Changamoto za hisa mwenye kuzijua tafadhali

Mfano mimi nataka kununua hisa 7000 kwa sh 3500000 je kwa mwaka ni faida gani napata kutokana na hii hela ninayoenda kuinunulia hisa

Na mimi ndicho ninachosubiri kwenye gawiwo ni kila mwaka au inakuaje na hiyo faida ni sawa na shilingi ngapi
Uwekezaji katika Bond au Hati fungani ni aina ya uwekezaji ambao imekuwepo kwa muda mrefu sana katika nchi mbalimbali,

Hata hivyo hapa nchini kwetu dhana hii ya uwekezaji bado inaonekana kwa ni ngeni miongoni mwa watu wengi

Bondi au Hati fungani ni nini?

Ni uwekezaji ambapo mwekezaji anaikopesha serikali au kampuni, na serikali hiyo au kampuni inaahidi kumlipa mwekezaji huyo baada ya hatifungani hiyo kukomaa,

Kwa kawaida faida inayoambatana na uwekezaji katika bond hugawiwa kila baada ya miezi 6.

Benki ya NMB ambayo ndiyo the most profitable bank, na ndiyo benki iliyo sambaa zaidi nchini Tanzania kwa sasa imetangaza uuzaji wa hatifungani yake, ambapo imeanza kuuzwa kutoka tarehe 10 May na itauzwa hadi tarehe 8 June 2016, kupitia madalali 10 wa soko la Hisa la Dar es salaam Mfano Arch Financials & Investments Advisory Limited wanaopatikana katika jengo la NIC life house lililopo mtaa wa sokoine posta jijini Dar es salaam, (Tel:+25522732922396,Mob: 0784952814) au Kupitia Tawi lolote la NMB lililo karibu nawe

Kwa Kiasi kidogo tu cha uwekezaji cha shillingi laki tano (500,000) unapata faida ya asilimia 13% kwa mwaka kwa muda wa miaka mitatu ambapo faida hii inakuwa inalipwa mara mbili kwa mwaka, bila kusahau kuwa bondi itakapo komaa "mature" NMB itakulipa pesa yako yote uliyokuwa umewekeza awali

Hati fungani hii ya NMB walengwa wakuu ni wawekezaji wadogo na wakati, japo hata wakubwa hawajazuiwa na ndiyo maana kiwango cha chini cha uwekezaji ni Tsh 500,000/= Tu na kuendelea, tofauti na Bondi nyingine za makampuni zilizo wahi tokea hapa Tanzania

Chukulia kama umewekeza Shillingi 1,000,000 kwa riba ya 13% kwa mwaka, hivi ndivo itakavyokuwa

1.Interest=Principal*Rate* Time

=1,000,000*13/100*1year

=Shillingi 130,000

2.Lakini interest hii inalipwa mara mbili kwa mwaka hivyo malipo ya mkupuo wa kwanza yatakuwa ni TZS130,000/2 =TZS 65,000/=

3.Kila mkupuo wa malipo unatozwa kodi ya zuio ya 10%

=65,000-(65000*10%)

=65,000-6,500

=TZS 58,500

Hivyo kufikia Disemba 2016(baada ya miezi 6) utapokea Shillingi 58,500

4.Baada ya miaka 3, uwekezaji wako katika hatifungani hii utakuwa umekuingizia Shillingi 351,000 (58,500*6) kutoka katika uwekezaji wako wa Shillingi 1000,000. Shullingi 1M yako itakwa imekuwa hadi kufikia shillingi 1,351,000 pasipo wewe kufanya chochote, umeingiza pesa hizi ukiwa umekaa tu nyumbani au upo kwenye shughuli zako nyingine.

Isitoshe endapo utapata dharura, kabla miaka mitatu haija isha,na ukahitaji hizi pesa zako bado una nafasi ya kupata pesa zako ulizo wekeza , ambapo utaweza ku uza hatifungani hii katika soko la Hisa la Dar es salaam, kupitia madalali wake

source,.

copied from Copy1

Nimeitoa sehemu guys

Source : TzInsight
Sasa mbona kama faida ndogo sana kwenye hati fungani? hiyo milioni 1 nikiianzishia biashara kwa kipindi hicho cha miezi 6 si nitakua nimevuka hiyo faida ya 351000?

kuwa wazi unanunua hisa za kampuni gani itakuwa rahisi kukushauri vinginevyo utanunua hisa sehemu mbaya , broker anaweza kukushauri ununue hisa sababu ukinunua kuna faida na yeye anapata , kama unaona ni private sana fanya PM nitakushauri bure.

yaani nimegundua mkuu ni biashara ya ulaghai,..haina tija kwa mtu binafsi,.
Biashara hii ugumu ni kwenye kuchagua kampuni na muda gani utakaa na hizo hisa, nina hisa nimenunu kampuni moja tofauti ya bei niliyonunulia na nitakayouza kama ni leo ni shilingi 6200/- . Lakini imechukua muda kufikia bei hiyo hapo inamaana kwa kila hisa moja nitakayouza sasa nina faida ya 6200 plus na kwa dividend ninazochukua ni kuwa hela yangu imerudi .Kuchagua kampuni tu ndio shida.

2171753475617225216

kuwa wazi unanunua hisa za kampuni gani itakuwa rahisi kukushauri vinginevyo utanunua hisa sehemu mbaya , broker anaweza kukushauri ununue hisa sababu ukinunua kuna faida na yeye anapata , kama unaona ni private sana fanya PM nitakushauri bure.
Mkuu ni DSE nataka kujua mfano nikinunua hisa 7000 kwa sh/ 3500000 ni gawio gani nitapata kwa mwaka? Please help me

Kabisa mkuu yaani m 1 kwa miezi 6 faida 351000 tu hii sio nzuri hii hati fungani inanyonya
mkuu kwa msingi wa mil1 unaweza kufanya wonders ndani ya mwaka na kupata zaidi ya mil1 nyingine......
mkuu b4 nilikuwa najua nikiwekeza kwenye hii biashara ya hati fungani baada ya mwaka nashindana na dangote au manji,..kumbe ni ujingaujinga2,.mabank na wafanya biashara wengine huwa hawajali maisha ya wengine,hua wanadili na kupata profit kubwa2 basi,.haijalishi pesa ya masikini au lahhhh
nimeshaachana na hii idea yani........bora nifuge kuku tu

Mkuu ni DSE nataka kujua mfano nikinunua hisa 7000 kwa sh/ 3500000 ni gawio gani nitapata kwa mwaka? Please help me
Gawio linatofautiana kati ya kampuni na kampuni kampuni inaweza kutangaza gawio labda la shilingi hamsini kwa kila hisa hivyo wewe kwa hisa zako elfu saba utapata 50*7000 = 350,000 , gawio linaweza kutolewa mara moja au marambili kwa mwaka. na kwa upande wa hati fungani ni kwamba wakitanganza rate yao ni 13 % ina maana kwa mwaka utapata faida asilimia 13 ya gharama ya hati fungani uliyonunua . Na ukienda DSE hununui hisa za DSE unanua hisa za kampuni iliyosajiliwa DSE , sasa na kampuni ni nyingi nyingine ni hasara tu huwezi pata la maana ndio maana nakwambia taja kampuni unayonunua hisa zake kama ni CRDB ,NMB , SWISS , ACA vinginevyo kama hauna uhakika unanunua hisa kwenye kampuni gani unaweza omba usaidiwe pia .

wadau kuna tofauti gani kati ya hati fungani na hisa??????????
na je mfano wanauza hati fungani kwa 500000 huko nmb,.wanasema faida yake ni 13% hii ndo inakuAje????????????
tunaomba elimu wadau mupo kimya kweliiii

Kuna mtu kasema "Hii nimeikopi sehemu" maelezo katika andiko lake yanefafanua vizuri ila naomba kuongezea.

Kwanza Hati fungani ni aina ya mkopo ambayo "mdogo" anamkopesha mkubwa kama ilivyo kwa NMB. Tofauti ya Hati na hisa.
1. Hati Fungani ina ukomo hisa haina ukomo. Mfano mzuri ni ni Hati Fungani za NMB, hizi unawakopesha hela ndani ya Miaka 3 na baada ya hapo pesa unarudishiwa. Ukinunua hisa za NMB wewe ni mmiliki na umiliki wako ni wa milele ima NMB wafirisike au kwa hiari yako uuze hisa zako.

2. Faida ya Hati Fungani inafahamika tangu awali na kipindi cha kuchukua hela zako kinajulikana (mature). Gawio la hisa hutegemea zaidi ufanisi wa kampuni husika na maamuzi ya wanahisa. Kama kampuni inapata hasara au ipo kwenye "break even point" Ni ngumu kupata Gawio.

3.Uwekezaji wa Hati Fungani japo una faida "kiasi" kwa kiwango kikubwa unakuepusha na hasara. Kwenye hisa "ukichemsha" katika kuchagua kampuni ya kuwekeza fedha yaweza zama.

Mifuko hii ya pesa imeonyesha tija na ufanisi mkubwa katika nchini zilizo na maendeleo kwa sababu kwa kiasi kikubwa wanafuata sheria na "rushwa haijatamalaki"

Gawio linatofautiana kati ya kampuni na kampuni kampuni inaweza kutangaza gawio labda la shilingi hamsini kwa kila hisa hivyo wewe kwa hisa zako elfu saba utapata 50*7000 = 350,000 , gawio linaweza kutolewa mara moja au marambili kwa mwaka. na kwa upande wa hati fungani ni kwamba wakitanganza rate yao ni 13 % ina maana kwa mwaka utapata faida asilimia 13 ya gharama ya hati fungani uliyonunua . Na ukienda DSE hununui hisa za DSE unanua hisa za kampuni iliyosajiliwa DSE , sasa na kampuni ni nyingi nyingine ni hasara tu huwezi pata la maana ndio maana nakwambia taja kampuni unayonunua hisa zake kama ni CRDB ,NMB , SWISS , ACA vinginevyo kama hauna uhakika unanunua hisa kwenye kampuni gani unaweza omba usaidiwe pia .
Kuna wakala pale wa TIB nilimpigia simu akanitaka nifike ofisini kwao ili tuongee kiukweli bado sijaamua ni kampuni ipi ninunue hisa ndio maana pia kama ningefaamishwa vizuri kuhusu hisa za kampuni ingenisaidia sana
Maana nimeambiwa DSE kuna hisa na moja inauzwa sh/ 500 sasa nashindwa kuelewa nianzie wapi
Na nimeambiwa nifike ofisini kwao karibu na sant joseph pale

Kuna mtu kasema "Hii nimeikopi sehemu" maelezo katika andiko lake yanefafanua vizuri ila naomba kuongezea.

Kwanza Hati fungani ni aina ya mkopo ambayo "mdogo" anamkopesha mkubwa kama ilivyo kwa NMB. Tofauti ya Hati na hisa.
1. Hati Fungani ina ukomo hisa haina ukomo. Mfano mzuri ni ni Hati Fungani za NMB, hizi unawakopesha hela ndani ya Miaka 3 na baada ya hapo pesa unarudishiwa. Ukinunua hisa za NMB wewe ni mmiliki na umiliki wako ni wa milele ima NMB wafirisike au kwa hiari yako uuze hisa zako.

2. Faida ya Hati Fungani inafahamika tangu awali na kipindi cha kuchukua hela zako kinajulikana (mature). Gawio la hisa hutegemea zaidi ufanisi wa kampuni husika na maamuzi ya wanahisa. Kama kampuni inapata hasara au ipo kwenye "break even point" Ni ngumu kupata Gawio.

3.Uwekezaji wa Hati Fungani japo una faida "kiasi" kwa kiwango kikubwa unakuepusha na hasara. Kwenye hisa "ukichemsha" katika kuchagua kampuni ya kuwekeza fedha yaweza zama.

Mifuko hii ya pesa imeonyesha tija na ufanisi mkubwa katika nchini zilizo na maendeleo kwa sababu kwa kiasi kikubwa wanafuata sheria na "rushwa haijatamalaki"
Nini kinachangia hela yako ipotee wakat umenunua hisa? Je ni kampuni gani zinafaa kununua hisa bila kua na wasiwasi?

Kuna wakala pale wa TIB nilimpigia simu akanitaka nifike ofisini kwao ili tuongee kiukweli bado sijaamua ni kampuni ipi ninunue hisa ndio maana pia kama ningefaamishwa vizuri kuhusu hisa za kampuni ingenisaidia sana
Maana nimeambiwa DSE kuna hisa na moja inauzwa sh/ 500 sasa nashindwa kuelewa nianzie wapi
Na nimeambiwa nifike ofisini kwao karibu na sant joseph pale
wewe nenda kaongee naye ila kabla hujanunua rudi tena hapa tunaweza wekana sawa kabla hujafanya maamuzi ila hisa za kampuni ambayo bei yake ni 500 ninazozijua hazifanyi vizuri

hati fungani(bonds) hii ni aina ya uwekezaji anayoifanya mtu kuelekea kwenye kampuni au taasisi kwa msingi wa kuikopesha kampuni au taasisi hiyo ambayo ina uhitaji wa kuongezea mtaji wake kwa makubaliano ya kipindi maalumu kwa maana ya muda na riba ya mkopo ambayo inaweza kubadilika au isibadilike kwahiyo unaposikia kampuni inauza hati fungani maana yake inataka mkopo kutoka kwako .
sifa za hati fungani tofauti na hisa
1. hati fungani hukwatwa kodi zinapoiva tofauti na hisa.
2. hati fungani haikupi sifa ya kumiliki kampuni tofauti na hisa.
3. hatakuwa na maamuzi yoyote juu ya taasisi hiyo kushuri n.k

Nini kinachangia hela yako ipotee wakat umenunua hisa? Je ni kampuni gani zinafaa kununua hisa bila kua na wasiwasi?
kinachoweza kuchangia fedha zako kupotea ni uwezo wa kampuni kuzalisha faida pale kampuni itakapokosa faida na ikapekea kutumia mtaji wako (yaani hisa yako)kulipia shughuli sizizo za uzalishaji utapoteza fedha zako.
kuhusu ni kampuni gani ya kununua hisa fanya utafiti wa kampuni gani ina mzunguko mkubwa wa fedha na bidhaa zake kwenye jamii zinahitajika sana

Asante nashukuru sana mkuu nitayafanyia kazi god bless you

Back
Top Bottom