Kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa uzima na afya, pia natumia fursa hii kukusalimia mpendwa wangu. Mimi naitwa Seif Ahmed Sambila mkazi wa kijiji cha Hanihani wilaya ya Igunga mkoa wa Tabora, kazi yangu kubwa ninayojishughulisha nayo ni kilimo, ni kazi yangu kubwa ambayo inaniingizia kipato na kukidhi mahitaji ya familia yangu, kama vile kulisha familia yangu, watoto kusoma na mambo mengine mengi.
Kitu ambacho sitakuja kusahau ni kwamba, mwaka 2019 nilitoka mkoani kwangu nikaenda mkoa wa Mbeya kwa ajili ya hii hii shughuli ya kilimo, ambapo nilifanikiwa kupata shamba la kukodi, nilikodi hekali mbili nikalima mahindi. Mahindi yalikubali vizuri sana, ilipofikia wakati wa kuanza kuvuna, heka heka za kuvuna kwa kila mtu zilianza mara moja. Nakumbuka ilikuwa siku ya alhamis, siku ya pili kwenda kuvuna shambani kwangu, nilikuwa na rafiki yangu Michael niliyemwomba anisaidie kuvuna mahindi shambani kwangu.
Tuliamka asubuhi na mapema tukajiandaa kuelekea shambani. Ilikuwa yapata saa mbili na robo ya asubuhi wakati tumekaribia shambani. Cha kusangaza niliona kundi kubwa la ng'ombe wakilisha shambani kwangu, sikuwa na cha kufanya kwa haraka zaidi ya kupiga hatua kulisogelea shamba, nilipokaribia nilikutana na yule mwenye hao ng'ombe na alinipokea kwa maneno ya kejeli na dharau akidai sina mamlaka ya kupaza sauti yangu kwake.
"Mimi nina pesa hata ukishitaki ko kote nitahonga pesa tu, na si wewe tu uliyelishiwa shamba, mashamba yote ya jirani nimechungia ng'ombe zangu". Alipokuwa katika kuongea hayo mara nikainua macho yangu kutazama mashamba mengine ya jirani yangu, nilibaki nimepigwa butwaa mara baada ya kuona ni kweli yote yameshaharibiwa vibaya na ng'ombe.
Nilijikaza nikamfuata huyo jamaa nikitamani hata kumtafuna kwa jaziba niliyokuwa nayo, nilipomkaribia alinipiga fimbo moja ya ubavuni ambayo kwa kweli sikuyasikia maumivu yake kutokana na hasira niliyokuwa nayo bali nilijikuta tu niko chini. Hapo ndipo Michael yule rafiki yangu aliponibeba na kunipeleka hospital maana tayari nilikuwa nimeshazimia. Nilikuja kuzinduka baada ya masaa 9 nikiwa hospitalini, hapo ndipo yule rafiki yangu alinieleza yote yaliyotokea baada tu ya mimi kuzimia.
Alianza kwa kusema "Ulipozimia tu yule jamaa kwa uwoga alikimbia akaziacha ng"ombe, nami niliamua kuchukua simu yangu nikapiga picha mashamba yaliyoharibiwa, kisha nikatuma picha kwa polisi mmoja niliekuwa na namba zake za simu na nikamwelekeza eneo nililopo nikamwambia aje na wenzake mara moja, hawakuchelewa maana ndani ya dakika 47 walikuwa tayari wamewasili sehemu ya tukio na hivi ninavyoongea na wewe wamezikamata ng'ombe ziko kituoni ila yule jamaa amekimbia".
Bas kesho yake tulihitajika kituon kutolea ushahidi na kwa bahati nzuri mmiliki wa zile ng'ombe alikuwa ameshakuja kituoni, tulivyofika wahanga wa uharifu huo, kila mmoja alitolea ushahidi kutokana na shamba lake lilivyoharibiwa na polisi walitaka tufike mpaka eneo la tukio, tuliweza kufika na yule mmiliki wa ng'ombe aliona uharibifu na akaridhia kulipa fidia. Siku iliyofuata tulifika tena kituoni na yule mmiliki wa ng'ombe alitoa fidia zote kwa wahanga wa tukio hilo na alitoa fidia mara mbili kwangu kutokana na vile nilivyopigwa na yule mchungaji wa ng'ombe wake.
Basi kesi ilimalizika na yule mmiliki aliruhusiwa kuwachukua ng'ombe wake. Hayo ndiyo yaliyonikuta, lakini tuachane na hayo, zaidi sana nazungumzia kuhusu kilimo na ninajikita sana kuzungumzia changamoto zilizopo katika sekta hii, ambazo mim binafsi nimewahi kukutana nazo, mojawapo ya changamoto hizo ni kukosa mtaji wa kutosha kuendesha kilimo, na hii imekuwa kikwazo kikubwa sana maana imekuwa ikinifanya kupata matunda kidogo ukilinganisha na ukubwa wa shamba lenyewe
Kupanda kwa bei za pembejeo za kilimo kama vile mbolea, mbegu na viuatilifu. Hii pia imekuwa changamoto kubwa sana kwani kila kukicha pembejeo za kilimo zinapanda bei. Hii inawaumiza wakulima wengi hasa wale wenye kipato cha kati, kushindwa kuzimudu gharama za pembejeo hizo. Tunaiomba serikali iangalie suala hili maana karibu asilimia sabini ya wakulima nchini tanzania vipato vyao ni vya kati hivyo imekuwa ni vigumu sana kumudu mabadiliko haya ya kupanda kwa bei za pembejeo za kilimo
Mabadiliko ya tabia nchi, hii pia imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya maeneo nchini kwetu, na haya mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakichochewa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira kama vile kuchoma misitu, kukata miti ovyo na kuharibu vyanzo vya maji. Nawaasa watanzania wenzangu tujitahidi sana kutunza miti na vyanzo vya maji kwa sababu ni rafiki sana na hali ya tabia nchi.
Kukosekana kwa soko bora la mazao, hiki pia kimekuwa kilio cha wengi maana soko la mazao limekuwa linasumbua sana hususani mazao ya biashara, hivyo tunaiomba serikali isikilize kilio chetu watanzania kwa kutoa bei elekezi katika mazao ya biashara ili sisi wakulima wa kipato cha kati tusipate shida katika kuuza mazao yetu.
Kama tunavyojua sekta ya kilimo ni moja ya sekta kubwa na ambayo inaingiza pato kubwa la nchi. Hivyo serikali ikielekezea nguvu yake katika sekta hii naamini itawainua watanzania wengi sana na kufanya mapato ya ndani kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
Na mwisho nimalize kwa kusema naipongeza serikali yetu kupitia Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kwa juhudi inayotumia kila kukicha kutatua kero na changamoto za wananchi wake, hivyo hata katika hili serikali haitanyamaza.

Upvote
1