Changamoto ya kupata ajira kwa wataalam wa afya na suluhisho

jembe_jembe

Senior Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
185
Reaction score
66
Habari wanajamvi

Tangu miaka michache iliyopita kulitokea changamoto ya upatikanaji wa ajira kwa wataalamu wa afya, na sasa tumefika mashala ambapo mtu anapomaliza internship, anarudi nyumbani na kukaa muda mrefu, hata miaka bila kuitwa hata kwenye usaili wa kazi nyingi ambazo ameshaomba.

Hiyo inapelekea kukata tamaa, majuto na msongo wa mawazo.

Kwa upande mwingine, nchi zilizoendelea kama Uingereza 🇬🇧 Marekani 🇺🇸 Canada na Australia 🇦🇺 zikiwa na uhaba na uhitaji mkubwa mno wa nguvu kazi ya taaluma hizo.

Nini basi tunaweza tukafanya kujikwamua na hii changamoto?

Tumeandaa fomu hii Je, umeridhika na kazi yako? kuangalia ukubwa wa tatizo ili tujaribu kulitatua pamoja, ukiacha anwani yako ya barua pepe, utapata mwongozo wa moja kwa moja wa fursa za kazi za kimataifa.

N.B: Walengwa ni wataalamu wa afya kama madaktari (MD and above), manesi (Diploma in nursing holders and above), wafamasia
(B.Sc Pharm), Physiotherapists, Occupational therapists

Wasalaam
Dr Kay
MD, GPST
Kent, UK 🇬🇧
 
Changamoto ya ajira "especially",kwenye sekta ya afya inachangiwa na mambo makuu yafuatayo:-
1.Uchumi wa nchi kua duni.
Inajulikana sekta ya afya haizalishi chochote,yenyewe ndio inatumia rasimali,ili uajiri watu wa kutosha na kuwalipa kadri ya maslahi yao,hapa utahitaji uchumi wa nchi madhubuti kutoka kwenye vyanzo vingine kama madini,viwanda,kilimo,uvuvi etc.....uwe na uwezo wa kuuza nje zaidi kuliko unavonunua.
Sasa kama madini mwekezaji anaondoka na 86%,viwanda mchina anazalisha hadi yeboyebo,kilimo cha jembe la mkono,mapato ya serikali kulipa wafanyakazi wake vizuri wanayatoa wapi?

2.Mazingira duni ya sehemu za kazi bila usawa.
Mtu amesoma chuo miaka 5+,unamuajiri kijijini ajitafutie nyumba ya kupanga,humlipi pesa ya masaa ya ziada,humlipi hata posho ya usafiri.....huku mtu huyo akiwa ndio tegemeo la kutoa huduma kwenye halmashauri.
Wakati huo huo halmashauri kila mkuu wa idara inamlipia zaidi ya laki tisa kwa mwezi kutoa OC,na makusanyo ya ndani,..........posho ya madiwani haikosekani kwa ajiri ya kumlalamikia mtumishi wa afya anaefanya kazi kadri ya uwezo wake kwenyev vikao vya madiwani.......unategemea huyu mtu akipata sehemu nyingine yenye maslahi atakaa?,unakuta mwisho wa siku watu wanaajiriwa baada ya miaka miwili wanaondoka,tatizo la ajira linarudi pale pale.

3.Kutokua na mipango inayoshabihiana ndani ya serikali.
Wizara ya afya na Tamisemi wote ni waajiri wakubwa wa sekta ya afya,ila mipango yao ni tofauti.....unakuta wizara ya afya imefuta kozi ya AMO,ila kwejye utumishi wa TAMISEMI, hospitali za wilaua AMO ndio wanahitajika zaidi kuanzia 12,.......unajikuta kuna gepu kubwa la hao wataalamu,....hii huenda sambamba na kada zingine.
Kila halmashauri ina populations inayotofautiana,.....lakini utakuta halmashauri ya Chato ina watumishi wengi kuliko ya Simiyu kwa kua tu labda raise anatokea kule ......hapo huwezi tatua tatizo la ajira,...wale wachache watachoka wanaweza kuacha kazi ama kuhama kabisa na kusababisha upungufu.

4.Idadi ya watu kuongezeka kwa kazi huku kipato kikiwa duni.
Kila mzazi anampeleka mwanae kusoma afya kwa kuuza mashamba na mazao,mwisho wa siku kila mtu anakua na taaluma huku sehemu za ajira zikiwa chache ,na hata waliojiajiri private hamna wateja,watu masikini wengi wanaumwa ila hawana hela,wanahitaji matibabu ya bure.

5.kutokua na mipango na Dira ya nchi kwenye kila kitu.
Hili ni tatizo,kila rais anayekuja yeye ni alpha na omega,anachowaza yeye ndio sahihi kwa wakati huo
 
Hii ni changamoto kwakweli lakini, kuna fursa za kazi nje ya nchi, mnazifuatilia?
Mtapenda kuzichangamkia? Kuna utayari wa kubadili mazingira ya kuishi na kufanya kazi?
 
Back
Top Bottom