KERO Changamoto ya ucheleweshaji wa maombi ya hati kwenye mfumo wa e-Ardhi Dodoma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Maombi ya hati kupitia mfumo wa e-Ardhi kwa wakazi wa Dodoma bado yanaendelea kuwa changamoto kubwa. Mtumiaji anaweza kufanikiwa kutuma maombi kwenye mfumo, lakini maombi hayo hukaa muda mrefu bila kusonga kwenye hatua za uidhinishaji (approval stages) hadi pale anapomtafuta afisa anayehusika ndipo mchakato unaanza kusogea.

Hali hii inazua mazingira yanayoweza kuchochea vitendo vya rushwa, kwani haieleweki kwa nini afisa asifanye wajibu wake bila mwombaji kulazimika kumfuata na kuomba msaada. Kuna wakati maombi hukaa kwa afisa wa Entry Data kwa mwezi mzima au kwenye hatua ya mapitio ya CRO kwa muda mrefu bila hatua kuchukuliwa.

Je, mfumo huu umeanzishwa kwa lengo la kurahisisha huduma au kuongeza vikwazo kwa wananchi? Kwa sasa watumiaji wa mfumo wanaweza kuona hatua ambayo maombi yao yamekwama, hivyo ni muhimu maafisa wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa wakati.

Tunaomba Ofisi ya Ardhi Dodoma Jiji iwajibike na kufanyika kwa ukaguzi wa mfumo (system audit) ili kubaini changamoto zilizopo na kuondoa mianya inayoweza kusababisha ucheleweshaji au vitendo vya rushwa.
 
Hata ukiomba kwa hard_ copy (physically) Kuna mlolongo. Nina miezi miwili sasa na nilishalipa kila kitu na kujaza formula zao zote
 
Yangu Mimi mbona ilichukuwa mize minne tu, ni Halmashauri Fulani ya Mji..
Nahisi hiyo miji mikubwa ina vishoka wanataka kuwapiga
 
Ubunifu Kila kukicha, Ardhi Clinic, e-Ardhi, programme mbalimbali n.k lkn tatizo lipo pale pale.
 

Mimi nililipia hati na kukamilisha taratibu zote halmashauri lakini mpaka sasa ni mwaka mmoja na miezi kadhaa sijapatiwa hati, kila siku unaambiwa uje baada ya wiki, wiki mbili mara mwezi lakini ukienda hakuna kitu wala hakuna sababu za kueleweka toka kwa wahusika.

Inasikitisha na kuumiza sana Wizara ya Ardhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…