Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ni mzee wa 2005/2006 mpaka 2008/2009 bila shaka hahaaUmejilipuwa mzee hadi kitambulisho umeweka. Alafu kumbe vitambulisho vilibadilika tena. Vitambulisho vilikuwa vina chip kama laini ya simu baada ya mgomo mwaka fulani chuo kilifungwa wanafunzi waliporudi walipewa vitambulisho vipya, Leo tena naona wamebadilisha. Haya bwana maafisa utumishi wenzio wanakusubiri huku halmashauri.
Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
DISCO inakuhusu nyauweeeNaitwa Abdul-Aziz Ally Carter mwanafunzi wa mwaka wa 3 chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), nasomea historia na sayansi ya siasa,
Namba yangu ya usajili 2021-04-01016.
UDSM tunafundishwa kwa namna 2, lectures za Darasani na seminar presentation,
Kwenye seminar presentation ndiyo sehemu pekee ya ufundishaji ambayo wanafunzi tunaruhusiwa kutoa mawazo, kuuliza maswali na kutetea hoja zetu.
Kuna baadhi ya seminar leaders kutoka department ya utawala wa umma na sayansi ya siasa na department ya historia hawatutendei haki katika seminar presentation,
Tunapouliza maswali,kujenga na kutetea hoja zetu tunapokea majibu ya udhalilishaji na kukatisha tamaa mfano muongo, huna hoja nk pasina kuuliza chanzo cha taarifa tulichotumia au kuturekebisha kwa njia ya kistaarabu,
Na hivyo kutufanya baadhi ya wanafunzi kushindwa kuuliza maswali, Kuhoji au kutetea hoja kwa hofu ya kukosolewa na seminar leaders ,
Hili tatizo limekuwa sugu na hatuoni dalili za hao seminar leaders kubadilika hasa katika hizo department 2 nilizozitaja hapo juu,
Tunashindwa kutoa taarifa kwa mamlaka kwa kuwa kama seminar leader hatochukuliwa hatua tatizo linabaki kwa mwanafunzi maana seminar presentation zina alama 15 na seminar leader ndiyo mwenye maamuzi ya kukupa ngapi kati ya hizo,
Baadhi ya wanafunzi tunajifunza vyema kupitia mijadala, kuuliza maswali ,Kuhoji na kudadisi mambo lakini baadhi ya seminar leaders kutoka kwenye hizo department wanatunyima haki yetu ya kujifunza kwa kauli zao za kukatisha tamaa.
Naomba tusaidie kusambaza ujumbe wetu ,ufike wizara ya elimu ili kero hii itatuliwe.
Ahsante
Aende akamuone kama ajalamba discontinueKabla ya kuja kulalamika huku ulishamuona mkuu wa idara ya PSPA au just course instructor na kuwasilisha malalamiko yako? Ndio usomi gani huu wa kutofuata taratibu? Unadhani wizara ya elimu ina mamlaka juu ya academic autonomy ya chuo?