GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Siikumbuki jina la clip.
Katika hiyo clip, Wazungu walikuwa wakijadili changamoto za Afrika, ambapo mmoja alionesha kushangazwa na tabia ya Mwafrika. Alisema kwamba Mwafrika anaweza akanunua simu ya gharama kubwa wakati choo hakina maji.
Siyo Watanzania wote, lakini wengi wanaweza wakaangukia kwenye mojawapo ya hizi changamoto:
1. Kutokujua jinsi ya kutumia choo kiusahihi
2. Kutokuwa na vyoo vinavyoikidhi vigezo vya kiafya na kiusalama
Mbaya ni kwamba hata watu
wanaochukuliwa kuwa wameelimika nao wanaweza wakaangukia kwenye mojawapo ya hayo makundi. Hii ni mifano niliyowahi kuishuhudia:
1. Choo cha nyumbani kisicho na mlango
Kwa wengine inaweza ikawa ni kawaida, lakini mimi nilishindwa kuelewa sababu ya hicho choo kutokuwa na mlango. Hela haikuwa tatizo kwake.
Nyumba yake ilikuwa kubwa na aliizungushia uzio wa tofali/ukuta.
Aliiwekea milango vyumba vyote vya ndani ikiwa ni pamoja na bafu na choo cha ndani.
Lakini choo cha nje, kiliachwa bila mlango. Kwa hiyo mtu aendapo huko, humlazimu kutembea "akiimba" ili kama kuna mtu atoe taarifa mapema.
2. Choo cha shule ya Msingi
Nilikiona miaka ya hivi karibuni wilayani Misungwi. Baada ya kupata fedha za Covid 19, hiyo shule ilizielekeza kwenye ujenzi wa vyoo vya wanafunzi. Vilikuwa vyoo vya shimo. Baada ya kupauliwa, kulijengwa ukuta mbele ya vyumba vyenye matundu ya vyoo ili kuwepo na mlango mmoja wa kuingilia kwenye korido ya vyoo. Lakini vyumba vyenye matundu ya vyoo havikuwekewa milango. Kwa hiyo mwanafunzi apitapo kwenda chooni wakati mwenzake yumo ndani, ana uchaguzi wa kumtazama au la. Hakuna kizuizi chochote cha kumfanya aliyepo chooni awe "faragha"
3. Choo cha shule ya Sekondari
Ilikuwa ni shule binafsi mkoani Mwanza. Na choo hicho klichangiwa na wanafunzi na walimu wao.
Nacho kilikuwa hakina milango, badala yake kulikuwa na ukuta mbele ya vyumba vya vyoo kumzuia aliye nje ya jengo la choo kuona kinachoendelea kwenye vyumba vya vyoo. Lakini ukishaingia kwenye korido la choo, utakwepa tu kumwona aliyemo kwenye chumba cha choo ikiwa utaamua kuangalia upande mwingine unapotembea kuelekea kwenye chumba cha choo ulichochagua ambacho nacho hakina mlango pia.
Lakini hiyo shule siyo kwamba haikuwa na uwezo wa kuweka milango, hapana.
Iweze kulipa mishahara ya walimu, iwe na makompyuta ya kutosha, iwe na magari, imudu kuwa na vifaa vya maabara, n.k., halafu ishindwe kuweka milango ya vyoo?
Ni kwamba milango haikuwa kipaumbele kwa wakati huo. Kama ingelikuwa haina uwezo, ingewakopa hata walimu wake.
Japo kulikuwa na mpango wa kuwekewa milango huko mbeleni, lakini haikuwa sahihi kutumika katika hali hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Hiyo inaonesha kwamba tatizo kubwa lipo kwenye mitazamo. Suluhisho likipatikana hapo na vyoo safi na salama kwa matumizi sahihi ya binadamu vitapatikana hata kwenye kaya masikini.