Changamoto za Ajira Portal

Changamoto za Ajira Portal

Mimi nimepata ajira kwenye taasisi nyeti nchi Hii bila kuwa na ndugu wala kushikwa mkono. Mkuu jipange ufaulu interview acha kusingizia upendeleo
Si kama watu hawapati ila usumbufu ni mkubwa usio na lazima,hivyo kupelekea majina machche tu ya candidates ndiyo yanawafikia huko utumishi...
Bado kwangu mfumo wa zamani ndiyo rafiki kwa mazingira ya kibongo sehemu ambapo hata internet yetu ipo weak
 
Hii kitu wangeondoa, dogo kashindwa kuapply na alikuwa na the same qualification ila akitaka kuapply inamkatalia inamwambia haja-qualify!

Simu hazipatikani na zinazopatikana hawapokei, katuma email kulalamika hakuna aliyejibu basi majanga tupu huu mfumo wangeondoa tu! Ni kero tupu
Upo sahihi 100%
 
Mm nauluza, ajira portal inataka uweke namba ya NIDA na kama inavyofahamika si wote wenye hizo namba kwann hawajaweka alternative ya hiyo namba mfano barua kutoka serikali za mtaa nk
Mambo mengi ya msingi hawakufikiria....eti unaulizwa taja makazi yako ya kudumu....hili swali unalijibuje kwa mfano?
Ukijaza unapoishi sasa wanakupa X ukijaza ulipokuaga unaishi kipindi unajisajiri Nida wanakupa X..
 
Kurudisha taasisi ziajiri zenyewe ni jambo la muda tu, kwa sababu watu wanaongezeka na central recruitment ni mambo ya kizamani.

Wanaosema taasisi kuajiri zinaleta ukabila, nani kakwambia central recruitment hakuna kunuana? There is no 100% fairness Duniani. Hata huko utumishi bado kuna kujuana.

Tutarudi tu kama zamani, labda utumishi watabaki kuajiri watu wa serikali kuu, ila serikali za mitaa, taasisi zitarudishiwa tu.
 
Si kama watu hawapati ila usumbufu ni mkubwa usio na lazima,hivyo kupelekea majina machche tu ya candidates ndiyo yanawafikia huko utumishi...
Bado kwangu mfumo wa zamani ndiyo rafiki kwa mazingira ya kibongo sehemu ambapo hata internet yetu ipo weak
Kiujumla hatujawekeza kwenye software infrastrucure na ni sababu ya kuwa na changamoto lukuki maeneo karibu yote tulikoamua kutumia njia za mtandao kufanya kazi. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kufanya maboresho na si kujikita tu kwenye mabarabara, reli n.k
 
  • Thanks
Reactions: amu
Mambo mengi ya msingi hawakufikiria....eti unaulizwa taja makazi yako ya kudumu....hili swali unalijibuje kwa mfano?
Ukijaza unapoishi sasa wanakupa X ukijaza ulipokuaga unaishi kipindi unajisajiri Nida wanakupa X..
Makazi ya kudumu wewe ndiye uliyejaza kwenye data za NIDA na fomu ulijaza Mwenyewe, unashindwa vip kukumbuka?
 
Si kama watu hawapati ila usumbufu ni mkubwa usio na lazima,hivyo kupelekea majina machche tu ya candidates ndiyo yanawafikia huko utumishi...
Bado kwangu mfumo wa zamani ndiyo rafiki kwa mazingira ya kibongo sehemu ambapo hata internet yetu ipo weak
Hiyo nayo ni sehemu ya mchujo maana ajira ni chache na waombaji ni wengi
 
Aliyekuambia undugu umetoweka nani mkuu wewe kama huna mtu kwenye taasisi yoyote ile andika maumivuu
Huu ni uongo mimi kama mtu nilieshuhudia zaidi ya watu 5 wakiajiliwa katika taasisi nzuri tu na hawana ndugu yoyote yule just wameshinda interview na wakawa offered job, Ajira portal unahitaji marekebisho kidogo katika System tu tena kidogo sana ila katika swala la transparency aisee Katibu mkuu Ajira Bwana Xavier amefanya kazi kubwa sana kuhakikisha haki inasimamiwa katika Saili mbalimbali. Nawapa pongezi team nzima inayosimamia
 
Kwani wewe huna ndugu?
Ninao ndugu. Tena kutokana na ajira yangu kuwa taasisi kubwa wanadhani kuwa nitawasaidia kupata kazi, huwa nawajibu tu kuwa siku hizi hayo masuala hayapo, hiyo kazi ya kuajiri inafanywa na taasisi moja tu nchini. Imenipunguzia usumbufu. Tukizipa taasisi mandate ya kuajiri tujiandae kwa upendeleo mkubwa kwenye nafasi za kazi serikalini. Mimi nasema ajira portal iendelee hivyo hivyo maana imepunguza kujuana kwa asilimia kubwa sana. Kikubwa, mapungufu yashughulikiwe.

Nadhani wewe una Kibosile mahali unataka mfumo wa zamani urudishwe ili akusaidie. Mkuu komaa fanya vizuri usaili kazi utapata. Kuhusu changamoto za mfumo, zitaboreshwa, hakuna kitu kipo [emoji817] kwa [emoji817] perfect
 
Bora vile kwa maana hata kama hela ya chai utatoa lkn kitaeleweka,ni afadhali mbona humu mabarabarani tunawapatia wajomba hela kidogo ya chai wanakuacha unaenda zako?
Sio kila mtu ana hio hela ya chai, Ushauri wangu ni kuwa Soma kwa bidii uje ufaulu usaili upate kazi, Impact ya huu mfumo wa ajira portal ni kubwa sana na utaona matokeo Chanya siku za usoni mana Almost watu wanaoingia nao kazini ni watu makini na sio watu wakubebwa bebwa sijui na uncle
Hata chain ya undugu kwenye taasisi inapunguza ufanisi ambapo Taasisi haiwezi kufanya kazi katika efficiency kubwa wewe leo ukienda sehemu na ukapata kazi afu mkurugenzi ni baba yako tena alikubeba basi tutegemee uozo tu sina mana hupaswi kupata kazi ofisi ya baba yako lahasha ila iwe kwa juhudi zako, Private na wenzetu nje huangalia zaidi mtu kichwani ana nini na sio sijui huyu ni mtoto wa nani, nimefanya kazi na kampuni ya kimarekani process zao za ku recruit ni poa sana mana ni wewe tu na kichwani unakipi cha kuoffer
 
Ukisema Tassisi ziajiri Kama zamani,
Kama Huna Ndugu kwenye Tasisi inayoajiri,kilio chake ni Mara 1000 ya unayodhani ni mapungufu ya system
Ni kweli kabisa,hiyo portal ibakie,ila ifanyiwe marekebisho makubwa ili isisumbue.
 
Ninao ndugu. Tena kutokana na ajira yangu kuwa taasisi kubwa wanadhani kuwa nitawasaidia kupata kazi, huwa nawajibu tu kuwa siku hizi hayo masuala hayapo, hiyo kazi ya kuajiri inafanywa na taasisi moja tu nchini. Imenipunguzia usumbufu. Tukizipa taasisi mandate ya kuajiri tujiandae kwa upendeleo mkubwa kwenye nafasi za kazi serikalini. Mimi nasema ajira portal iendelee hivyo hivyo maana imepunguza kujuana kwa asilimia kubwa sana. Kikubwa, mapungufu yashughulikiwe.

Nadhani wewe una Kibosile mahali unataka mfumo wa zamani urudishwe ili akusaidie. Mkuu komaa fanya vizuri usaili kazi utapata. Kuhusu changamoto za mfumo, zitaboreshwa, hakuna kitu kipo [emoji817] kwa [emoji817] perfect

Kwa hiyo wasiofaulu usaili hawajui kitu mkuu au? Nafasi mbili watu 65 hapo ataepata ndio anajua sana kuliko wengine au sio mkuu
 
Kwa hiyo wasiofaulu usaili hawajui kitu mkuu au ? Nafas mbili watu 65 hapo ataepata ndio anajua sana kuliko wengine au sio mkuu
Ndio mana kuna inshu ya Kanzidata(Database) Ukifika japo oral na ukafaulu chance ya kuitwa pakitokea uhitaji ni kubwa, Kama umekuwa aware na Placements zao huwa wanasema ambao hawajaona majina yao basi wajue hawakupata nafasi/ hawakufauli usaili ivo unaweza kufaulu na usipate nafasi kutokana na uchache wa vacancies ila whenever chances occurred you will be summoned
 
Verification mara ngapi?serikali umenihakiki na kuridhika ukanipatia card kama kithibitisho kupitia taasisi maalum ya Nida leo hii naombabajira sehemu serikali hiyo hiyo kupitia taasisi nyingine wanashindwa kuamini uraia wangu!mambo ya ajabu sana
No coordination bro
 
Ndugu yako kashindwa kukupa connection kwa sababu ha hii na kama tasisi zitaajili nahakkka Mjomba wako ndani ya wiki atakupatia ajira
 
Kwa hiyo wasiofaulu usaili hawajui kitu mkuu au ? Nafas mbili watu 65 hapo ataepata ndio anajua sana kuliko wengine au sio mkuu
Kwani darasa la watu 300 wote mlikuwa mnapata maksi sawa kwenye mtihani? Factors zitatumika nyingi ili kupata candidates wa nafasi husika na sio kwamba wanakosa kazi ni vilaza bali ukweli ni kuwa nafasi ni chache, hivyo wanaokosa sio wajinga bali tu hawakupita kwenye chujio
 
Tatizo si kujuana shida imekua ikisemwa ni vyeti feki..kama urasimu huunashindwa kuuona basi inashangaza
Urasimu unaousema ni muhimu kuwepo kwa kuwa ni 'verification procedures' yaani hatua za uthibitisho maana huyo atakayeajiriwa atakuwa mwakilishi wa serikali katika kuhudumia umma. Mtu wa hivyo ni muhimu athibitishwe kuwa ndiye anayefaa kuhudumia umma kupitia kodi za wananchi.
Kama taarifa zako kuhusu kufaa kwako hazina wasiwasi basi huna haja ya kuuchukia huo unaouita urasimu maaa upo kwa nia njema.
 
Za majukumu Wakuu,

Nina jaribu hapa kumfungulia mtu account ajira portal, mwisho inaniambia ni activate account, sijui ukitaka ili ifanye kazi unafanya nini, baada ya kuwa umeji register?
 
Back
Top Bottom