eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,356
- 16,379
kwa mbaali naanza kuelewa kuhusu HISA lakin sasa unafaidika je sasa wewe unaenunua kwa mfano mimi na HISA 10% CRDB hyo asilimia nazinunua kwa shiling ngap na nakuwa napata kiac gan per certain timeKwa tafsiri lahisi HISA ni kumiliki. Mtu akisema anamiliki Hisa basi huwa anamiliki kampuni ambayo amenunua hisa. Ile hela unayonunua hisa ni hela inayoenda kuchangia mtaji.
Katika kununua Hisa ni vizuri ukaangalia yafuatayo :
1. Menejimenti ya kampuni :- Kufanikiwa kwa kampuni yoyote sokoni ni matokeo ya menejimenti nzuri. Kampuni ambayo haina menejimenti nzuri ima itadumaa au thamani ya hisa zake itakuwa ya kusuasua sokoni. Mfano CRDB.
2.Taswira ya kampuni katika jamii (Goodwill). Kuna kampuni ambazo taswira yake katika jamii si nzuri hili husababisha ufanisi wake usiwe mzuri sokoni.
3.Mipango ya maendeleo ya Taifa. Ni vizuri ukitambua kampuni inaakisi vipi au inaingia vipi kwenye mipango ya Taifa. Serikali ni mmoja wa wateja wakubwa na kama kampuni unayoenda kununua hisa zake inajishughulisha na mambo ambayo ni kipaumbele cha serikali ni lahisi HISA za kampuni hiyo kupanda thamani.
4. Je, shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ni kwa kiasi gani zimelifikia soko? Katika kila watanzania 100 wenye uhitaji wa huduma za benki ni 20 tu waliofikiwa, kwa tafsiri hiyo soko la benki lina nakisi kubwa ya huduma. Mtu anunua hisa kwenye taasisi ya fedha ambayo ni makini uhakika wa kupata faida ni mkubwa.
5. Fuatilia vizuri umiliki wa soko wa kampuni husika na mikakati yake ya baadae. Mfano shirika la Bima la Taifa linamiliki soko kwa chini ya 10% kutoka kumiliki 100%. Kununua hisa kwenye kampuni ya aina hii kunahitaji kujua mipango na mikakati yao ya Muda wa kati na mrefu ili kujiridhisha.
Mengine nitaelezea baadae kwa kadri ya maswali yako.
mkuu mimi nataka za nmb hizi walizotangaza juzi........faida na hasara zake plizNadhani ungepata msaada mzuri kama ungesema umepanga kununua hisa toka kampuni ipi, inaonekana ushafanya chaguzi
mkuu nmb wanauza hati fungani laki5.........utofauti wa hisa na hati fungasni ni nini????????Ingia mtandaoni jielimishe mwenyewe kwanza ili hata mtu akileta uzoefu wake upate cha kulinganisha. Pia kuna hati fungani (treasury bills?) ambazo nadhani ni salama zaidi kuliko hisa. Ingia website ya BoT ujielimishe. NMB pia nimeona wanauza. Nenda huko DSE au kwa wakala yeyote ukiwa na mwanga kidogo. Hongera kwa kufikiria kuwekeza.
kwa mbaali naanza kuelewa kuhusu HISA lakin sasa unafaidika je sasa wewe unaenunua kwa mfano mimi na HISA 10% CRDB hyo asilimia nazinunua kwa shiling ngap na nakuwa napata kiac gan per certain time
mkuu sasa nmb wanauza hati fungani kwa laki5.......na faida ni 13% inakuaje hii????????????Naomba nijibu kwa mfano. Benki ya CRDB inaweza kuwa na hisa milioni 2 ambazo zimeuzwa na kila hisa ina thamani ya Tsh 300. Ili umilikiki 10% ya hisa zake utachukua 10% ya 2 milioni ambayo ni hisa 200000. Utachukua Tsh 300 kwa kila hisa mara hisa 200000 na utapata Tsh 60 mil. Kwa maana hiyo unahitaji Tsh 60 mil kumiliki 10% ya hisa za CRDB.
Faida utakayopata
1. Gawio.
Hesabu za kufunga mwaka zikifanyika na CRDB ikapata faida. Mfano milioni 2,000/=. Kikao cha wanahisa hukaa kuamua faida itakayogawiwa kwa wana hisa iwe kiasi gani. Wakiamua milioni 1,000 zigawiwe, unachukua hiyo 1 bilioni unagawa kwa milioni 2 ambayo ni Tsh 500 kwa kila hisa. Kwa kuwa wewe una hisa 200,000 basi unachukua 200,000 mara 500 ambayo ni Tsh mil 100.
2. Thamani ya hisa kupanda.
Unaweza kununua hisa kwa Tsh 300 kampuni ikafanya vizuri sokoni baada ya Miaka 3 thamani ikawa Tsh 800. Kwa hiyo ukiziweka hisa zako sokoni unapata faida.
Dhamana.
Hisa hutumika kama dhamana ya mkopo katika baadhi ya taasisi za kifedha. Kwa maana hiyo badala ya kuweka nyumba au gari unaweka hisa zako
Tutaendelea kwa kadri ya maswali.
Nimekuelewa vizuri mkuu nashukuru sana kwa msaada wako sasa sina budi kuifatilia hii ninayotaka kwenda kununua hisaKwa tafsiri lahisi HISA ni kumiliki. Mtu akisema anamiliki Hisa basi huwa anamiliki kampuni ambayo amenunua hisa. Ile hela unayonunua hisa ni hela inayoenda kuchangia mtaji.
Katika kununua Hisa ni vizuri ukaangalia yafuatayo :
1. Menejimenti ya kampuni :- Kufanikiwa kwa kampuni yoyote sokoni ni matokeo ya menejimenti nzuri. Kampuni ambayo haina menejimenti nzuri ima itadumaa au thamani ya hisa zake itakuwa ya kusuasua sokoni. Mfano CRDB.
2.Taswira ya kampuni katika jamii (Goodwill). Kuna kampuni ambazo taswira yake katika jamii si nzuri hili husababisha ufanisi wake usiwe mzuri sokoni.
3.Mipango ya maendeleo ya Taifa. Ni vizuri ukitambua kampuni inaakisi vipi au inaingia vipi kwenye mipango ya Taifa. Serikali ni mmoja wa wateja wakubwa na kama kampuni unayoenda kununua hisa zake inajishughulisha na mambo ambayo ni kipaumbele cha serikali ni lahisi HISA za kampuni hiyo kupanda thamani.
4. Je, shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ni kwa kiasi gani zimelifikia soko? Katika kila watanzania 100 wenye uhitaji wa huduma za benki ni 20 tu waliofikiwa, kwa tafsiri hiyo soko la benki lina nakisi kubwa ya huduma. Mtu anunua hisa kwenye taasisi ya fedha ambayo ni makini uhakika wa kupata faida ni mkubwa.
5. Fuatilia vizuri umiliki wa soko wa kampuni husika na mikakati yake ya baadae. Mfano shirika la Bima la Taifa linamiliki soko kwa chini ya 10% kutoka kumiliki 100%. Kununua hisa kwenye kampuni ya aina hii kunahitaji kujua mipango na mikakati yao ya Muda wa kati na mrefu ili kujiridhisha.
Mengine nitaelezea baadae kwa kadri ya maswali yako.
Na mimi ndicho ninachosubiri kwenye gawiwo ni kila mwaka au inakuaje na hiyo faida ni sawa na shilingi ngapiwadau kuna tofauti gani kati ya hati fungani na hisa??????????
na je mfano wanauza hati fungani kwa 500000 huko nmb,.wanasema faida yake ni 13% hii ndo inakuAje????????????
tunaomba elimu wadau mupo kimya kweliiii
mkuu kuna uzi humu jamaa kaelezea vizuri ngoja nikupe mlink,.nikuvuteNa mimi ndicho ninachosubiri kwenye gawiwo ni kila mwaka au inakuaje na hiyo faida ni sawa na shilingi ngapi
Asante sana mkuu nazidi kufunguka kichwa kuhusu hisaNaomba nijibu kwa mfano. Benki ya CRDB inaweza kuwa na hisa milioni 2 ambazo zimeuzwa na kila hisa ina thamani ya Tsh 300. Ili umilikiki 10% ya hisa zake utachukua 10% ya 2 milioni ambayo ni hisa 200000. Utachukua Tsh 300 kwa kila hisa mara hisa 200000 na utapata Tsh 60 mil. Kwa maana hiyo unahitaji Tsh 60 mil kumiliki 10% ya hisa za CRDB.