Biashara ya Home delivery inachangamoto sana hasa wateja wanapo kuwa ni Wabongo wenzetu.
Inahitaji moyo sana kufanya hii biashara na wabongo make kuna changamoto sana.
Changamoto kubwa sana ni mtu ku cancel oda dakika za majeruhi, au kupunguza quantity, au kupeleka mzigo na simu anazima.
Kuna wakati nilikuwa nafanya Delivery ya kuku walio chinjwa kwa kweli nilienjoy sana kwa Wahindi na Wazungu na nilikuwa napata shida sana kwa Wabonho wenzangu.
Swala la unapigiwa simu uandae kuku labda watatu then baada ya lisaa unaambia sory nitachukua wawili tu make nimepata dharura mtoto kauhua ghafla ilikuwa ni jambo la kawaida sana.
Siku nyingine unaandaa unapeleka na simu inazimwa mtu hapatikani kabisa na mwanzo alikuwa anasisitiza sana upeleke.
Siku nyingine unapewa oda baadae anakuambia tualishe nimepata safari ya ghafla sana au mtoto kaugua ghafla naenda hospitali.
Au unapeleka anatafuta sababu ili asichukue au unafikisha anakuambia amepungukiwa hela hivyo pesa nyingine atanimalizia wakati mwingine.
Au unapelea tna unafika swala la bei mnaanza tena ku negotiate upya na mwanzo alikuwa anajua bei.
Ila kwa Wahindi sikuwahi kukutana na Changamoto ya kwamba usilete tena mara sijui punguza idadi.
Kufanya delivery na wabongo wenzetu labda cash kwanza kitu ambacho pia huwa ni kigumu sana.
Hii ni kwa vitu vingi sana na wanao fanya hizi Biashara watakuwa nimashahidi wa usumbufu wanao upata