Changamoto za Duka la rejareja

Changamoto za Duka la rejareja

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Huu ni uzi maalumu wa kuelezea changamoto wanazopitia wafanyabiashara wa Maduka ya Rejareja almaarufu "Maduka ya Mangi".

Kama una Changamoto yoyote unayopitia andika hapa, hata kama wateja wanakukosea pia ongea hapa.

Asante.
 
Kuna jamaa yangu mmoja ana Duka mahali, katika kupiga stori akaniambia biashara ya Uchuuzi ni Changamoto sana kwenye jamii yetu.

Mteja hanunui vitu kwako, anakuja mara mojamoja tena baada ya siku kadhaa!. Mteja Ananunua bidhaa Duka la jirani akikosa bidhaa ndio anakuja dukani kwako.

Mteja kama huyo anaomba umkopesha, unamwambia sikopeshi anakwambia mbona wenzako wanakopesha.

Hiyo ni moja ya Changamoto kwenye biashara ya Uchuuzi almaarufu Maduka ya Rejareja.
 
Wateja wengi wa hivyo ni matapeli, ukishamkopesha humuoni
 
Ninayo app nzuri ya kupiga mahesabu ya duka.Inafaa kutumia wakati wa kufanya stock.
1.Unaweza kujua duka lako limekuingizia sh. kwa mwezi au kwa mwaka.
2. Inaonyesha thamani stock iliyopo dukani
3. Inaonyesha Kila bidhaa unayouza Ina faida ya sh. ngapi
4. Kama Kuna upotevu wa fedha inaonyesha.

INAFAA KUTUMIA KWENYE SMART PHONE AU COMPUTER

Ili kuitumia unatakiwa kuwa na rekodi sahihi za Kila manunuzi na mauzo ya Kila siku. Nicheki Whatsapp 0753546162
 
Back
Top Bottom