Changamoto ya Haki za Binadamu Zanzibar, somo latolewa kwa AZAKI jinsi ya kupambana

Changamoto ya Haki za Binadamu Zanzibar, somo latolewa kwa AZAKI jinsi ya kupambana

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Taasisi ya Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania (THRDC) imetoa mafunzo kisiwani Zanzibar kwa kujengea uwezo AZAKI visiwani humo juu ya namna ya ufuatiliaji, uandishi wa ripoti za haki za binadamu na utunzaji wa kumbukumbu.

“Mafunzo haya yanakwenda kuwajengea uwezo namna ya kufuatilia namna ya kuhifadhi, kusambaza taarifa za haki za binadamu sababu nyinyi ni jeshi kubwa linalofuatilia na kulinda haki za binadamu kwa niaba ya serikali,” anasema Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Taifa wa THRDC na kuongeza:

“Tunafahamu Zanzibar kuna changamoto za haki ya binadamu, hasa zile za udhalilishaji, madawa ya kulevya, haki za watoto, hivyo mafunzo haya yatawasaidia jinsi ya kusambaza kwa niaba ya Serikali.

“Mwenye jukumu la kulinda na kutetea haki za binaadamu ni Serikali lakini ninyi mtakuwa sehemu ya kusaidia Serikali.”



CHANZO: THRDC

-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

MAANA YA AZAKI
Asasi za Kiraia (AZAKI) zinatafsiriwa kuwa ni muunganiko wa asasi za mashirika na taasisi ambazo zinafanya kazi zake kwa kushirikiana na kaya, sekta binafsi na Serikali katika kushughulikia masuala ya umma.

AZAKI zinajumuisha taasisi nyingi zinazofanya kazi kimataifa, kikanda, kitaifa na katika ngazi za Serikali za Mitaa. AZAKI inajumuisha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs), Vikundi vya

Kijamii, Taasisi za Elimu, Sehemu ya Wanahabari, Jumuiya za Kitaaluma, na Jumuiya za Kidini.

Nchini Tanzania, hakuna Sera wala Sheria yoyote ambayo inafafanua maana na mawanda ya utendaji kazi wa AZAKI na badala yake, zipo sheria tofauti tofauti ambazo kwa ujumla wake zinatambua, kusimamia, kuratibu na kufafanua utendaji kazi wa AZAKI.
 
Back
Top Bottom