Changamoto za Biashara ya Delivery kwa Bongo

Changamoto za Biashara ya Delivery kwa Bongo

Aisee delivery zina changamoto mno ila ukiwapata Wazungu au Wahindi au Wachina uta enjoy sana
Mie kuna mdau juzi ananiambia nimwagizie hadi ufike ndio achukue wee nilisoma sms nikakaa kimya maana chumba kimejaa bidhaa za watu bila hata mteja
 
Kote kote tu changamoto, wauzaji nao vichefuchefuuu. Unachoagiza sicho unacholetewa na ushaingia gharama[emoji134]

Au picha anatumia ya quality nyinginee bidhaa anayouza sasa[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
 
Tena yule anaye kusisitiza sana muogope sana huyo make hapo ndo huwa anatengeneza mazingira ya kukataa ili baadae useme kwamba kweli alikuwa na nia ila imetokea bahati mbaya. Waogope sana wanap sisitiza mno
Duh inaumiza sana yaan mm mwanzo nilitoa chozi mtu ananisisitiza sanaaa anataka huduma mpaka unamuamini unaarrange namna ya kwenda hahahhahahahahah ukifika muda anakwambia kapata dharura dah bongo nyoso
 
Kwasisi wa tz hizi biashara za kimtandao tunafanya tu kama hobbies nyingine yaani tunajaribu hatupo nayo serious sana. Hii mwisho wa siku inafanya tusione unafuu unaokuja na huu mfumo.

A. Wauzaji.

1. Anatangaza bidhaa au huduma bei anasema njoo inbox.
2. Anatangaza bidhaa au huduma but hatoi full description ya anachouza au huduma anayotoa.
3. Anakuwa na majibu ya jazba pale wateja wanapohoji au kidadisi kuhusu bidhaa au huduma.

4. Jambo la ajabu ni nafuu sana kwenda kununua kitu kariakoo kuliko mtandaoni, wanauza vitu kwa bei za kilanguzi sana plus wanapenda kuweka gharama za after service kama delivery charges zimuangukie mteja mwisho wa siku wateja hawaoni unafuu wowote.

5. Wauzaji wanakuwa interested kuuza tu na sio kutoa huduma kwa mteja kwa maana ya baada ya mauziano kupata mrejesho wake kuwa ameridhika ama la. Unaweza letewa kitu ukakuta ni kinyume na standard ulitaka then unashangaa ukimjulisha muuzaji anakuwa mbogo na wachache sana wanakuwa tayari kukusaidia kupata haki yako kama mteja.

6. Hakuna hati ya makabidhiano kama risiti wengi wanafanya biashara kiholela tu sababu hawana trainings za kuwa merchant wa mtandaoni.
Yapo mengine mengi sana yanayokwamisha hii kitu.

B. Wanunuzi.

1. Hawana imani na mauziano ya kimtandao.
2. Hawapo tayari kuingia gharama ya ziada na bei halisi wanaijua na wanajua wapi wanaweza pata bidhaa hiyo wakitaka kwa unafuu zaidi.
3. Wengi huagiza kama kujaribu na sio serious kuwa wanataka kuwa tegemezi ya mfumo huo wa manunuzi kwa njia ya mtandao.
4. Uvivu wa kufanya research ya anachotaka mfano hawasomi maelezo kama yakiwapo wanakwenda straight kuuliza details hata kama zipo kwenye bango.

So ili huu mfumo wa biashara mtandaoni ufanikiwe inabidi pande zote mbili wawe serious na kutokuwa na makando makando na kudeal na uhalisia wa mazingira ya kibiashara na sio kuwmbase uongo na taarifa za kusadikika.
Umeelezea vyema kabisa.
 
Haya ni huko facebook mkuu na ni kitambo kidogo, nilikuja kuacha, na kubadili model
Acha kabisa wacha tukomae mdogo mdogo kama mwl rtc maana nae alitukanwa sana humu ila mwisho wa siku kila mtu anamwelewa labda aliejiunga leo jf ndio hata mwamini ila jamaa ni mwaminifu hadi kwenye uaminifu wenyewe so ngoja nasi tupambane
 
Ndio mana wanasema biashara ni akili nying inabid itumike.mim nmeavoid biashara zote za kunyenyekea mteja.sasa biashara nazofanya ni either utataka au hutak unasepa.na amani ya moyo nmeiona kubwa snaaa toka nilipoanza ubunifu wa biashara hzo.na pesa mbele pia
 
Kwa 'tech-preneurs' hii ni fursa. Inaweza kutatuliwa kwa njia moja tu (kwa jinsi ninavyofikiri mimi) ambayo ni ESCROW.

ESCROW NI NINI?
Achana na habari za Tegeta Escrow; hapa nafafanua Escrow yenyewe kabisa - Ni malipo yanayohifadhiwa na 'third party' mpaka pale vigezo na masharti yatakapotimizwa. Kwa mfano; Tuseme mtu anataka kuagiza kuku watatu; hatua ya kwanza anakupigia simu ili kujua bei, muda utakaotumia kumfikishia na sifa za kuku. Mkikubaliana anafanya malipo kwenda kwenye akaunti ya escrow. Wewe muuzaji unapewa taarifa kuwa kuna malipo kwaajili ya kuku watatu yamefanywa katika akaunti ya Escrow na unatakiwa kufanya delivery ya kuku kwa namna mlivyokubaliana.

Kisha wewe unafanya delivery. Na mteja akithibitisha kupokea mzigo wenye sifa mlizokubaliana basi pesa inatumwa kuja kwako muuzaji.

escrow_model.png

SWALI NI JE, VIPI KAMA MTEJA AKILIPA HALAFU AKAPOKEA MZIGO TOFAUTI NA MAKUBALIANO.

Mteja akipokea mzigo aidha umeharibika, au una mapungufu yoyote yale, au umefika kwa kuchelewa - hapo ndipo ;third party anaingia. Third party ndiye msuluhishi na kazi yake kubwa ni kuhakikisha kuwa mwanzo kabisa wa process ya kuuziana mnaweka wazi makubaliano yenu juu ya nini kifanyike endapo changamoto tajwa hapo juu zitajitokeza.

Vivyo hivyo upande wa mteja; iwe amezima simu, au analeta janja janja ya namna yoyote - kwanza anatakiwa ajue kuwa anaiweka hatarini pesa yake. Kwasababu kama makosa ni ya mteja basi pesa inatumwa kwa muuzaji.

Lakini hii kitu yote inahitaji kuwekwa katika mfumo rahisi, salama na ambao una kasi ya kuendana na mazingira ya sasa. Actually mimi nipo nalifanyia kazi wazo hili. Lakini najua wazo ni wazo mpaka pale linapofanyiwa kazi - hivyo ni fursa pia kwa mjasiriamali yeyote anaeweza kuliweka wazo hili katika matendo.

Ukweli ni kwamba; tayari kuna kampuni nyingi zinafanya kazi kwa kutumia mfumo huu nje ya nchi, mfano ni hawa: PAYLAX, ESCROW KENYA na ESCROW.COM. Ila hapa kwetu bado changamoto.

Kuna mawili; Tulifanyie kazi kabla big players hawajaingia au tusubiri mpaka watakapoingia halafu sisi tuwe watumiaji tu. Vyovyote iwavyo mfumo huu utaondoa changamoto nyingi za e-commerce... ikiwemo madalali. Eee si ndio? Utamdalalia vipi mtu wakati pesa hupati mpaka mzigo umfikie mteja na aukubali.

BOTTOM LINE
Business can solve anything.
 
View attachment 1480907

Good idea
 
Ndio mana wanasema biashara ni akili nying inabid itumike.mim nmeavoid biashara zote za kunyenyekea mteja.sasa biashara nazofanya ni either utataka au hutak unasepa.na amani ya moyo nmeiona kubwa snaaa toka nilipoanza ubunifu wa biashara hzo.na pesa mbele pia

Ni Ile ya kulima mahindi?
 
Njoo inmbox nazani huwa ni kwa ajili ya negotiation wanaaogopa to negotiate bei hadharani make na wengine watataka hiyo hiyo
Kama hiyo ndo sababu ya kuita wateja inbox basi kiaina wanafeli.
Negotiation inakuja baada ya kujua bei halisi. Sio post ya bidhaa imekaa kizembezembe tuu yani hata muamko wa kununua unapungua kama sio kuisha kabisa.
 
Unaiuzaje hiyoo HP....
Mkuu kwa hayo alivyoeleza jamaa hapo juu ni kweli tupu maana hali tulionayo hadi aibu tupu mimi nina kampuni yangu ya kuagiza mizigo midogo midogo hasa electronic kutoka mataifa ya ulaya na amerika, sasa unakuta mtu anakwambia niagizie kitu fulan mpaka ifike nitakuwa tayari nina hela aisee mtu unajipinda kununua mzigo unafika jamaa unamtafuta hapatikani au anasingizia mengine.

Balaa lake linakuja pale amekuagiza kitu ambacho ni ngumu wewe kupata mteja hadi inauma sana mfano nina macomputer ya ajabu ajabu mno bei zake ni ghali sana nimebaki naziangalia tuView attachment 1479452
Kupata tu hata mteja wa kuiulizia ni shughuli
 
Back
Top Bottom