Changamoto ya kiafya iliimarisha ubinafsi hata katika maamuzi mazuri ya kisiasa na kiuchumi

Changamoto ya kiafya iliimarisha ubinafsi hata katika maamuzi mazuri ya kisiasa na kiuchumi

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Changamoto ya afya ya moyo ya Mkuu wa tano wa utawala wa nchi yetu ilijulikana kwa kuchelewa sana (baada ya kifo chake) kuwa alikuwa na matatizo ya kiafya.

Changamoto ya afya ya moyo ambayo ndiyo iliyomlazimu (hili nina uhakika kabisa ukirejea utaalamu wa kiafya) asiweze kusafiri mbali kwa usafiri wa ndege aliitumia kwa ubinafsi wa hali ya juu.

Yeye aliamua watu wake wasisafiri na kuifanya kama Sera (Sera Tamko) kumbe tu ilikuwa ni ubinafasi tu na kuona wivu watu wengine kusafiri. Aliamua wasaidizi wake wachache wasafiri huku safari zingine nyingi akizifumbia macho. Alijaribu kutufumba mambo kwa kuzifanya safari za nje ya nchi zionakane mbaya na zisizo na maufaa kumbe yote hiyo kwa sababu yeye asingeweza kusafiri kwenda mbali.

Ukweli ukiwa na kiongozi mbinafsi wa kiwango kile basi ujue watu wataumia sana na siasa hizo na hata uchumi wa nchi ni lazima tu uporomoke. Huwezi kujustify ukuaji wa uchumi kama nchi yako imejiwekwa kisiwani yenyewe.

Angalia nchi kama USA na China ambazo raia wake (serikalini na binafsi) wanasafiri sana duniani ndiyo nchi ambazo zinakimbiza uchumi wa dunia kwa sasa. Wakati mwingine ukweli kabisa inabidi mtu anayegombea uongozi wa juu kwa nafasi ya Rais aangaliwe afya yake kabla. Tusioneane aibu! Kiongozi mbinafsi hatufai!
 
Ni moyo huohuo uliotupeleka uchumi wa kati. Safari safari kwa nchi ambazo zinakopa pesa za covid kwa ajili ya madawati ni mzigo kwa wananchi. Wizi wenu umeanza.
 
Ni moyo huohuo uliotupeleka uchumi wa kati. Safari safari kwa nchi ambazo zinakopa pesa za covid kwa ajili ya madawati ni mzigo kwa wananchi. Wizi wenu umeanza.
Kiwango cha kukua kwa uchimi Enzi za JK na kiwango cha kukua kwa uchumi kwa Enzi za Jiwe ndiyo kipo wazi kuwa Jiwe alikuwa ni mwizi Zaidi!
 
Mtu unaumwa then unatumia kuumwa kwako kuwa ubinafsi
 
Ili mradi hawezi kuongea tena mzee wa watu atasingiziwa kila lilibaya na kila lililozuri litapelekwa kwa walio hai
Chungeni nyumba yenu mnayojenga
Kwani hujaona clip anakiri na kujisifia kusafiri nje ya nchi mara tatu tu? Tena nchi zenyewe za hapa karibu karibu tu. Why hakuwahi kwenda mbali!
 
Jamaa alikuwa mbinafsi na mchoyo, hakutaka kabisa watu waone ama wasome chapisho lake la kitaaluma, yaani "thesis", aliloliandika kuhusu asidi iliyopo ndani zao la korosho katika shahada yake ya uzamivu.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Je kwa sasa hilo andiko lake linaweza kupatikana?
 
Back
Top Bottom