KERO Changamoto ya Scanner za nCard katika Vivuko vya Azam Marine – Kivukoni Ferry

KERO Changamoto ya Scanner za nCard katika Vivuko vya Azam Marine – Kivukoni Ferry

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Azniv Protingas

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2020
Posts
352
Reaction score
585
Habari wana JamiiForums,

Ningependa kuibua changamoto niliyokutana nayo katika matumizi ya nCard kwenye vivuko vya Azam Marine, eneo la Kivukoni Ferry, Dar es Salaam.

Nilikuwa nimeweka salio la TSh 1,000 kwenye nCard yangu. Nilipofika kwenye scanner, nilimskania ndugu yangu na akaweza kuvuka. Hata hivyo, nilipojaribu kujiskania mwenyewe, scanner haikufunguka.

Mlinzi alipokuja, nilimweleza kuwa nilikuwa nimeweka salio muda mfupi tu uliopita na nikamwonyesha risiti ya muamala huo. Akanielekeza nikaangalie salio, nilipoenda kuangalia salio langu, nilikuta hakuna pesa iliyobaki.

Na nakumbuka mara ya mwisho niliweka 1500 nikapita mimi kuna mtu aliniomba nimpitishe kwa card yangu, kwa hiyo ilitakiwa ikatwe 1000 lakini cha ajabu 500 ambayo ilikuwa imebaki haikuwepo kwenye card.

Hali hii imenifanya nijiulize maswali kadhaa:

1. Kwa nini kusiwe na ujumbe wa maandishi pindi abiria anaposcan?

2. Je, mfumo wa nCard una utaratibu wa kurejesha au kuhakiki pesa pale ambapo malipo yamefanyika lakini huduma haijapatikana?

3. Abiria anapaswa kufuata utaratibu gani ili pesa yake iweze kufuatiliwa na kurejeshwa endapo kutakuwa na hitilafu kama hii?

Ninaomba wahusika wa nCard na Azam Marine walifuatilie suala hili na kutoa ufafanuzi. Ni muhimu kuhakikisha kuwa mfumo wa malipo na scanner vinafanya kazi kwa ufanisi ili kuepusha usumbufu kwa abiria. Sijajua upande wa kivuko cha serikali hali ipoje.

Nimeleta suala hili hapa ili kupata uzoefu wa wengine ambao huenda wamewahi kukutana na changamoto kama hii, pamoja na majibu kutoka kwa wahusika.
 
Vya kwetu walala hoi ukiscan inaonesha maandishi ya 'wellcome' na ikiwa salio halitoshi inaonesha isufience balansi kaka, na pia kama salio umeweka kwa wale watu ambao wamekaa nje wanakata 100 kwenye kila jero
 
Back
Top Bottom