JIna langu naitwa Elly kijana wa miaka 31 sasa nina elimu ya Diploma ya masoko, chuo nilimaliza mwaka 2013 ila wakati nikiwa katika masomo nimekuwa katika ajira zilizoweza kuniwezesha kujikimu kimaisha kwa udogo wake na pia kunisaidia kulipa ada.
Baada ya kumaliza nikiwa ndani ya ajira nilitamani kupata mafanikio zaid kimaisha ili niwe mtu wa kuweza kujisimamia kiuchumi na kufanya mambo makubwa zaidi, mwaka 2014 kampuni binafsi niliyokuwa nikifanyia kazi iliyumba kiuchumi tukapunguzwa kazini, nikawa sina ajira kwa miaka 2.
Mwaka 2017 nikapata kazi ya muda mfupi ilipoisha nikangoja tena mpka mwisho wa mwaka nikapata nyingine nikafanya kwa bidii sana nikajifunza kuweka akiba kwa kuwa niliamua nipate mtaji niingie kwenye kilimo kwa kuwa watu wengi walikuwa wanasema kinalipa.
Nikajikusanya kamtaji kangu kadogo 1.5mil nikaenda mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero kijiji kinaitwa Turiani kata ya Mzambarauni baada ya kuelekezwa na marafiki wenyeji nilienda na rafiki yangu tuliyetoka nae mjini lengo ni kulima na kupata pesa nyingi ya haraka, tukakodi shamba heka 3 kwa gharama ya laki 1 kwa heka kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, kutokana na ugeni wa kazi hiyo shamba tulidanganywa ni heka 3.
Hivyo gharama tulizokuwa tukilipa ni kwa kipimo cha heka 3 kwa kuwa kuna kazi za kusafisha shamba, kulima na trecta mwenyeji wetu ndiye aliyekuwa akituongoza hjvyo tulitoa pesa ili kazi iende kwa haraka, lengo letu ilikuwa kulima zao aina ya Beet root tulilifanyia utafiti wa juu juu kuhusu bei zake sokoni zinavyouzwa bila kufatilia taratibu zake za kulima na jinsi ya kuliuza.
Hivyo tulikurupuka kwa kuwa katika masoko makubwa mfano Kisutu (DSM) kilo 1 kwa wakati huo iliuzwa mpaka 16,000 tukawaza kwa haraka tukilima tukivuna hata tukiuza 10,000 kwa kilo shambani itatulipa, tukaanza kazi haraka tukanunua mbegu tukazisia kwenye vitalu pamoja na mbegu ya hoho na mboga mboga za majani ili zitusogeze katikat ya kazi, mda huo tulipata nyumba mbovuu sana ya kupanga ya tope na miti haina choo na ilikuwa inavuja sana wakati wa mvua hivyo usiku mvua ilipokuw ikinyesha tulipata tabu sana mwanzoni.
Baadaye tukahamia chumba kingine tuwe karibu na shamba hatukutaka kuishi kimjini ili kupunguza gharama maana mtaji ni mdogo. Mbegu zilipofikia muda wa kuhamishia shamba tulichimba shimo kubwa katikat ya shamba kwa lengo la kufanya liwe kisima ili tuwe tunachota maji kumwagilia mimea shimo baada ya shimo kwa kutumia ndoo tukafanikiwa kuyafikia maji, kazi ikawa nzuri mwanzoni maana tulipata mvua chache zikatusaidia baadae kiangazi kikaanza kututesa kazi tukaiona ngumu kwa kumwagilia kutumia ndoo tukawa tunapumzika jioni tumechoka sana kumbuka kazi zote shamba lote tunafanya kazi watu wawili tuu, tukashauriana tutafute mashine (honda) kwa ajili ya kumwagilia pesa za kuinunulia tukaomba kwa ndugu yetu atudhamini maana tulijua tutapiga pesa kwenye mavuno (🤣).
Tukanunua tukaifunga karibu na mto mdogo tukawa tunamwagilia, tumeenda vizuri beetroots zikazaa vizuri zikawa kuubwa sana zikakomaa tukaanza kutafuta soko, nikabeba baadhi nikaenda soko la mawenzi morogoro nikakosa wa kumwuzia, nikaenda dar kariakoo na kisutu nikaishia kupewa ahadi kwamba watanunua wakachukua na mawasiliano lakini hawakuwah kupiga kuhitaji zao nikawa nawapigia tunapewa ahadi tuu nikashauriana na mwenzangu niende Dodoma kwamba iwe ndo njia iliyobaki nikaenda dodoma nikafikia kwa ndugu yangu mmoja.
Asubuhi nikachukua matunda yale nikaenda nayo masokoni kutafuta mnunuzi wa jumla nako sikupata maana waliyonayo wnasema hawanunui mzigo mkubwa sana kwa kuwa utokaji wake ni wa taratibu sana ni tofauti na mazao mengine kwa sababu sio kitu cha lazima sana kutumia nikapata wazo kujaribu soko la Saba saba Dodoma nikazunguka nikakutana na bwana mmoja anaitwa Mogela ana meza anauza limao na tangawizi akanambia mimi siwez kuyanunua bali ntakupa meza upande uuze mwenyewe yakiwa yanatoka labda utanishawishi.
Nikashauriana na mwenzangu tukabuni jina la biashara tukaliita (Tukutane sokoni) tukaweka bidhaa tunayouza na mawasiliano tukatengeneza vipeperushi vya rangi vya kuvutia na mawasiliano yetu ili anayepita nimpatie asome au aone kwa picha faida ya kutumia beetroot.
Nikapanga bidhaa zangu bahati nzuri mteja mmoja mmoja sana wenye uelewa wa ile bidhaa wakawa wananunua kwa siku elfu 20 -30 nikawa nauza siku nyingine elfu 5 siku nyingine siuzi hata tunza moja pesa nayopata nafanyia gharama za kawaida za binadamu ukiwa ugenini na baadhi namtumia mwenzangu nliyemwacha shamba ili aendelee kujikidhi na kunitumia mzigo kidogo kidogo, nikafanikiwa kuuza kama 150,000.
Changamoto zilikuwa nyingi sana badae mwenzangu akanipigia kwamba amechoka kukaa shamba anataka kurudi mjini hivyo nifanye nirudi nibaki shamba yeye aondoke hataki kuteseka zaidi ikabidi nifanye makubaliano na mtu wa sokoni kwamba nitakuwa namtumia mzigo anauza ananitumia hela.
Nikarudi shamba Turiani nikampa mwenzangu nauli akaondoka asubuh mimi nikabaki peke angu mwanzoni dalali yule mizigo miwili ya kilo 25 kila mmoja tulienda vizuri akawa ananitumia tu hrla ndogo ndogo za kutumia, nikaanza kukata tamaa huku mwenye shamba akawa anataka shamba lake kwa kuwa muda wa kukodi umeisha, pesa sina, zao haliuziki kabisa kama nlivyowaza nikawa na mawazo sana na wakunisaidia hakuna maana kila mtu anasema kilimo kinalipa lakin sio lelemama.
Nikauvuna mzigo wote nikauweka ndani ninapoishi kwa kuwa sina chumba kingine na wazoefu wa beetroot wanasema inahifadhika kwa muda kidogo nikahifadhi huku nkitafuta soko lakini wapi nikahangaika sana matunda yakaanza kuoza baada ya mwezi hivi ikabidi niyatoe nikayafukie kwenye shimo nikakabidhi shamba nikaondoka kwenda kwa ndugu yangu mmoja Morogoro, sikuweza kurudi Dar kwa kuwa sina kitu sina kazi ntaenda kuishi vipi?
Nikakaa kwa ndugu yangu kama miezi 2 nikitafuta hela na kujiuliza maswali mengi kwamba mbona kama nafeli maisha, watu wanasema kilimo kinalipa mbona ni kigumu sana mbona sijafanikiwa mbona mateso ni mengi sana.
Nikaamua kutokata tamaa nikajisemea mimi ntalima na ntafanikiwa bahati nzuri ndugu yangu akaniunganisha mahali kwenye kazi nikatafuta mtaji lengo ni lile lile kwamba ntarudi shamba na nataka nifanikiwe maana ajira bado haitanifikisha mahali napotaka nikafanya ile kazi miezi 5 nikapata kamtaji kangu kadogo nikahamia eneo linaitwa Ruaha mbuyuni kunaposifika kilimo cha vitunguu na nyanya nikasema ntapambana mpaka nitoboe.
Mwaka 2020 mwezi wa 6 ndo mwaka niliongia rasmi Ruaha mbuyuni nikapata mwenyeji nikapenda kujifunza kilimo cha nyanya, nikajiwazia moyoni nisiende kwa pupa niende taratibu kwa kujifunza, nikajichanganya na wenyeji wakulima wakubwa wa nyanya wakawa wananipa mbinu na njia sahihi za kulima nyanya.
Nikaanza kwa kulima mbegu za kawaida sana zisizo za kisasa nikaanza na robo heka kwa kuwa nilitaka kujifunza changamoto zake kwa uhalisia zaidi nikishuhudia kwa mikono yangu mwenyewe na macho kwamba hatua zipi sahihi zinapaswa kuzingatiwa ili kuweza kulifikisha zao kwamba hili lipo tayari kwa kuuzwa na likamvutia mteja, nikaandaa shamba, nikasia mbegu mwezi wa 10 ilikuwa tarehe 16 kwa malengo ya kuja kuvuna nyanya mwezi wa 2.
Mwaka 2021 na nikawa nimeamua kazi zangu nakuwa nafanya mwenyewe kwa kuwa sina mtaji wa kuweka vibarua, nikajinyima sana nikajpambna hatimae mwezi wa 2 ulipofika nikaanza kuuza nyanya kwa bei ya chini kwa kuwa aina ya mbegu nliyolima haikuwa ya kisasa ukilinganisha na wengine waliolima za kisasa ila nilifurahi sana kwa mara ya kwanza kwenye zao ambalo sina uzoefu nalo kuuzia shambani na bila usumbufu nikamshukuru Muungu kwa kuwa najua huko mbeleni nitakuza mtaji na nitanikiwa kulima kwa kisasa zaidi kama wengine.
Nikaitunza nyanya nikaenda nayo kwa kipindi kifupi kulingana na mbegu ilivyokuwa haina maisha marefu, pesa niliyopata mwezi huo huo wa pili nikaamua kuizungusha isikae nikaamua kulima pilipili hoho niliandaa robo heka nikanunua gramu 200 ya mbegu nikaiweka kwenye vitalu mwezi wa 3 nikaipanda mwezi wa 4 tarehe 14 nikaanza kuivuna mwezi wa 6 mwaka huo 2021 nikaenda nayo mpaka mwezi wa 8 mwishoni nikapumzika mwezi mmoja kwa ajili ya kulima tena nyanya nikaweka mbegu mwezi wa 10 nikapanda mwezi wa 11 na niliongeza eneo kutoka robo mpaka nusu heka kwa kuwa nyanya inataka mtaji wa kutosha hivyo kama nlivyosema niliamua kukuza mtaji kidogo kidogo lengo ni siku moja niweze kulima heka 1.5 au 2.
Namshukuru Mungu nilifanikiwa kuanza kuvuna nyanya mwezi wa 2 mwishoni mwa mwaka 2022 nikaihudumia nikasogea nayo mpaka mwezi wa 4 ilipoisha kutokana na changamoto za ukungu mkali ukizingatia mtaji bado wa kuunga unga nikapumzika kidg mpka mwezi wa 7 nikaandaa mbegu na hivi sasa ni mwezi wa 8 nimeshapanda nyanya ndo kwanza zina wiki 3 malengo ni kuvuna mwezi wa 10 mwishoni.
Nimejifunza maisha ya utafutaji sio mepesi kama tunavyoaminishana na kilimo sio chepesi na cha matokeo ya haraka kiivyo, cha muhimu usikate tamaa na usikatishwe tamaa na usiogope kupata hasara au kupoteza mtaji wako wote ili kuyafikia mafanikio yako, changamoto ni nyingi sana ila ukipambana utaweza kuzishinda.

Upvote
2