son_african_star
Member
- May 30, 2023
- 9
- 15
Kuleta changamoto zinazoyakumba maisha ya wengine ni kwamba wengi wetu tunakosa ujasiri wa kuthubutu na kufanya mambo mbalimbali yaletayo katika maisha yetu.
Changamoto hii imekuwa ni kubwa sana kwa kizazi hiki.
Wengi hupata mawazo mazuri ila wengi huishia kwenye hatua ya awali yaani ya kuwaza tu, wengine hawawezi kubadili kile wakiwa kwenye matendo kwa sababu ya kukosa ujasiri wa kujiamini.
Wengi hutawaliwa na mawazo hasi, wengi hudhani haiwezekani, ila ukweli ambao upo bayana ni kwamba ukiweza kujijengea uwezo wa kujiamini kwenye kila jambo, basi mafanikio makubwa yatakuwa upande wako.
Na ili uweze kujijengea uwezo huo kujiamini unatakiwa kuwa na vitu viwili muhimu katika maarifa sahihi ya kile unachokifanya au unachotaka kufanya au kuwa na umuhimu katika jambo husika. Ukiweza kuyafanikisha mambo hayo utaondokana na tatizo la kutokujiamini.
changamoto kubwa zinazoikabili dunia hii ni pamoja na kutokuwepo na watu wenye uwezo wa kutatua changamoto au matatizo fulani.
Wengine wa watu waishio katika dunia hii kila jambo ambalo lipo katika sura ya changamoto basi wao huiachia serikali kusubiri tatizo fulani litatuliwe na serikali.
Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba endapo unataka mafanikio ya aina fulani na unazongwa na changamoto fulani basi usisubiri serikali yako ndiyo itatue tatizo hilo.
Bali unatakiwa kuwa mmoja wa watu wenye uwezo wa kutafuta majibu ya kila changamoto ambayo unayokukabiri, ukiendelea kusubiri kila tatizo ulilonalo litatuliwe na serikali yako ni kwamba utazidi kuchelewa unakotaka kwenda. Serikari ni wewe mwenyewe.
Changamoto kubwa ambayo inakumba maisha ya watu wengi ni pamoja na uvivu wa akili. Watu wenye maisha ya kawaida kila jambo husema siwezi kumudu, kwa mfano mtu akiambiwa asilimia kumi ya kila pato lake, jibu jepesi la mtu huyu atakwambia siwezi kumudu.
Siwezi kumudu, ni jibu jepesi ambalo msingi wake mkuu hutoka na uvivu wa akili wa mtu huyo. Kwa nukta hiyo unatakiwa kuelewa ili uweze kufanikiwa kwenye masuala ya fedha na mambo mengineyo maishani unatakiwa kuepukana na tatizo hili la uvivu wa akili na uanze mara moja kuanza kuanza chanya kila wakati.
Kwa mfano akili za matajiri mara nyingi huwaza namna ya kutimiza jambo fulani, wengine wao hujawa na maswali kwamba nitawezaje? Na huepukana na tatizo la uvivu wa akili, kwamba siwezi kumudu.
Hata wewe unaweza kufanikiwa katika mambo mbalimbali endapo utawaza chanya namna sahihi ya kufanikiwa katika jambo fulani kama wafanyavyo matajiri.
Waza chanya kila wakati ili utimize malengo yako.
Tunaaminishwa ya kwamba mnyama mwenye ngozi ngumu kuliko wote huenda ikawa ni mamba, japo hakuna uthibitisho kamili juu ya hilo. Uwezo wa mnyama mwenye ngozi ngumu ni mnyama mwenye uwezo wa kuvumilia mengi ikiwemo uwepo wa jua kali wakati wa kingazi.
Kama ilivyo kwa mnyama mamba basi hata sisi tunaambiwa ili tuwe na ngozi ngumu katika kufanya mambo mbalimbali, ikiwa na maana ya kwamba tunapaswa kuvulimia kila changamoto ambazo zitakuwa zinajitokeza kwenye kukamilisha mambo mbalimbali.
Ni muhimu kuwa na ngozi ngumu kwa sababu wengi wetu tumekuwa ni watu wa kukata tamaa sana, hasa pale zinapojitokeza changamoto mbalimbali kwenye mambo tuyafanyayo.
Ila ukweli ambao napaswa kukumbusha siku ya leo ni kwamba pamoja na changamoto zote zinazojitokeza kwenye mambo mbalimbali tunakumbushwa ya kwamba tunapaswa kuwa wavumilivu kwani mvumilivu ndiye ambaye atakula mbivu, au kwa maneno mengine anayevulia ndiye atakayefanikiwa zaidi.
Hakuna mazingira, kizuizi au yoyote ambayo ina uwezo kabisa wa kukuzuia ushindwe kufanikiwa. Kila changamoto au mazingira yanayokuzuia wewe kufanikiwa una uwezo wa kuyashinda na hilo linawezekana kwako.
Kama imetokea kwako umeshindwa kupata mafanikio yako kwa sababu ya changamoto, habari mbaya kwako nikwambie ni kwa sababu uliamua kufanya hivyo, yaani uliamua ushindwe tu na sio changamoto ndio zilizokuzuia moja kwa moja.
Kwa nini nakwambia hivyo? sababu, hakuna changamoto ambayo ina uwezo wa kuhimili nguvu ya kujitoa kwako na nguvu ya mwelekeo. Ikiwa utaweka nguvu ya kujitoa na mwelekeo na ukajipa muda, utazishinda changamoto na kufanikiwa.
Tatizo kubwa la watu wengi wanapokutana na changamoto, wanakuwa ni watu ambao, wanazikuza sana hasa kwa kuzifikiria, badala ya kutumia nguvu hizo kujitoa na wakati kila linawezekana kuzishinda changamoto zao.
Kitu cha kuzingatia, kila changamoto una uwezo wa kuishinda. Hata unashinda changamoto zako, hata kama itachukua muda mrefu tofauti na ule uliojiwekea, jukumu lako ni changamoto zako kwa namna yoyote ile.
Changamoto kubwa ambalo wengi wao wameikumbatia kwa muda mrefu na bado wanaendelea kuibeba ni pamoja na kuendelea kutafuta zaidi badala ya kuangalia faida.
Kwa mfano, wengi wao husema leo nimeuza mauzoya elfu hamsini na kusahau kuangalia faida itokanayo na mauzo hayo ya shilingi hamsini. Wengi huweka mauzo na faida kama ni kitu kimoja ambacho siyo sahihi hata kidogo.
Kitendo hiki cha kuangalia mauzo kama faida kimewafanya watu wengi biashara zao zife kwa sababu wamekuwa hawaelewi kama wanakula mtaji bila wao kujua kwa sababu wao huangalia mauzo badala ya kuangalia faida.
Ikiwa na wewe ni miongoni mwa watu wenye tabia hii ya kuuza badala ya faida kuanzia leo kuu mtazamo wako utakaokusaidia kutofautisha kati ya mauzo na faida.
Kwenye kila mauzo yako unapaswa kujua faida ni ipi, ili ujue namna sahihi ya kutumia faida hiyo kwa maendeleo yako binafsi na biashara kiujumla. Ukifanikiwa katika hili utaona biashara yako inakua na utazidi kusonga mbele kila uchwao.

Upvote
2