasimulia jambo nililosikia kwa mtu mwingine. Nimekuwa ndani ya mfumo huu. Nimefanya kazi hii. Nimebeba mzigo. Nimezunguka kwenye mauzo. Nimetumia gharama zangu binafsi. Nimeuza bidhaa za kampuni. Nimebank fedha za kampuni. Na mpaka sasa mimi mwenyewe ni mdaiwa.

WANA-EXPLOIT WATU. WANAANGALIA UPANDE WAO TU, WAKATI WAFANYAKAZI NDIYO WANAOBEBA MZIGO MKUBWA WA KAZI NA RISKS NYINGI.

IMG-20260306-WA0000.jpg
20260207_094622.jpg
20260207_092105.jpg
20260207_092255.jpg
 
Duuh polee sanaa, hope wahusika wataona na kufanyia marekebisho na kupatikana suluhisho.
 
Watu wa Sales wanatoka na gari kubwa kuzunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania mpaka mzigo wa juice, pipi, biskuti na maziwa uishe. Kama haujaisha, wanasema hakuna kurudi kiwandani. Watu wanakaa kwenye mauzo mpaka mzigo uishe, na wakati mwingine mtu anaweza kukaa zaidi ya siku 30 akiwa kwenye mauzo.
Sas hili Lina shida gani hata ukikaa mwaka mzima
 
Mwarabu anaejali wafanyakazi wake ni GSM pekee

Labda uwe unatembea na mmoja ya wale waarabu. Hapo sawa. Wanalalamika sana hawa watu ambao wamekaza hawataki kuliwa. Maisha ni magumu. Kuna madogo kila mara wanaomba pesa kwa kaka zao. Mishahara kidogo. Na wale waaarabu wanataka wawe wanawala nyota.
 
Sales wanauza mzigo wa zaidi ya TZS milioni 30 hadi TZS milioni 60, lakini total ya commission haizidi TZS laki 3 hadi TZS laki 5, ambayo ni kati ya takribani 1% hadi 1.7%, na wakati mwingine hata kufikia 2%, jambo ambalo linahitaji kuchunguzwa kama linaendana na makubaliano na taratibu zinazotakiwa katika ajira na mfumo wa commission.
Kwani hizo kazi mmelazimishwa kufanya wazee? Mkalimw mache kulalamika kwenye biashara za watu
 
Mauzo ya mzigo unakaa nayo au kila utakachouza unatia bank? Huna mkataba na unabaki na mauzo ya 30m+,unanyanyaswa unashindwa kumtelekeza dereva na gari lake wewe ukasepa na 30m? Ukaenda hata nachingwea ndaaani uko ukajifunze kufuga hata bata bukin ili swala lipotee?
 
Kuna jamaa wa USANGU nadhani alikuwa na madhila kama haya
Jamaa aliuza tank na mafuta likaenda kupatikana misitu ya Congo katikati huko 😆
 
Kwani hizo kazi mmelazimishwa kufanya wazee? Mkalimw mache kulalamika kwenye biashara za watu
Huu ni ushauri gani hebu tujaribu kuwa wastaarabu, suluhisho la tatizo SI kuzira nikufanya marekebisho.
Kujua sababu ya tatizo na kulitatua. Sio kukimbia.
Inawezekana mwenye kampuni Hana taarifa hizo. Hapa pia ni sehemu sahihi ya kupaza sauti
 
Yaani mwenye Kampuni asije kinachoendelea kwa miezi mitatu , sita hadi mwaka?
 
Mkuu natumai hizo picha hujawahi tumia kwenye Whatsapp group la kazi au mfanyakazi mwengine na hilo gari kulingundua ni rahisi ku connect dots wewe ni nani, umesema wanajuana na mamwela alafu una deni bado... Ila uoga sio ishu walipue tuu.
 
Hii kampuni jau sana, wafanyakazi wengi ni wakenya.
hapo ndipo penye point,asilimia kubwa wabongo tunafeli sana hasa kwenye sales and markerting...ndio maana kampuni nyingi zilizoendelea zimeajiri wakenya sababu wabongo wengi mda wa kuomna kazi ni tofauti na akishazoea kazi
 
Back
Top Bottom