H
Wana jf nimeamua kwa mara ya kwanza katika maisha yangu kua nataka kununua hisa za sehemu fulan sasa ninachoomba msaada kwenu ni kuhusu changamoto zake au hasara zake kuhusu faida nimezisikia nyingi ila nataka kujua hasara inakuja wakati gani maana najua hakuna biashara isio na hasara
Kiukweli nimeamua kununua hisa kwa mara ya kwanza na wapi pa kuanzia nimepewa kila kitu na nimeambiwa nakaribishwa ofisini muda wowote
Wana jf hasa wenye uelewa na hisa naomba msaada wenu
Nawasilisha asanteni nitashukuru kama mkinisaidia hili
Hisa/Shares
Unaponunua hisa unakuwa umenunua kipande cha kampuni, kwa mfano kama kampuni imetoa hisa 1,000,000 na unanunua hisa 1,000 basi unamiliki 0.1% ya kampuni.
- Nini kinasababisha bei kupanda/kushuka:
Bei ya hisa inatokana hasa na fikra za soko kuhusu kampuni itafanya nini huko mbele i.e itaweza kukua au itabaki ilipo au kurudi nyuma.
E.g. Hisa za kampuni ya Apple zinashuka hivi sasa pamoja ya kwamba ndo moja ya makampuni makubwa na yenye faida zaidi duniani, hii ni kwa kuwa wawekezaji wanahofia Apple haina sehemu inayoweza kukuza soko lake huko mbeleni na haina bidhaa mpya itakayokamata soko.
- Unapataje faidi kwa kununua hisa?:
Faida ya hisa zinaweza kutoka sehemu mbili, kupanda kwa thamani ya hisa i.e umenunua hisa kwa Tsh 500/each lakini baada ya miaka miwili hisa hiyo ina thamani ya 1,000/each.
Kupata gawio/dividends; Kampuni inaweza kuamua kutoa gawio kutokana na faida zake kwa wanahisa. E.g. kwa kila hisa moja kampuni inaweza kuamua kutoa gawio la TSH 90 (NMB) so kama una hisa 1,000, hiyo ni 1,000 X 90 = 90,000 kabla ya makato ya kodi (5%).
HAKUNA HAKI YA GAWIO! Kampuni inaweza kuamua kutotoa gawio hata kama imepata faida maradufu, gawio linatokana na maamuzi ya Bodi ya kampuni na si wanahisa, hivyo bodi ina haki ya kutotoa gawio au kupunguza/kuongeza gawio.
- Nitapata faida kiasi gani nikinunua hisa?:
Hauwezi kujua! Kwa vile faida za hisa zinatokana na jinsi soko lilivyo/litakavyokuwa hauwezi kujua utapata kiasi gani cha faida/hasara huko mbeleni.
Unaweza kujaribu kuotea kwa kuangalia historia ya hisa, ila wataalamu wanasema "Past Performance is Not Necessarily Indicative of Future Results".
- Napataje hasara na hisa?:
Hasara kwenye hisa unapata pale thamani ya hisa yajo itakaposhuka kwenye soko i.e umenunua hisa kwa 1,000/each baada ya mwaka hisa ina thamani ya 500/each, hapo inakuwa sio tu haujapata faida bali hata ule mtaji wako/principle umeliwa kwa 50%!
Pia kampuni ikifilisika unakuwa umepoteza investment yako yote.
Hati fungani/BONDS
Unapoweka hela zako katika Bond unakuwa umeikopesha kampuni au serikali kama ni bond za serikali.
- Unapataje faidi kwa bond?:
Faida ya Bond inatokana na riba/rate iliyowekwa na kampuni/serikali wakati wanaiuza hiyo bond, na muda wa hiyo bond, kwa mfano NMB wametangaza bond ya 13% kwa miaka 3, basi faida yako itakuwa ni 13% kwa mwaka ya kiasi ulichoweka (minus kodi)
e.g Umeweka 1,000,000 basi utapata 1,000,000 X 0.13 = 130,000 kwa mwaka au 130,000 X 3 = 390,000 kwa miaka mitatu ya hiyo bond (minus tax). Na mwisho wa muda utarudishiwa mtaji/principle yako (1,000,000).
- Nitapata faida kiasi gani nikinunua bond?:
Angalia mahesabu hapo juu, faida inatokana na makubaliano ya rate na muda wa bond hivyo unaweza kujua utakuwa na kiasi gani mwisho wa siku.
- Napataje hasara na bond?:
Kwa vile bond haitegemei soko bali inategemea makubaliano ya awali njia pekee ya kupata hasara katika bond ni kufilisika kwa kampuni au kwa serikali na kushindwa kulipa madeni yake.
Ndo maana unaweza ukaona faida ya bond ni ndogo ukifananisha na biashara kwa vile ni very low risk na passive yaani haihitaji kufuatiliwa.