Changamoto ya usikuvu na mapambano katika soko la ajira

Changamoto ya usikuvu na mapambano katika soko la ajira

ALENI WAKALA

Member
Joined
Oct 31, 2023
Posts
33
Reaction score
28
HABARI WANAJAMII!!

Naitwa ALLEN WAKALA, nimehitimu shahada ya Utawala (Public administration) KATIKA Chuo Kikuu mzumbe. Nipo Dar es Salaam, ninapambana na changamoto ya maisha kama kijana anayejitegemea. Hata hivyo, ninakutana na kikwazo kikubwa kinachohusiana na afya yangu, kwani nina changamoto ya usikivu.

Kwa sasa, najiandaa kuingia katika soko la ajira, lakini changamoto yangu kubwa ni kuhusu mchakato wa usaili (interview), ambapo mara nyingi huhitaji mawasiliano ya moja kwa moja na usikivu mzuri.

Pamoja na changamoto hii, bado nina shauku kubwa ya kutumia elimu yangu kuboresha maisha yangu na kuleta mchango chanya katika jamii.

Nimeamua kusuka uzi huu ili kupata ushauri kutoka kwa wanajamii wenye uzoefu na maarifa, hasa:

1. Jinsi ya kushinda changamoto ya usikivu kwenye usaili wa kazi.
2. Mawazo ya mbinu za kujiajiri kwa kutumia ujuzi wangu wa Course niloyosoma.
3. Fursa za kazi zinazoweza kunifaa, hata nikiwa na changamoto ya usikivu.

Ninaamini kuwa jamii hii ina watu wenye maarifa na mioyo ya kusaidia. Naomba ushauri wenu, mawazo, au hata kama kuna fursa za ajira mnazojua ambazo zinaweza kunifaa.

Pia, ningependa kuwashukuru wale ambao wangependa kunisaidia kwa namna yoyote—iwe kwa ushauri, maelekezo, au hata kwa kunipa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu.
NAMBA ZANGU ZA SIMU 0624513983 AU 0747869519👈🏿(Whatsapp)
Barua Pepe: aleni.wakala2@gmail.com

Ninapambana, na siogopi changamoto. Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Asanteni sana!
 
Back
Top Bottom