Changamoto za Ajira Portal

Changamoto za Ajira Portal

Habari zenu wakuu, mimi ni muathirika wa hili janga la ukosefu wa ajira linalotusumbua vijana wa kitanzania kila uchwao, nimekuwa nikifanya bidii za kutafuta kazi bila kuchoka kwani naamini kuwa mtafutae huwa hachoki.

Sasa niende moja kwa moja kwenye hoja, ni kwamba serikali kupitia Utumishi wana system yao inayoitwa Ajira portal ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuomba kazi za serikalini.

Kwakweli system hii tangu ifanyiwe marekebisho imekuwa moja kati ya system mbovu ambazo nazijua, kila ninapoomba kazi za serikalini kupitia Ajira portal naambiwa failed huwezi kuomba kazi hii kwakuwa hujakidhi vigezo, wakati ukweli ni kwamba nimekidhi vigezo vyote wanavyotaka na pia vigezo vinavyotakiwa kwenye kazi husika.

Jambo hili limekuwa sugu kiasi cha kwamba si mimi peke yangu ninayeilalamikia system hii bali tupo wengi na hata tunapowatumia msg kupitia namba walizoweka hawajibu lakini tunapowapigia simu wanatoa majibu mepesi as if system haina tatizo lolote.

Tunaomba wahusika waliangalie hili mapema au kama sivyo basi tutaamini kuwa jambo hili ni mpango mkakati wa wahusika kupeana kazi kwa kujuana.

NawasilishaView attachment 1453119View attachment 1453119
unategemea nn kazi chache waombaji ni maelfu lazima system ichanganyikiwe ..
 
Hilo nilikutana nalo juzi wakati naomba nafas fulani, nikashangaa mana nilikuwa nimekizi vigezo. Nilifanya hivi
1. Nilibadilisha vigezo tofauti kabisa ambavyo sina ila vipo kwenye tangazo ili kuangalia kama itakubali, chakusangaza ilikubali ila sikumalizia sehemu ya kuweka barua.
2. Nikarudi tena na kubadilisha vigezo na kuweka vyangu sahihi ikakubali, nikamalizia kuweka barua
3. System yao haipo stable so ukiweza kui trick kama nilivyofanya nadhani utafanikiwa. Kila laheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, mkuu ubarikiwe sana nilikuwa naumia roho kila napotumia mfumo huo jibu ni failed nilifikia kipindi nikatamani nifute details zangu tu, sababu nmeupdate information lakin bado ni yale yale tu..

Walau nitaendelea kujaribu kuomba japo kibishi system ishakuwa mbovu ka mgonjwa wa degedege daah shida kweli.

Wahusika walifanyie kazi hilo jambo..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu, mimi ni muathirika wa hili janga la ukosefu wa ajira linalotusumbua vijana wa kitanzania kila uchwao, nimekuwa nikifanya bidii za kutafuta kazi bila kuchoka kwani naamini kuwa mtafutae huwa hachoki.

Sasa niende moja kwa moja kwenye hoja, ni kwamba serikali kupitia Utumishi wana system yao inayoitwa Ajira portal ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuomba kazi za serikalini.

Kwakweli system hii tangu ifanyiwe marekebisho imekuwa moja kati ya system mbovu ambazo nazijua, kila ninapoomba kazi za serikalini kupitia Ajira portal naambiwa failed huwezi kuomba kazi hii kwakuwa hujakidhi vigezo, wakati ukweli ni kwamba nimekidhi vigezo vyote wanavyotaka na pia vigezo vinavyotakiwa kwenye kazi husika.

Jambo hili limekuwa sugu kiasi cha kwamba si mimi peke yangu ninayeilalamikia system hii bali tupo wengi na hata tunapowatumia msg kupitia namba walizoweka hawajibu lakini tunapowapigia simu wanatoa majibu mepesi as if system haina tatizo lolote.

Tunaomba wahusika waliangalie hili mapema au kama sivyo basi tutaamini kuwa jambo hili ni mpango mkakati wa wahusika kupeana kazi kwa kujuana.

HABARI;

Sasa mfumo umeboreshwa kiasi kwamba kama huna sifa stahiki huwezi kuomba kazi. Ujumbe unaoletewa ni muhimu sana kuuelewa kwani ili uweze kufanikiwa kuomba, hakikisha degree/diploma uliyonayo ni sawa na zile zilizowekwa kwenye tangazo la ajira. Ukiudanganya mfumo haitasaidia.

Maboresho ya mfumo yanaruhusu waombaji wenye sifa pekee kwa mujibu wa tangazo waweze kuomba na hivyo kuondoa maombi ya waombaji wasio na sifa. Endapo sifa zote unazo na unashindwa kuomba wapigie namba zinazopatikana kwenye portal ya ajira ili wakusaidie.

Mwisho;
Kuna user manual imetolewa kwenye portal ya ajira ambayo inaelekeza hatua za kufanya na maboresho yapi yamefanyika.
 
Mimi tatizo ku update namba ya Nida, kila nkieka naulizwa maswali ma 5, nayajibu namaliza nkienda ku apply naambiwa sijaweka namba ya nida..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi tatizo ku update namba ya Nida, kila nkieka naulizwa maswali ma 5, nayajibu namaliza nkienda ku apply naambiwa sijaweka namba ya nida..

Sent using Jamii Forums mobile app
Soma ile user manual iliyoko pale kwenye portal ikuelekeze na unaweza wapigia simu kupitia namba za simu zinazopatikana kwenye portal ili wakusaidie. Mfumo sasa umekuwa mzuri sana
 
Naomba kuuliza kwa wanaofahamu,

Hivi Ajira Portal huwa wanashotlist majina kabla ya kuwaita kwenye interview? sababu naona majina mengi mno kwa nafasi chache kama hakuna aliyekuwa shortlisted vile, au wanashortlist watu baada ya interview ila mkiapply mnaitwa wote.
 
Naomba kuuliza, je Post ya Administrative Officer iii, huko SUA wameshafanya interview au wanafanya lini?
 
Naomba kuuliza kwa wanaofahamu,hivi Ajira Portal huwa wanashotlist majina kabla ya kuwaita kwenye interview sababu naona majina mengi mno kwa nafasi chache kama hakuna aliyekuwa shortlisted vile, au wanashortlist watu baada ya interview ila mkiapply mnaitwa wote.
Mkuu huwa wanashortlist.
Tatizo leo wahitimu ni wengi wenye sifa na hata walioko makazini kampuni binafsi na serikali wanaomba wakikidhi masharti.

Kama wasingekuwa wanashortlist hapo ungeona watu zaidi ya 10k+ kwa kada moja
 
Back
Top Bottom