Kwa 'tech-preneurs' hii ni fursa. Inaweza kutatuliwa kwa njia moja tu (kwa jinsi ninavyofikiri mimi) ambayo ni ESCROW.
ESCROW NI NINI?
Achana na habari za Tegeta Escrow; hapa nafafanua Escrow yenyewe kabisa - Ni malipo yanayohifadhiwa na 'third party' mpaka pale vigezo na masharti yatakapotimizwa. Kwa mfano; Tuseme mtu anataka kuagiza kuku watatu; hatua ya kwanza anakupigia simu ili kujua bei, muda utakaotumia kumfikishia na sifa za kuku. Mkikubaliana anafanya malipo kwenda kwenye akaunti ya escrow. Wewe muuzaji unapewa taarifa kuwa kuna malipo kwaajili ya kuku watatu yamefanywa katika akaunti ya Escrow na unatakiwa kufanya delivery ya kuku kwa namna mlivyokubaliana.
Kisha wewe unafanya delivery. Na mteja akithibitisha kupokea mzigo wenye sifa mlizokubaliana basi pesa inatumwa kuja kwako muuzaji.
View attachment 1480907
SWALI NI JE, VIPI KAMA MTEJA AKILIPA HALAFU AKAPOKEA MZIGO TOFAUTI NA MAKUBALIANO.
Mteja akipokea mzigo aidha umeharibika, au una mapungufu yoyote yale, au umefika kwa kuchelewa - hapo ndipo ;third party anaingia. Third party ndiye msuluhishi na kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa mwanzo kabisa wa process ya kuuziana mnaweka wazi makubaliano yenu juu ya nini kifanyike endapo changamoto tajwa hapo juu zitajitokeza.
Vivyo hivyo upande wa mteja; iwe amezima simu, au analeta janja janja ya namna yoyote - kwanza anatakiwa ajue kuwa anaiweka hatarini pesa yake. Kwasababu kama makosa ni ya mteja basi pesa inatumwa kwa muuzaji.
Lakini hii kitu yote inahitaji kuwekwa katika mfumo rahisi, salama na ambao una kasi ya kuendana na mazingira ya sasa. Actually mimi nipo nalifanyia kazi wazo hili. Lakini najua wazo ni wazo mpaka pale linapofanyiwa kazi - hivyo ni fursa pia kwa mjasiriamali yeyote anaeweza kuliweka wazo hili katika matendo.
Ukweli ni kwamba; tayari kuna kampuni nyingi zinafanya kazi kwa kutumia mfumo huu nje ya nchi, mfano ni hawa:
PAYLAX, ESCROW KENYA na
ESCROW.COM. Ila hapa kwetu bado changamoto.
Kuna mawili; Tulifanyie kazi kabla big players hawajaingia au tusubiri mpaka watakapoingia halafu sisi tuwe watumiaji tu. Vyovyote iwavyo mfumo huu utaondoa changamoto nyingi za e-commerce... ikiwemo madalali. Eee si ndio? Utamdalalia vipi mtu wakati pesa hupati mpaka mzigo umfikie mteja na aukubali.
BOTTOM LINE
Business can solve anything.