Changamoto ya usikuvu na mapambano katika soko la ajira

ALENI WAKALA

Member
Joined
Oct 31, 2023
Posts
33
Reaction score
28
HABARI WANAJAMII!!

Naitwa ALLEN WAKALA, nimehitimu shahada ya Utawala (Public administration) Chuo Kikuu mzumbe. Nipo Dar es Salaam, ninapambana na changamoto ya maisha kama kijana anayejitegemea.

Hata hivyo, ninakutana na kikwazo kikubwa kinachohusiana na afya yangu, kwani nina changamoto ya usikivu.

Kwa sasa, najiandaa kuingia katika soko la ajira, lakini changamoto yangu kubwa ni kuhusu mchakato wa usaili (interview), ambapo mara nyingi huhitaji mawasiliano ya moja kwa moja na usikivu mzuri.

Pamoja na changamoto hii, bado nina shauku kubwa ya kutumia elimu yangu kuboresha maisha yangu na kuleta mchango chanya katika jamii.

Nimeamua kusuka uzi huu ili kupata ushauri kutoka kwa wanajamii wenye uzoefu na maarifa, hasa:

1. Jinsi ya kushinda changamoto ya usikivu kwenye usaili wa kazi.

2. Mawazo ya mbinu za kujiajiri kwa kutumia ujuzi wangu wa Course niloyosoma.

3. Fursa za kazi zinazoweza kunifaa, hata nikiwa na changamoto ya usikivu.

Ninaamini kuwa jamii hii ina watu wenye maarifa na mioyo ya kusaidia. Naomba ushauri wenu, mawazo, au hata kama kuna fursa za ajira mnazojua ambazo zinaweza kunifaa.

Pia, ningependa kuwashukuru wale ambao wangependa kunisaidia kwa namna yoyote—iwe kwa ushauri, maelekezo, au hata kwa kunipa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu.
NAMBA ZANGU ZA SIMU
Barua Pepe: aleni.wakala2@gmail.com

Ninapambana, na siogopi changamoto. Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Asanteni sana!
 
Kwa sasa sahau kuhusu public administration tafuta ujuzi wa kueleweka, kwanza kwa elimu ya Tz na kozi kama hio sidhani kama kuna ujuzi hapo, hizo fikra za public administration waachie taesa na ajira portal wazizoom 😂, halafu kama unachangamoto kama hio jikite sana na kutafuta ujuzi ambao hauathiriwi na tatizo lako ili walau kidogo unakua special, ila hakuna profit organization ya private sector watakuajili kwa huruma hata siku moja labda ya ndugu.
 
Pole Sana.

Ila njia nyingine ambayo ni bora zaidi jikite kufanya kazi kwakutumia teknolojia mfano Simu , computer n.k

Hii itakupa utulivu zaidi

Mfano umesoma Afisa mahusiano unaweza kujibrand Kama Afisa masoko na mahusiano Kwa wakati mmoja na ukawa unailink Kampuni na clients mbali mbali kupitia E-mail n.k .

Jaribu kuandaa CV nzuri Sana
Kuwa closed na hr mbalimbali
Then watumie email huku uki-highlight namna gani utaongeza potential katika Kampuni zao.

Kwa sasa Kampuni ni nyingi hasa DSM na kipindi hiki watu hawakai sehemu mmoja hivyo kupata Kazi ni rahisi endapo ukatumia mbinu mbali mbali Kama hizo.

NB kuwapata hr tumia LinkedIn usisubiri nafasi itangazwe wewe watumie email au ingia inbox.

Tumia ule mchezo wa namba the more you try the more you get
 
Asante Sana Maoni Yako nimeyapoke mkuu
 
ASANTE SANA
USHAURI WAKO NI MZURI SANA, NTAJITAHIDI KUUFANYIA KAZI, UBARIKIWE MKUU🙏
 
HABARI WANAJAMII!!

Naitwa ALLEN WAKALA, nimehitimu shahada ya Utawala (Public administration) Chuo Kikuu mzumbe. Nipo Dar es Salaam, ninapambana na changamoto ya maisha kama kijana anayejitegemea.

Hata hivyo, ninakutana na kikwazo kikubwa kinachohusiana na afya yangu, kwani nina changamoto ya usikivu.

Kwa sasa, najiandaa kuingia katika soko la ajira, lakini changamoto yangu kubwa ni kuhusu mchakato wa usaili (interview), ambapo mara nyingi huhitaji mawasiliano ya moja kwa moja na usikivu mzuri.

Pamoja na changamoto hii, bado nina shauku kubwa ya kutumia elimu yangu kuboresha maisha yangu na kuleta mchango chanya katika jamii.

Nimeamua kusuka uzi huu ili kupata ushauri kutoka kwa wanajamii wenye uzoefu na maarifa, hasa:

1. Jinsi ya kushinda changamoto ya usikivu kwenye usaili wa kazi.

2. Mawazo ya mbinu za kujiajiri kwa kutumia ujuzi wangu wa Course niloyosoma.

3. Fursa za kazi zinazoweza kunifaa, hata nikiwa na changamoto ya usikivu.

Ninaamini kuwa jamii hii ina watu wenye maarifa na mioyo ya kusaidia. Naomba ushauri wenu, mawazo, au hata kama kuna fursa za ajira mnazojua ambazo zinaweza kunifaa.

Pia, ningependa kuwashukuru wale ambao wangependa kunisaidia kwa namna yoyote—iwe kwa ushauri, maelekezo, au hata kwa kunipa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu.
NAMBA ZANGU ZA SIMU
Barua Pepe: aleni.wakala2@gmail.com

Ninapambana, na siogopi changamoto. Ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

Asanteni sana!
Pole sana ndugu kumbe una changamoto ya kusikia,pole sana Cha msingi dhidi kuomba Mungu na Wala usikate tamaa
 
Back
Top Bottom