Changamoto ya kupata mke

Mkuu 34 au 35 ndio mtu aoe, je umesahau shughuli ya kupata mtoto inaweza chukua hata miaka mi tatu au mitano?
acheni kukatishana tamaa. shughuli ya kupata mtoto inaweza kuchukua miezi tisa au miaka mitatu hadi mitano hadi ishirini au asipatikane milele hata kama utaoa na miaka 19. Mbona waliooa mapema wanaendelea kuzaa watoto wao tatu au wanne wakiwa na miaka hata 40? cha msingi uoe mwanamke ambaye ana nguvu. siyo unataka watoto watatu unaoa mwanamke yuko late 30s. kwa interval ya miaka miwili miwili atafika menopause hajamaliza kuzaa ingawa kuna tofauti kati ya mwanamke na mwanamke kimaumbile. Pia ni vizuri kuwa open minded ukubali kuwa ndoa si kwa ajili ya watoto tu bali ni kwa companion zaidi.
 
Titizo ni pasepshen za wadada zetu ndo Zinatufanya tupate changamoto ya kuoa. Wanataka uwe na gari, nyumba af muwe mnaishi maisha flan ya kwenye TV
wala. mbona kuna watu wanaume wana nyumba, hela, magari na sura nzuri lakini hawajapata wake? kila mtu ana mtihani wa aina yake bila kujali hali yake. mbona kuna wanaume hawana kitu na wameoa wake wema tu?
 
tulia hivyo hivyo dawa iingie maana ukipata mke kirahisi utakosa unyenyekevu. Ukimpata kirahisi utasema umempata kwa sababu una ajira serikalini, biashara, maisha yako yako poa, pesa siyo mtihani n.k. Uteseke kumpata ili siku ukimpata umhimidi Mungu na useme "si kwa majeshi, wala silaha.........." ni kwa neema tu, na uitunze hiyo ndoa ukikumbuka hiyo neema. sawa sawa?
 

Serikali tena mkuu teeh teh
 
Dah hiyo ni changamoto sana siku izi, usishangae hauko peke yako...yeyote aliye makini na anataka mwanamke makini maishani atakiri ni changamoto japo inawezekana kabisa, endelea ivo ivo kutafuta usikate tamaa japo uvumilivu ni muhimu sana

Ata kwangu ni changamoto lakini nimekubali matokeo
 
Vigezo vingi sana mkuu
 
Mwalimu napita tu...........
 
Pole ila wakati utafika.....utampata mtu sahihi.
 
Asante, Jibu Zuri sana
 
Ndo hivyo Mkuu lakini watu wenye navyo wapo. Wewe umekosa kipi hapo? Au we ni Me?
Ushauri, usikate tamaa... Na usithubutu kuzaa ndugu, yaani ukimpa mimba mtu tu na mwana atatokea then utajuta! Mungu anapima uvumilivu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…