Habari zenu wakuu, mimi ni muathirika wa hili janga la ukosefu wa ajira linalotusumbua vijana wa kitanzania kila uchwao, nimekuwa nikifanya bidii za kutafuta kazi bila kuchoka kwani naamini kuwa mtafutae huwa hachoki.
Sasa niende moja kwa moja kwenye hoja, ni kwamba serikali kupitia Utumishi wana system yao inayoitwa Ajira portal ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuomba kazi za serikalini.
Kwakweli system hii tangu ifanyiwe marekebisho imekuwa moja kati ya system mbovu ambazo nazijua, kila ninapoomba kazi za serikalini kupitia Ajira portal naambiwa failed huwezi kuomba kazi hii kwakuwa hujakidhi vigezo, wakati ukweli ni kwamba nimekidhi vigezo vyote wanavyotaka na pia vigezo vinavyotakiwa kwenye kazi husika.
Jambo hili limekuwa sugu kiasi cha kwamba si mimi peke yangu ninayeilalamikia system hii bali tupo wengi na hata tunapowatumia msg kupitia namba walizoweka hawajibu lakini tunapowapigia simu wanatoa majibu mepesi as if system haina tatizo lolote.
Tunaomba wahusika waliangalie hili mapema au kama sivyo basi tutaamini kuwa jambo hili ni mpango mkakati wa wahusika kupeana kazi kwa kujuana.
Nawasilisha
View attachment 1453119View attachment 1453119